Jukumu la Maendeleo ya Mtanzania ni letu sote

Jukumu la Maendeleo ya Mtanzania ni letu sote

Joined
Jun 11, 2021
Posts
6
Reaction score
1
Kama tukitambua kuwa kama wananchi tuna majukumu kadhaa ya kuweza kusaidia kuinua uchumi wa serikali yetu na kusaidia katika ukusanyaji wa kodi. je ni wangapi hukumbuka kudai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali au kupata huduma?

Je, tunafahamu ni kiasi gani tunajiibia kwa kutokuwa tayari kudai risiti halali na pia kuwafaidisha wafanyabiashara wasio waaminifu? Watanzania tunapaswa kuanza uzalendo kwanza sisi kama wananchi halafu tuweze dai kwa watendaji wasio wazalendo.

Kodi ni kwa maendeleo ya taifa.
 
Wabunge watuongoze kulipa Kodi za mishahara yao (payee),lasivyo iwekwe Sheria kabla hujawa mbunge ni lazima upitie JKT kujifunza Uzalendo Kama wafanyavyo wanaotaka kwenda vyuo😁😁

Tulipe kodi,tuijenge nchi yetu
Wabunge mtuongoze.
 
Mishahara ya wabunge, kiinua mgongo na malupulupu yao yakatwe kodi kubwa zaidi.
Wasomi wa hii nchi wako mstari wa mbele kuelewa hizo kodi mpya kwamba ni ngumu kupata vyanzo vipya vya mapato...wakisahau kuna mishahara isiyokatwa kodi, kuna exemptions kibao tu.

Wasomi ni rahisi zaidi kudanganyika na kutawalika.
 
Wananchi tunaplay part yetu vizuri, viongozi nao wanapaswa kuplay part yao vyema, cha kwanza wawe wawazi ktk matumizi ya Kodi zetu, na pia wasiwe wakali tunapohoji matumizi ya Kodi zetu.
 
Jukumu letu sawa, ila tunaowalipa ni wajibu wao watutumikie badala yake wanatunyonya sioni value ya our hard earned cash...
 
Uwepo na usawa pia kwenye mishahara na posho sio wengine Wafalme wengine watumwa huku kodi tunalipa sawa.
 
Inasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
 
Back
Top Bottom