View attachment 3304077
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima mara baada ya kukamilika kwa zoezi la Vyama vya Siasa kutia saini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Mwaka 2025 alisema, kati ya Vyama 19 vilivosajiliwa ni Chama kimoja tu cha Siasa ambacho hakikuitikia wito wa INEC.
"Bahati nzuri tumepata Vyama 18, mosi vimeridhia maadili hayo na pili vimesaini maadili hayo, ni chama kimoja tu ambacho hakijahudhuria na kusaini maadili hayo, sasa hatma ya chama ambacho hakijasaini maadili hayo ni kutopata fursa ya kushiriki Uchaguzi" alisema Kailima akifanya mahojiano Maalum na Shirika la BBC ofisini kwake jijini Dodoma.
Aliongeza kuwa, siyo kwamba hawatashiriki Uchaguzi wa mwaka huu, bali hawatashiriki Chaguzi nyingine ndogo katika muda wa miaka mitano.
Akijibu Hoja iliyoitaka Tume kuitisha Mkutano wa kujadili Sheria za Uchaguzi, alisema Tume haiwezi kuitisha Mkutano wa kujadili Sheria kwa kuwa siyo jukumu wala mamlaka ya Tume (INEC) kutunga Sheria. Aliongeza, Sheria hutungwa na Bunge na INEC wanabaki kama watekelezaji huku Mahakama ikiwa na jukumu la kutafsiri Sheria hizo.