Jukwa hili vipi?

Jukwa hili vipi?

mambucha

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
279
Reaction score
160
Kuna miswada mitatu ya sheria iko bungeni, lakini sijaona hata thread moja kwenye hili jukwaa kuhusiana na hili naona inajadiliwa kwenye jukwaa la siasa. Vp wanasheria chambueni hii miswada hapa jukwaani nini tafsiri yake kwa maslahi mapana ya nchi?

Parliament of Tanzania
 
Kuna miswada mitatu ya sheria iko bungeni, lakini sijaona hata thread moja kwenye hili jukwaa kuhusiana na hili naona inajadiliwa kwenye jukwaa la siasa. Vp wanasheria chambueni hii miswada hapa jukwaani nini tafsiri yake kwa maslahi mapana ya nchi?
Weka hiyo miswaada hapa kwan hatujaipata. hatuwezi kutoa maoni kwa mihemko/povu ya itikadi fulan.
 
  • Thanks
Reactions: sab
Ndio aiweke ichambuliwe fasta
 

Attachments

Attachments

BAADHI YA MAMBO YALIYOPENDEKEZWA KWENYE MISWAADA NI HAYA.

1. Mabadiliko ya sheria inataka Katika Uwekezaji kwenye sekta ya madini endapo kutatokea sintofahamu yeyote basi kesi zote zitaamuliwa na mahakama za ndani ya nchi ya Tanzania.

2 . Mabadiliko ya sheria ya madini yanafanya serikali kumiliki madini share kiasi cha 16% bila kutoa fedha Taaslim kwa kuwa yenyewe inamiliki madini na ndio mtaji wake kwa kila mwekezaji...

3 . kama ilivyo kwenye mafuta kuna EWURA basi na mabadiliko ya sheria yanapendekeza kuanzishwa chombo kama hicho ili kuongeza jicho la usimamiaji..

4. Kwenye mabadiliko haya kutakuwa na Uanzishwaji wa hifadhi ya dhahabu na madini ya Vito vya thamani itakayokuwa Benki kuu ya Tz..

5 . Bunge limepewa uwezo wa kupitia mikataba ya madini na maliasiri za Nchi na kupendekeza mabadiriko kama itakuwa mibovu..

6. Theruthi 3 ya mrahaba italipwa kwa serikali kwa njia ya madini na si fedha Taaslim na kuwekwa B.O.T moja kwa moja..

7. Sheria inataka kila mwenye mgodi kuanzisha sehemu salama ya kuhifadhi makinikia na madini kabla ya kupelekwa kwenye maghala ya serikali yakisubilia kuchenjuliwa.

8. Mabadiliko ya sheria inasema madini yote ni mali wananchi na serikali imemilikishwa na wananchi ili iweze kuyasimamia hivyo hakuna tena kampuni itakayoweza kumiliki madini ila serikali tu.

9. Mabadiliko ya sheria inasema Mauzo yote ya madini yatatakiwa kuwekwa hapa kwenye mabenki ya kizalendo Tanzania na fedha zitakazoruhusiwa kutoka nje ni zile za gawio lao tu si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom