Kibamba anasema kwa kua kuna wabunge wanatembea na bastola hadharani na kwa kua bungeni wanasema wazi wazi kwamba wanaharakati wapewe adhabu.. basi polisi itoe ulinzi kwa wananchi dhidi ya hawa wabunge
amenifurahisha mwanadada mmoja toka gongo la mboto amemunga mkono chadema kutoka nje.Kibamaba aukubali uamuzi wa chademakutoka nje asema Ndiyo njia inayotumiwa hata na nchi za nje. Amesema wabunge wa chadema HAwakuwa tayari kuonekana wasaliti mbele ya wananchi kwa kupitisha mswada wa kihuni
Kuhusiana na Chadema kutoka nje' kibamba anasema hata kimataifa wabunge huwa wanatoka nje kupinga jambo fulani,hvyo anasema ni haki yao,yeye anadhani ingekuwa ni usaliti kwa wananchi waliosema wanataka wawaone wabunge ambao wapo upande wao.
mwananchi aponda tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa katiba kwani tayri ina shutuma nyingi.
Jukwaa nalo laipinga NEC yataka tume ya mpito iratibu upigaji kura, washangaa serikali imekataa hilo, washangaa serikali hii iko tanzania kweli maana yanyotakiwa serikali haifanyi
kibamba apongeza wananchi kwa kuamka kudai na kufatilia haki zao. asema watanzania wanataka mabadilko co mapinduzi kama ya libya. Asisitiza watawatangaza wote wanaopinga katiba mpya na watawapa pia Vyeti vyeusi
Hata hao jukwaa la katiba porojo nyingi hakuna kitu waoga tu'wanajf wote tunaopinga huu muswada feki wa katiba tuingie road tuache pc zetu kwa muda tufikishe ujumbe kwa hao tuliowapa kazi naona kazi imewashinda hatuna budi kuwafukuza