Jukwaa la Kuni Mtoni Kijichi

Jukwaa la Kuni Mtoni Kijichi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
LINGO LA KUNI MTONI KIJICHI
Inaweze kufika zaidi ya miaka 60 nilikuwa sijaona lingo la kuni.

Katika utoto wangu nikikua Dar es Salaam kulikuwa na malingo nengi ya kuni sehemu zikiwekwa kuni nyingi kwa ajili ya kuuzwa.

Lingo ninalolikumbuka mimi lilikuwa Gerezani hapa ambapo hivi sasa ni sehemu ya viwanda vidogovidogo.

Katika miaka ya 1950 sehemu hii kati ya Mtaa wa Mbaruku na Kisarawe palikuwa na lingo kubwa ikiwekwa miti ya kila aina kwa ajili ya ujenzi na mingine kuni za kupikia chakula.

Saad Juma Mzee mmoja wa Waafrika tajiri na mtu maarufu Dar es Salaam alikuwa na lingo kubwa la kuni.

Miaka ili Saad Juma Mzee alikuwa mmoja wa viongozi wa Sunderland Football Club baadae ikaitwa Simba.

Lingo la kuni ilikuwa sehemu muhimu ya nishati kwani ndiko palipopatikana kuni kwa ajili ya kupikia na pia miti kama mikoko kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

Leo nimeliona lingo lakini Mtoni Kijichi.

Umeme upo, mafuta ya taa yapo na halikadhalika gesi lakini kuni za kupikia nazo bado zipo.

Lingo la kuni Mtoni Kijichi limenilumbusha mbali sana.


View: https://youtu.be/nev16P-fe-k?si=cSjTTMoJFK8_3pz1
 
Sasa hivi wanataka kutukata kutumia ma lingo yetu ya kuni eti tutumie gesi wanatuhaminisha kwamba gesi ni nafuu sijui kwanini tusipikie umeme; Nina uhakika katika makuzi yako ulitumia umeme na kuwasha taa za watt 100 iweje leo ishindikane ?
 
Ukiingia Mbagala (Rangi 3 na Mbagala kuu/Kijichi), Buguruni, Kiwalani, Tandika, Buza, Gongo la mboto (Mazizini).

Malingo ya kuni yapo ya kutosha.
Wanatumia kukaangia samaki, dagaa, mihogo na kupikia pombe.
 
Back
Top Bottom