Jukwaa la ma-CEO lasisitiza ushirikiano kulinda biashara dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi

Jukwaa la ma-CEO lasisitiza ushirikiano kulinda biashara dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Jukwaa la Watendaji Wakuu Tanzania (CEOrt) limetoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kulinda biashara na shughuli za kiuchumi dhidi ya majanga yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi yanayoongezeka.

Akizungumza katika mkutano wa wanachama wa CEOrt Oktoba 17, 2026, chini ya kaulimbiu "Zaidi ya Utabiri: Kujenga Ustahimilivu Dhidi ya Hatari za Tabianchi", viongozi wa kibiashara walisisitiza haja ya kugeuza utabiri wa hali ya hewa kuwa hatua za vitendo, kuboresha miundombinu na kuimarisha maandalizi ili kupunguza hasara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Dkt. Obinna Anyalebechi, alisema taarifa za hali ya hewa zina thamani tu pale zinapotafsiriwa kuwa maamuzi yanayolinda maisha ya watu, biashara na mazingira.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a, alisema kuunganisha utabiri wa msimu kwenye mipango ya kiuchumi kunaweza kusaidia sekta kama kilimo, usafirishaji, utalii na viwanda kutarajia hatari na kupunguza athari zake.
PICHA TMA.jpg

Wakati huo huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Paul Deogratius, alitoa wito wa masuala ya mazingira kuingizwa kwenye mipango ya maendeleo ya Taifa chini ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.
 
Back
Top Bottom