Jukwaa La Mapishi, Food Corner

Jukwaa La Mapishi, Food Corner

Sita Sita

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2008
Posts
1,397
Reaction score
520
Hello Mods

I think you will agree with me kwamba hamna kitu muhimu hapa duniani kama Kula (apart from Praying and Believing in your Religions)

Watu wa dini na makabila tofauti wanaweza kuunganishwa na chakula.

Chakula kina part yake kwenye mapenzi.

Chakula ni symbol tosha ya utamaduni wa mtu.

Kuzingatia hayo.

Naomba mods muanzishe jukwaa maalum kwa ajili ya watu kuweka Recipes mbalimbali. Wengi humu ndani hatujui utundu wa kuandaa chakula. Itakua vizuri sana kama hili jukwaa litakuwepo ili tuweze kushare experience.

Wengine tunakula mikate kila siku kwa kuwa hatujui namna ya kuandaa breakfast mbalimbali.

Nawasilisha
image.php

Wana'JF Wote wenye kupenda kula na kunywa kwa Afya Bora, hapa ndio sehemu yako. Wote mnakaribishwa ili kubadirishana uzowefu wa MAPISHI, Mahanjumati na Makulaji.Jisikie Huru Kushirikiana na kila mwanachama katika kuboresha LISHE Bora.Aina zote za Mapishi yatapatikana hapa.ShukraniKaribuni Wote WanaJF
________________________________

Virutubisho Vinavyopatikana Katika Vyakula

Mwili wa binadamu (na viumbe vingine hai) ili uweze kukua na kunawili unahitaji vitu vinavyojulikana kama virutubisho au viinirishe. Kwa lugha ya kigeni virutubisho vinaitwa "Nutrients". Virutubisho hivyo vinapatikana katika vyakula mbalimbali.

Vile vile tunajuwa kuwa, virutubisho vyote hugawanywa katika makundi makuu sita, ambayo ni kabohaidreti (wanga, sukari na nyuzi nyuzi), protini, mafuta, vitamini, maji na madini (minerals). Ili mwili uweze kukua na kunawili vizuri lazima upate virutubisho vyote.

Chakula (kama cha asubuhi, mchana, jioni au usiku) chenye virutubisho vyote sita hujulikana kama mlo kamili au "balanced deit" kwa lugha ya Waingereza. Kwa vile takribani vyakula vyote tunavipata kwa gharama kubwa (fedha au kazi), swala la uchaguzi wa vyakula haliepukiki.

Pia unategemea mazoea ya mlaji, radha na sura ya chakula, virutubisho na mambo kadhaa wa kadhaa. Ili kufikia uchaguzi sahihi wa vyakula, elimu ya chakula gani kina virutubisho gani ni ya msingi. Jukwaa La Mapishi, (Food Coner) linakusudia kukidhi haja hiyo kwa wasomaji wote. Katika kukidhi haja hiyo, vitataja aina ya chakula, virutubisho vya msingi na virutubisho vya ziada vinavyopatikana katika vyakula hivyo.

Nafaka:
Nafaka ni vyakula vya punje punje au chembechembe kama vile mtama, mahindi, ngano, uwele (mawele), mpunga n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula vya nafaka ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni Protini, vitamini (kundi la B) na baadhi ya madini.

Vyakula jamii ya mizizi na matunda:
Vyakula jamii ya mizizi (starchy roots) ni kama vile viazi (vitamu, mviringo, n.k) mihogo, n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula jamii ya viazi na matunda ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi (dietary fibres). Zaidi ya virutubisho hivyo ni baadhi ya madini, vitamini C (kama chakula hicho siyo kikavu) na vitamini A (kama chakula hicho kinarangi ya njano).

Vyakula jamii ya maharage:
Vyakula jamii ya maharage nikama vile maharage ya kawaida na yale ya soya, kunde, choroko, n.k. Virutubisho vya muhimu katika kundi la vyakula vya hapo juu ni wanga, protini na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni vitamini (kundi B) na madini.

Mbegu za mafuta:
Mbegu za mafuta ni kama vile alizeti, pamba, ufuta, nazi, mawese (chikichi), kweme, maboga, tikiti maji, matango, n.k. Virutubisho vinavyopatikana kwa wingi katika mbegu za mafuta ni mafuta, protini na nyuzi nyuzi. Ziada kundi B. (B- Vitamins).

Nyama/Samaki:
Virutubisho vya msingi katika nyama au samaki ni protini, mafuta na madini ya chuma. Virutubisho vingine ni vitamini vya kundi B na madini (zaidi ya yale ya chuma).

Ini:
Ini linatupa virutubisho vya msingi vya protini, madini ya chuma na vitamini.

Maziwa:
Virutubisho tunavyovipata kwa wingi katika maziwa ni mafuta, protini, baadhi ya madini na vitamini.

Mayai:
Mayai yana virutubisho vya msingi vya protini na vitamini. Zaidi ya hivyo ni mafuta na madini (siyo ya chuma).

Mafuta:

Mafuta kama chakula yanatupa mafuta kama kirutubisho cha msingi. Zaidi ya hicho ni uwezekano wa kupata vitamini A.

Mboga za majani:
Mboga za majani hasa zile za kijani zinavirutubisho vya msingi vya vitamini A, C na B, Zaidi ya hivyo ni protini, madini na nyuzi nyuzi.

Matunda jamii ya machungwa:
Matunda jamii ya machungwa ni machungwa, machenza, n.k virutubisho vya msingi tunavyovipata kutoka katika matunda jamii ya machungwa ni sukari, vitamini A na C. Zaidi ya hivyo ni madini na nyuzi nyuzi.
 
Nilwahi kuona mtu mmoja alitoa maoni kama haya sijui iliishia wapi. MODs tusaidieni
 
Jamani majukwaa yatakuwa mengi, haya tu yaliyopo mengine hayana wachangiaji!
 
mi naona ingewekwa kama sub-forum kwenye jukwaa la JF Doctor........:tongue:

tukianzia hapa hapa.....hebu tuanze na makange.......dude nalipenda kweli ila sijui linapikwaje vile......
 
He! Kuna group la mapishi. Na mimi ni mwanachama ila kumedoda huko.
 
mi naona ingewekwa kama sub-forum kwenye jukwaa la JF Doctor........:tongue:

tukianzia hapa hapa.....hebu tuanze na makange.......dude nalipenda kweli ila sijui linapikwaje vile......

Dah umenikumbusha makange ya Rose Garden na Club ya Salenda wanapika hii kitu sijawahi kuona nimejaribu nimeshindwa
 
Hello Mods

I think you will agree with me kwamba hamna kitu muhimu hapa duniani kama Kula (apart from Praying and Believing in your Religions)

Watu wa dini na makabila tofauti wanaweza kuunganishwa na chakula.

Chakula kina part yake kwenye mapenzi.

Chakula ni symbol tosha ya utamaduni wa mtu.

Kuzingatia hayo.

Naomba mods muanzishe jukwaa maalum kwa ajili ya watu kuweka Recipes mbalimbali. Wengi humu ndani hatujui utundu wa kuandaa chakula. Itakua vizuri sana kama hili jukwaa litakuwepo ili tuweze kushare experience.

Wengine tunakula mikate kila siku kwa kuwa hatujui namna ya kuandaa breakfast mbalimbali.

Nawasilisha

Wazo zuri sana,itatusaidia na mabachelor pia
 
Jamani majukwaa yatakuwa mengi, haya tu yaliyopo mengine hayana wachangiaji!

Yes yatakuwa mengi,ila kuna majikwaa mimi sioni umuhimu wake kwa sasa mfano:-
1.Dini/Imani (hili jukwaa la kukwazana kiimani sio kukuzana,halifai)
2.Mambo ya kikubwa
3.Matangazo madogo madogo
4.Jamii photos

Kama majukwaa yatakuwa mengi basi moja kati ya haya yaondolewe ila priority ni kwa hayo mawili ya kwanza
 
Dah umenikumbusha makange ya Rose Garden na Club ya Salenda wanapika hii kitu sijawahi kuona nimejaribu nimeshindwa

hao hapo kwenye blue ni kiboko hasa la kuku unaweza ukazimia kwa utamu

waungwana,mwenye recipe yake atupe basi
 
Yes yatakuwa mengi,ila kuna majikwaa mimi sioni umuhimu wake kwa sasa mfano:-
1.Dini/Imani (hili jukwaa la kukwazana kiimani sio kukuzana,halifai)
2.Mambo ya kikubwa
3.Matangazo madogo madogo
4.Jamii photos

Kama majukwaa yatakuwa mengi basi moja kati ya haya yaondolewe ila priority ni kwa hayo mawili ya kwanza

labda la dini, lakini hayo mengine ni burudani hasa hilo nililobold na blue........ngoja wenye jukwaa wakusikie
 
hao hapo kwenye blue ni kiboko hasa la kuku unaweza ukazimia kwa utamu

waungwana,mwenye recipe yake atupe basi

mhandisi,,kuja pande hii nikupe hiyo maneno ingawa bado nna hasira,,lolz:nod:
 
labda la dini, lakini hayo mengine ni burudani hasa hilo nililobold na blue........ngoja wenye jukwaa wakusikie

Hahaha,ila kama watataka kutoa moja basi watoe la dini,wakitaka kutoa mawili watoe dini + jukwaa la wakubwa!

Me nilikuwa natembelea huko lakini duh,ni balaa
 
Hahaha,ila kama watataka kutoa moja basi watoe la dini,wakitaka kutoa mawili watoe dini + jukwaa la wakubwa!

Me nilikuwa natembelea huko lakini duh,ni balaa

Maria Rosa, Mchonga, El-Toro n.k wataua mtu mkitoa jukwaa la wakubwa. Kwenye dini sijui kama Max Shimba, Marytina Gavana et al watawaelewa...
 
Kuhusu jukwaa la mapishi naunga mkono hoja, mwenzenu kila siku naunguza...
 
Back
Top Bottom