Jukwaa La Mapishi, Food Corner

Jukwaa La Mapishi, Food Corner

Maria Roza, Mchonga, El-Toro n.k wataua mtu mkitoa jukwaa la wakubwa. ...

Labda ni njama ya kuwafukuza jamvini, kwao ni bora hata jukwaa la siasa liondoke.
ila wavumao baharini papa kumbe.....
 
Labda ni njama ya kuwafukuza jamvini, kwao ni bora hata jukwaa la siasa liondoke.
ila wavumao baharini papa kumbe.....

Sigma wa ukweli, as long as kila mtu ana interest zake na majukwaa yako active, let them stand still, au?
 
ninavyopenda kura!!.ntaanza kuwapima kwa ubora wa kupika siyo rongolongo za ailavuyu.
nimeipenda hii ya mapishi.mia
 
nachukia kupika,unatu100 masaa 3 kukipika chakula lkn utatumia dk 3 kukila! Ila napenda sana kula
 
Uenikumbusha hii kitu,nia siku sijatia timu mitaa ya Rose Garden.Tam sana....
 
image.php
Wana'JF Wote wenye kupenda kula na kunywa kwa Afya Bora, hapa ndio sehemu yako. Wote mnakaribishwa ili kubadirishana uzowefu wa MAPISHI, Mahanjumati na Makulaji.Jisikie Huru Kushirikiana na kila mwanachama katika kuboresha LISHE Bora.Aina zote za Mapishi yatapatikana hapa.ShukraniKaribuni Wote WanaJF
________________________________



Virutubisho Vinavyopatikana Katika Vyakula

Mwili wa binadamu (na viumbe vingine hai) ili uweze kukua na kunawili unahitaji vitu vinavyojulikana kama virutubisho au viinirishe. Kwa lugha ya kigeni virutubisho vinaitwa "Nutrients". Virutubisho hivyo vinapatikana katika vyakula mbalimbali.

Vile vile tunajuwa kuwa, virutubisho vyote hugawanywa katika makundi makuu sita, ambayo ni kabohaidreti (wanga, sukari na nyuzi nyuzi), protini, mafuta, vitamini, maji na madini (minerals). Ili mwili uweze kukua na kunawili vizuri lazima upate virutubisho vyote.

Chakula (kama cha asubuhi, mchana, jioni au usiku) chenye virutubisho vyote sita hujulikana kama mlo kamili au "balanced deit" kwa lugha ya Waingereza. Kwa vile takribani vyakula vyote tunavipata kwa gharama kubwa (fedha au kazi), swala la uchaguzi wa vyakula haliepukiki.

Pia unategemea mazoea ya mlaji, radha na sura ya chakula, virutubisho na mambo kadhaa wa kadhaa. Ili kufikia uchaguzi sahihi wa vyakula, elimu ya chakula gani kina virutubisho gani ni ya msingi. Jukwaa La Mapishi, (Food Coner) linakusudia kukidhi haja hiyo kwa wasomaji wote. Katika kukidhi haja hiyo, vitataja aina ya chakula, virutubisho vya msingi na virutubisho vya ziada vinavyopatikana katika vyakula hivyo.

Nafaka:
Nafaka ni vyakula vya punje punje au chembechembe kama vile mtama, mahindi, ngano, uwele (mawele), mpunga n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula vya nafaka ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni Protini, vitamini (kundi la B) na baadhi ya madini.

Vyakula jamii ya mizizi na matunda:
Vyakula jamii ya mizizi (starchy roots) ni kama vile viazi (vitamu, mviringo, n.k) mihogo, n.k. Virutubisho vya msingi vinavyopatikana katika vyakula jamii ya viazi na matunda ni wanga, sukari na nyuzi nyuzi (dietary fibres). Zaidi ya virutubisho hivyo ni baadhi ya madini, vitamini C (kama chakula hicho siyo kikavu) na vitamini A (kama chakula hicho kinarangi ya njano).

Vyakula jamii ya maharage:
Vyakula jamii ya maharage nikama vile maharage ya kawaida na yale ya soya, kunde, choroko, n.k. Virutubisho vya muhimu katika kundi la vyakula vya hapo juu ni wanga, protini na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni vitamini (kundi B) na madini.

Mbegu za mafuta:
Mbegu za mafuta ni kama vile alizeti, pamba, ufuta, nazi, mawese (chikichi), kweme, maboga, tikiti maji, matango, n.k. Virutubisho vinavyopatikana kwa wingi katika mbegu za mafuta ni mafuta, protini na nyuzi nyuzi. Ziada kundi B. (B- Vitamins).

Nyama/Samaki:
Virutubisho vya msingi katika nyama au samaki ni protini, mafuta na madini ya chuma. Virutubisho vingine ni vitamini vya kundi B na madini (zaidi ya yale ya chuma).

Ini:
Ini linatupa virutubisho vya msingi vya protini, madini ya chuma na vitamini.

Maziwa:
Virutubisho tunavyovipata kwa wingi katika maziwa ni mafuta, protini, baadhi ya madini na vitamini.

Mayai:
Mayai yana virutubisho vya msingi vya protini na vitamini. Zaidi ya hivyo ni mafuta na madini (siyo ya chuma).

Mafuta:

Mafuta kama chakula yanatupa mafuta kama kirutubisho cha msingi. Zaidi ya hicho ni uwezekano wa kupata vitamini A.

Mboga za majani:
Mboga za majani hasa zile za kijani zinavirutubisho vya msingi vya vitamini A, C na B, Zaidi ya hivyo ni protini, madini na nyuzi nyuzi.

Matunda jamii ya machungwa:
Matunda jamii ya machungwa ni machungwa, machenza, n.k virutubisho vya msingi tunavyovipata kutoka katika matunda jamii ya machungwa ni sukari, vitamini A na C. Zaidi ya hivyo ni madini na nyuzi nyuzi.
 
Saratani ya tumbo ni tatizo linalotishia maisha ya watu kama zilivyo aina nyingine za kansa. Wataalamu wanasema kwamba katika nchi ambayo vyakula vya kila siku vya watu ni vile vilivyohifadhiwa kwa madawa (preservatives), vyenye chumvi (nyingi) na vilivyosindikwa (Pickled foods), idadi ya watu wenye ugongwa wa salatani ya tumbo huwa ni kubwa.

Ukweli wa jambo hilo uko wazi zaidi katika nchi za Asia Mashariki, ambayo wananchi wake wanatumia zaidi vyakula vya aina niliyoitaja hapo juu. Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2008, kansa ya tumbo ndiyo iliyokuwa inaongoza kwa kuua watu wengi zaidi ikilinganishwa na aina nyingine za kansa. Hata hivyo, wataalamu hao wanasema kuwa, katika miaka 25 iliyopita, ugonjwa wa kansa ya tumbo duniani umepungua kwa asilimia sitini (60%). Hii ni kwa sababu ya teknolojia ya kuhifadhi vyakula kwenye majokofu (refrigeration). Vyakula vikihifadhiwa kwenye majokofu (ubaridi) huweza kukaa siku nyingi bila ya kuharibika. Kwa hiyo, mahitaji ya kuhifadhi vyakula kwa kutumia njia zenye kusababisha kansa (kama njia ya kuweka madawa, chumvi, moshi, n.k.) yanapungua.

Ili kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tumbo hasa inayosababishwa na vyakula tunavyokula, watu lazima wazingatie ushauri wa lishe ufuatao:

Kwanza
, watu waache kula vyakula vilivyohifadhiwa kwa kutumia madawa hasa ‘nitrites’ na ‘nitrates’. Katika utumbo wa mwanaadamu, madawa hayo yanapambana na vitu vingine vijulikanavyo kama ‘aminesi’. Kutokana na mapambano hayo vitu vyenye kusababisha kansa hutokea. Vitu hivyo vinaitwa ‘nitrosamines’. Siku hizi ni jambo jepesi kununua vyakula visivyokuwa na ‘nitrites’, ‘nitrates’ na madawa mengine ya hatari.

Jambo la kufanya ni kusoma ‘lebo’ kabla ya kununua chakula chochote kilichotengenezwa (kiwandani).

Pili, epuka vyakula vyote vilivyohidhiwa kwa kutumia chumvi na kukaushwa kwa moshi kama vile sausage. Vile vile epuka kula mara kwa mara aina ya vyakula vijulikanavyo kama ‘pickled foods’.

Tatu, watu waepuke kula kila siku vyakula vilivyokaangwa kwa mafuta au vile vilivyookwa kwa kutumia oven (grilled foods). Hii ni kwa sababu njia hizo za kutayarisha vyakula zinasababisha nyama na samaki kutoa vitu vinavyosababisha kansa ya tumbo. Hivyo basi, ni vema watu wakapendelea vyakula vya asili na vile vilivyopikwa au kuokwa kwa njia ambazo si za hatari. Nne, watu wajitahidi kula vyakula vyenye vitamini A, B na C na pia vyenye madini ya ‘selenium’. Kwa ushahidi wa utafiti, vitu hivyo (vitamini na madini) vinasaidia kuzuia kutokea kwa kansa.
 
x-paster, asante sana! nilikuwa sijatumia mtindi ku-marinade kuku! kesho mpango mzima,lol!
 
Back
Top Bottom