Jukwaa la wafanyakazi huru (freelancers marketplace) kwa Afrika linaweza kushamiri?

Jukwaa la wafanyakazi huru (freelancers marketplace) kwa Afrika linaweza kushamiri?

Maxwell Makware

New Member
Joined
Nov 3, 2017
Posts
4
Reaction score
5
Nauliza kama jukwaa au soko la freelancers au wafanyakazi huru linaweza kua na tija au uhitaji kwa Africa mashari au hata Africa kwa ujumla. Kwa kiasi flani watu wengi naona wako Fiverr, Upwork etc ambayo ni makampuni ya Marekani au ughaibuni huko.

- Najua vijana wanahitaji na wako tayari kujiajiri kama wafanya kazi huru, ama kazi pekee au kama kazi ya ziada.

- Ambacho sina hakika ni makampuni na taasisi kama yako tayari au ulazima kuweza tumia platforms kama hiyo.

Niko na project kama hiyo lakini nikaona nipate maoni ya wadau mbalimbali hapa jukwaa la jamii.

Nikipata mawazo pia kutoka kwa wadau walio na mamlaka ya kutoa kazi za muda mfupi na ambazo zinaweza fanyika ofisini moja kwa moja au remotely itapendeza sana.

Asanteni...
 
Salaam,

Naomba nijikite Tanzania.

Ni wazo zuri sana ingawa kuna changamoto ya Watanzania wengi kutokuwa exposed kuhusu suala zima la gig economy.

Kwa kudhani tu, sina hakika kama 10% ya graduates wa Bongo wana ufahamu wa hizo freelancing platforms za kimataifa kama Upwork, Fiverr, Flexjobs, Toptal n.k. Ukiuliza utajibiwa ukimya au siasa.

Tupo tunaosaka kazi kwa miaka na mikaka tukisaga mbuga na bahasha za khaki tusijue kuna gig economy. Hata hivyo, wapo wachache wanaishi mjini kwa namna hiyo.

Lakini pia, huenda utamaduni wa ku-outsource haujasambaa sana kwenye makampuni na mashirika ya hapa kwetu. Na hata kama utamaduni upo; je, wanatazama upande huo kupata huduma zao?

Hivyo basi, kama mpango ni kuanzisha hapa Tanzania, nadhani kuna kazi kubwa ya kuelimisha watu waelewe unachomaanisha.

Tanzania tayari kuna the likes of Worknasi, GigSpace [Tanzania] nk. Unaweza kupata mwanga kidogo kwa kutazama muitikio wa wananchi kwa hayo majukwaa. Ila usiishie hapo.
 
Nilikua na wazo sawia na lako miaka 3 nyuma.

Tayari kuna kampuni zinafanya kitu hicho hapa Bongo kama mdau hapo juu alivyoeleza.

Changamoto ya hii kitu bado ni utamaduni unaokua taratibu sana hapa kwetu.

Unachoweza kufanya ni kuja na njia bora za kuwapiku washindani wako. Naamink ukifanya deep research utakuja na kitu bora zaidi na kuleta mageuzi.

Kila la heri!
 
Asante sana mdau, umenipanua mawazo kwa undani sana. Nadhani moja kubwa kabisa ni kama ulivyo sema hapo juu; tamaduni za ku-outsource huduma kwa makambuni na taasisi haujawa na mwamko au bado haujapata mhamasishaji na muelimishanji.

Kuh graduates kua na awareness sidhani kama ni tatizo, mwenyewe umusema kwamba vijana/graduates na wenye taaluma mbalimbali wanasota miaka wakiwa na bahasha mikononi kutafuta ajira na vibarua. So focus kubwa ni kuelimisha makampuni, taasisi kua kuna kazi/ projects zinaweza kua outsourced kwa individual, kampuni au kwa kikundi.

Pia kwa mawazo yako hapo juu, inamanisha kunahitajika uwekezaji uli oserious zaidi hasa kwe elimu na awareness( Hard Cash ku facilitate kama ni seminars na aina nyingine za promos kwa ma executives na project decision makers)

Asante sana, acha nikae niendelee kuweka mambo sawa.
Kama una mawazo karibu sana chief, tunaweza badilishana mawazo.
 
Nilikua na wazo sawia na lako miaka 3 nyuma.

Tayari kuna kampuni zinafanya kitu hicho hapa Bongo kama mdau hapo juu alivyoeleza.

Changamoto ya hii kitu bado ni utamaduni unaokua taratibu sana hapa kwetu.

Unachoweza kufanya ni kuja na njia bora za kuwapiku washindani wako. Naamink ukifanya deep research utakuja na kitu bora zaidi na kuleta mageuzi.

Kila la heri!
Maridhawa kabisa na ninafurahi kupata mawazo kutoka kwa mtu aliye jaribu. Karibu sana.
Maswali yangu kwako:
>Ulipoona soko gumu ukaachana na idea yako?
>Nini kilikurudisha nyuma kabisa?
>Tusubiri mtu mwingine aanzishe njia au tuendelee na hali taratibu mpaka kieleweke?
>Kama uliachana na idea yako miaka 3 iliyopita, leo tena ungepata nafasi ya kufanya maamuzi kama yale, bado ungeamua kama ulivyo amua miaka 3 nyuma au ungebadiri majibu?

Chief asante sana kwa mchango wako... asante sana..
 
Hawa freelancer unataka kuwa kwa kazi ipi inayofikiria.zipo kampun. ziwatumia kwa ajili ya mauzo ya nidhaa zao wanazozalisha na kuwapa malengo ya siku pamoja na mwezi
 
Shida ni kwamba upwork na hao wenzake wapo kwenye first world countries ambako uchumi ni mkubwa kwa hiyo ni rahisi kumwambia clients wa nchi husika kuwa anaweza kutafuta labour kwa Bei ya chini kabisa na kazi ikawa poa Sasa kwa sisi tz clients anatakubali ku mlipa Bei ileile ambayo angemlipa ambaye anamuona labda clients atoke tz hafu worker awe burundi
 
Back
Top Bottom