Jukwaa la Wahariri Tanzania latoa tamko kwa Haji Manara kutokana na kumdhalilisha Prisca Kishamba

Jukwaa la Wahariri Tanzania latoa tamko kwa Haji Manara kutokana na kumdhalilisha Prisca Kishamba

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitishwa na linalaani kitendo cha Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kumdhalilisha Mwandishi wa Habari wa Radio Clouds FM, Prisca Kishamba.

Udhalilishaji huo ulioambatana na maneno ya kashfa dhidi ya Prisca, ulifanywa na Msemaji huyo wa Simba kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Juni 30, 2021, katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ulizungumzia mchezo wa Ligi Kuu ya Bara baina ya timu ambazo ni watani wa jadi; Simba na Yanga.

Kauli za vitisho vya Manara ni mwendelezo wa tabia na mwenendo wake dhidi ya Waandishi wa Habari ambao wamekuwa wakiripoti habari za Klabu ya Simba kwa maslahi mapana ya umma na Sekta ya michezo kwa ujumla.

Tukio la Juni 30 dhidi ya Prisca na Waandishi wa Habari wengine walipokuwa wakiuliza maswali kwenye mkutano huo, linafikirisha na linatufanya tutafakari ikiwa ni sahihi kwa vyombo vya habari kuendelea kuripoti habari zinazitolewa na Klabu ya Simba kupitia kwa Msemaji wake huyo.

Kimsingi vitendo vya aina hii vinavyofanywa na Haji Manara kwa Waandishi wa Habari siyo vya kiungwana na havivumiliki hata kidogo.

Wakati waandishi wa habari wanapokuwa kazini mara zote tumekuwa tukiwahimiza kufuata maadili ya kazi zao, vivyo hivyo kwa watoa habari wanapaswa kuwa waungwana hata pale wasipotaka kuyasikia maswali wasiyoyapenda.

Kwa tamko hili, tunamtaka Manara aache mara moja tabia ya kutumia mikutano ya Klabu ya Simba kwa Waandishi wa Habari na hata mitandao ya kijamii kuwadhalilisha wanahabari.
 
Duh hizi Political Correctness going Mad...., Wewe mwandishi sometimes unajua kabisa unakutana na vichaa lazima uwe na ngozi ngumu au vipi badilisha kazi au badala ya kuwahoji wadau wa michezo wafuate Masheikh, Mapadri na Viongozi wa nchi...

Bora msema hovyo anayesema anachokifikiri kuliko mnafiki anayesema kile unachotaka kukisikia..., (Hawa wangekutana na kina Sir Alex Ferguson si wangelia kabisa)
 
Hivi Kuna mtu hapa bongo kwenye sector ya michezo ayanetaniwa na kusemwa vibaya na kudhalilishwa kama haji Manara?
Kina shafii Dauda walikia hatua ya kuposti kwenye account zao za mitandao ya kijamii picha za Nguruwe wakimaanisha Haji ni Nguruwe je yeye alishitaka popote au kuna tamko lilitolewa?

Kuna mapicha kibao wame edit mitandaoni humu Haji kawekewa mi shape ka mwanamke mbona yeye halalamiki wala kushtaki mtu?
Kuwena wavumilivu kama yeye alivyo pia.
 
Hawajielewi hao wao kuisema simba ovyo ovyo wako sahihi wakigiswa wanajificha kwenye kivuri cha uwanahabari taka taka zote izo
 
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitishwa na linalaani kitendo cha Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kumdhalilisha Mwandishi wa Habari wa Radio Clouds FM, Prisca Kishamba..
Huyo jamaa HAJI MANARA anajiona yuko JUU YA KILA mwanadarisalama.

Huyo jamaa HAJI MANARA anajiona yuko JUU YA KILA MTANZANIA.

Binafsi ninamuona ni "MSHAMBA SMART" tu.

Haji Manara ana POST TRAUMATIC STRESS DISORDER(PTSD) labda kwa sababu ya "CHILDHOOD ABUSE".....pengine...Who knows?!!!

Haji Manara ana "GRANDIOSITY".....he is GRANDIER DELUDED.

MPENI MSAADA.

TUMUONEE HURUMA.

Hakika jamaa "ako" na matatizo "mazee".....🤣

POLE SANA DADA WA NGUVU PRISCA KISHAMBA.....

#WeAreWithPriscaKishamba
#HajiManaraApelekweMuhimbiliKamaJonasMkude
 
Hivi Kuna mtu hapa bongo kwenye sector ya michezo ayanetaniwa na kusemwa vibaya na kudhalilishwa kama haji Manara?
Kina shafii Dauda walikia hatua ya kuposti kwenye account zao za mitandao ya kijamii picha za Nguruwe wakimaanisha Haji ni Nguruwe je yeye alishitaka popote au kuna tamko lilitolewa?.....
Tofautisha mtu kumtania haji manara na pres conference ni vitu viwili tofauti
 
Hivi huyo prisca kishamba ni shabiki wa Simba au yanga? Tuanzie hapo maana hawa waandishi waone hivi hivi tu.
 
Hivi Kuna mtu hapa bongo kwenye sector ya michezo ayanetaniwa na kusemwa vibaya na kudhalilishwa kama haji Manara?
Kina shafii Dauda walikia hatua ya kuposti kwenye account zao za mitandao ya kijamii picha za Nguruwe wakimaanisha Haji ni Nguruwe je yeye alishitaka popote au kuna tamko lilitolewa...
Hajji mvumilivu?
 
Utopolo mtupu na shule za kuunga unga kwa madesa.

Wewe uliyeletwa mjini na TCU unawezaje kumwita mtoto wa Kariakoo mshamba?

Sina uhakika kama una exposure ya jiji lolote duniani zaidi ya Dar tu ulipoletwa na TCU
Huyo jamaa HAJI MANARA anajiona yuko JUU YA KILA mwanadarisalama.

Huyo jamaa HAJI MANARA anajiona yuko JUU YA KILA MTANZANIA...
 
Huyu wangemsusia hizo press conferences za Simba. Ndio maana hawezani na mtu yoyote. Hata hii familia mpya sasa hivi itaamsha virago vyake. Amenyimwa busara kabisa.
 
Back
Top Bottom