Jukwaa limechafuka, tulisafishe

canfi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,368
Reaction score
1,477
Ukifuatilia michango ya members hapa jukwaani utagundua kuwa wengi hawana vifua vya kuvumilia hoja au mada zenye habari/ujumbe wenye mlengo tofauti na timu zao ktk kipindi husika. Matokeo yake ni kujaa kwa matusi na dhihaka.

Nashauri tujikite kujadili mada kwa hoja na sio mihemko/uhayawani. Vinginevyo tunalichafua jukwaa hili muhimu. Kama huna cha kuandika ni bora ukae kimya au usome michango ya wenye akili timamu.
 
Nitaandika kwa hekima na tafakuri jadidi lakini bado nitahakikisha maslahi kwa timu yangu ya Mnyama yanazingatiwa na kulindwa vilivyo..!

Mara moja moja nitawatania Yanga kama mtani na timu pinzani ya SIMBA ila sitaweza kuweka dhihaka za kukera maana michezo no furaha.. Michezo inatuunganisha imani zetu, itikadi zetu na asili zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utani si kitu kibaya. Lkn kuandika kwa makusudi ya kukera ni mbaya sana.
 
Kuna kipindi timu yako ikiwa inapata au kukosa matokeo uwe makini ku comment.
Simba tangu msimu umeanza imekua ikipata matokeo kutokana na mapungufu ya maamuzi, hali kama hii ilianza kwenye ngao ya jamii mpaka sasa.
Huwezi kusema ni bahati mbaya kwa mechi zaidi ya nne.
Haiwezi kuwa bahati mbaya kwa timu kufunga magoli ya offside lakini na yenyewe iyo timu ikifungwa magoli halali yanakua offside.

Sisi kama wadau tunacho hitaji ni fair play, Simba wasionewe wala asi bebwe.
Ata kama ita bebwa bado haita weza kutwaa ubingwa kwakua inamapungufu mengi zaidi ni marefa kudhalilika.
 
Sawa Mkuu. Kikubwa busara iwepo kwenye michango yetu. Tuache matusi hasa pale timu zetu zinapopata matokeo (bila kujali yamepatikanaje)
 
Hapa ndipo penye tatizo kwa wengi kushindwa kutofautisha utani na dhihaka/udhalilishaji.

Unakuta mtu unaandika utani wa kawaida wenye staha lakini jitu linakuja na majibu kama vile vita maana anatukana ukoo wako mzima.
Kuna watu wa ajabu sana humu
 
Utakavyokuja na maoni yako ndio namna utajibiwa
 
"Mashabiki wa Yanga ni mambwa hakuna lolote wanalojua kuhusu kandanda ila muda wote wanazomea tu utadhani manyani"

Dr Luc Eymael 2020
 


YANGA ina Mashabiki mapumbavu.

YANGA Inaa Mashabiki wajinga.

YANGA Inamashabiki wasio na Elimu, wasiosoma na Mazuzu.
 
Hili tatizo ni la muda mrefu so jukwaa la michezo hata jukwaa la siasa.
Kuna baadhi ya watu badala ya kujadili hoja wanakimbilia matusi na mods wapo kimya.
Wanaotukana matusi ni wachache Sana lakini wameachiwa kutamba.
 
Nilitamani nianzie kufundisha hapa Jamii forum kwa maswali na majibu kuhusu......

1. Coaching.

2. MIFUMO ya mpira wa Miguu.

3. Sheria Moja Moja ya Mpira wa Miguu kwa maswali na majibu.

4. Historia ya Mpira wa Miguu.

5. Scauting ya mchezaji mzuri.

6. Elimu ya analysis ya mpira wa Miguu nk

ILA NILICHOGUNDUA MASHABIKI WENGI WA YANGA NI MAPUMBAFU NA HAYAFUNDISHIKI.
 
Daaaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…