Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa), Mhe. Juliana Didas Masaburi amefanya ziara katika Bandari ya Mtwara ambapo aliambatana na Baraza la Vijana la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara.
Katika ziara hiyo akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mtwara Komredi Abuu Athumani, Mhe. Juliana Masaburi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji wa miundombinu wa zaidi ya shilingi Bilioni 400 katika Bandari ya Mtwara, uwekezaji ambao unachochea Maendeleo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Juliana Masaburi amempongeza Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ndugu Fernand Nyati kwa kusimamia vyema Bandari ya Mtwara na kujipanga kwa maandalizi ya kusafirisha Korosho kwa kupokea Meli zaidi ya 3 zenye makasha ya kusafirisha Korosho hizo.
Naye, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mtwara, Komredi Abuu Athumani amesema wameamua kumleta Mgeni, Mhe. Juliana Masaburi kutembelea Bandari ya Mtwara ili aone uwekezaji wa Serikali na Baraza la Vijana lipate la kujifunza kupitia Bandari hiyo.
Mbunge Juliana Didas Masaburi ameenda Mtwara kwaajili ya kushiriki Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara kilichofanyika 05 Oktoba, 2024 katika Ukumbi wa Bandari ya Mtwara
Aidha, Mhe. Juliana Masaburi akiwa katika Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Mtwara ametoa kiasi cha shilingi Milioni Moja (1,000,000) na Matofali 1000 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mtwara na pia, amegawa vyeti vya pongezi kwa wadau wa UVCCM Mkoa wa Mtwara.
#KijanaNaKijani
#TunazimaZoteTunawashaKijani
#TunaendeleaNaMama.
#KaziIendelee