Juliana Shonza Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Kata ya Kalembo, Ileje

Juliana Shonza Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Kata ya Kalembo, Ileje

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

JULIANA SHONZA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KATA YA KALEMBO, ILEJE​

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya ziara ya kikazi katika Kata ya Kalembo Wilaya ya Ileje kwa lengo la kuendelea kuwainua kiuchumi wanawake kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Juliana Shonza amesema kuwa, anaendelea kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka 2020 wakati wa uchaguzi mkuu ambapo aliahidi kuwainua kiuchumi wanawake wa Mkoa wa Songwe kwa kuwapa mitaji itakayowasaidia kupata vyanzo vya mapato.

"Ni muhimu sana wanawake tuwe tunajishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya biashara, ujasiriamali, ukulima, ufugaji na ushonaji ili tuwe na mchango kwenye familia zetu na Taifa kwa ujumla" Juliana Shonza

"Mwanamke ukiwa na kipato siyo rahisi kunyanyasika lakini pia itakusaidia kutimiza ndoto zako, itakusaidia kuwalea watoto wako vizuri na kuwasomesha

Aidha, Juliana Shonza ametoa Salamu za shukurani kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa na Miaka Minne Madarakani yenye matokeo mazuri kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 hasa katika Mkoa wa Songwe kwa kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu, Madini, Utalii, Miundombinu ya usafirishaji na Maji

Vilevile, Juliana Shonza amewasihi wananchi wote wa Kata ya Kalembo, Ileje kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutoa ushirikiano kwa viongozi waliopo madarakani ili kuendelea kuleta maendeleo makubwa kwenye jamii

Pia, pamoja na mambo mengine, Mbunge Juliana Shonza amekabidhi fedha za mitaji kwenye vikundi vya ujasiriamali vya Wanawake wa Kata ya Kalembo ambao wamejiajiri akiwa na lengo la kuhamasisha wanawake kufanya kazi kwa bidii na kuwa na vyanzo vya mapato.

Mwisho; Wanawake wa Kata ya Kalembo, Ileje wamesema kuwa wameridhishwa sana na utendaji kazi wa Juliana Daniel Shonza katika kuwawezesha wanawake kiuchumi ambapo wamemmwagia zawadi za kutosha ili kumtia moyo na kuendelea kumuunga mkono.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.10.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.10.jpeg
    346.1 KB · Views: 50
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.08.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.08.jpeg
    733.3 KB · Views: 47
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.08 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.08 (1).jpeg
    418.6 KB · Views: 43
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.10.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.10.jpeg
    346.1 KB · Views: 46
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.11 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.11 (1).jpeg
    387.3 KB · Views: 41
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.12.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.12.jpeg
    393.1 KB · Views: 49
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.12 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.12 (1).jpeg
    376.5 KB · Views: 44
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.13.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.13.jpeg
    214.2 KB · Views: 44
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.07.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.07.jpeg
    608.5 KB · Views: 42
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.08 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.08 (1).jpeg
    418.6 KB · Views: 45
  • WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.09.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-19 at 08.31.09.jpeg
    359.5 KB · Views: 45
Back
Top Bottom