Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
JULIANA SHONZA NA JITIHADA ZA KUINUA UCHUMI WA WANAWAKE WILAYA YA SONGWE
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza ametembelea vikundi vya ujasiriamali vya Wanawake alivyovianzisha na kuvipa mitaji ili kuwainua kiuchumi kwa shughuli za kujiajiri wanazozifanya
Juliana Daniel Shonza ameendelea na ziara ya Kata kwa Kata ndani ya Wilaya ya Songwe ikiwa na lengo la kueleza matunda ya utekelezaji wa Ilani ya CCM (2020-2025); Uwezeshaji, kutoa hamasa na elimu ya vikundi vya ujasiriamali kwa wanawake na kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu
Awali kabla ya kuanza Ziara, Juliana Daniel Shonza alifika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe kumpa taarifa ya ziara yake ndani ya Wilaya lakini pia kupata mrejesho wa mikopo wa asilimia kumi (10%) ya namna fedha zilivyoanza kutolewa na kujua vikundi vilivyonufaika na mikopo hususani vya wanawake (4%)
Juliana Shonza amewashukuru sana wanawake wa Kata ya Ngwara wilayani Songwe kwa mapokezi mazuri na kusema hakika kazi imefanyika chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wanaendelea kujenga imani na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Vilevile, Mbunge Juliana Daniel Shonza amewashukuru wanawake wa Kata ya Udinde kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwasihi waendelee kukiamini hata kwenye uchaguzi mkuu unaokuja Mwezi Oktoba, 2025.
Attachments
-
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.25.jpeg526.8 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.25 (1).jpeg655 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.40 (1).jpeg302.5 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.40 (5).jpeg324.3 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.55.jpeg378.1 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.55 (3).jpeg335.9 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.55 (4).jpeg592.1 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.55 (5).jpeg313.5 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.55 (6).jpeg496.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 11.16.55 (7).jpeg458.3 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2025-02-26 at 13.32.35.jpeg592.1 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-02-27 at 12.13.48.jpeg458.7 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2025-02-27 at 12.13.49.jpeg437.3 KB · Views: 2