Julius Kambarage Nyerere Special Thread

Julius Kambarage Nyerere Special Thread

Sunbae

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2015
Posts
254
Reaction score
176
Habari Wakuu, lengo la uzi huu ni kukusanya taarifa nyingi kadri tunavyoweza zinazomhusu Baba wa Taifa letu na kuziweka mahala pamoja. Mnaruhusiwa kuongeza makala zake, vitabu na machapisho pia hotuba zake.

Let's Celebrate Our Founding Father.

Nyerere.png

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "baba wa taifa". Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule. Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."

Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama Waziri Mkuu, halafu kama Rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama Rais.

Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.

Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma linashughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu".

MAISHA YA MWL JK NYERERE

Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).

Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.

Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.

Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.

Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary.

Mwaka 1949 alipata [[skolashipu[[ ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).

Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.

Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.

Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.

Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.

Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.

Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi.

Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.

Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.

Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.

MAFANIKIO ALIYOYAPATA MWL JK NYERERE

Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani".

Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda.

Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).

TUZO ALIZOPATA MWL JK NYERERE

Nyerere2.PNG

RAIS WA AWAMU YA 3 BENJAMIN MKAPA AKITANGAZA KIFO CHAKE MWALIMU NYERERE.

Hii hapa chini ni video inayoonesha Makumbusho ya Butiama.

2011e34f-8700-48e5-b190-deea6fd48fe1.jpg

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Pwani waliokuwa naye bega kwa bega katika harakati za kudai Uhuru. Kutoka kushoto na sehemu aliyokuwa anaishi ni Abdallah Shomari (Tandamti No. 3), Nassoro Kalumbanya (Simba), Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo), Mtoro Ally (Muhonda), John Rupia (Misheni Kota),Julius Nyerere (Pugu Sekondari), Said Chaurembo (Congo/Mkunguni), Jumbe Tambaza (Upanga), Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
 
AUSTIN+MORRIS+A.40.JPG

Moja ya gari aliyowahi kutumia Mwl JK NYerere, gari hii ni AUSTIN MORRIS A-40

Gari aina ya Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba wa Taifa na Rais wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu Nyerere alilitumia gari hilo toka mwaka 1955 – 1960 katika shughuli mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake maarufu kwa jina la SAID TANU. Baadaye Mwalimu Nyerere alilikabidhi gari hilo kwa vijana wa TANU kwa kazi za chama kabla ya kupelekwa Makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
 
AUSTIN+MORRIS+A.40+VAN+GUARD.JPG

AUSTIN MORRIS (A-40 VAN GUARDS)

Gari aina ya Austin Morris A-40 maarufu kama Van Guards lilitengenezwa kati ya miaka ya 1945 – 1950. Gari hili lilitumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli za TANU akiwa Dar es Salaam na ziara za mikoani kuhamasisha shughuli za chama. Dereva wake alikuwa ni SAID TANU
 
ROLLS ROYCE

ROLLS+ROYCE+2.JPG

Gari aina ya ROLLS ROYCE lilitengenezwa 1938 na kuletwa na Gavana wa wakati huo Harold Mac Michael katika utawala wa wakoloni waingereza na lilitumiwa na Gavana wa mwisho kuitawala Tanganyika Sir Richard Turnbull. Rolls Royce lilitumika kupokea wageni mbalimbali waliotembelea Tanganyika wakati huo wakimwemo Rais wa zamani wa Liberia Hayati William Tubmann na Mfalme wa zamani wa Ethiopia Hayati Haille Sellasie. Gari hilo lilitumika hadi mwaka 1962 baadaye mwaka 1978 Rais wa kwanza Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere aliagiza Rolls Royce kuhamishwa toka Ikulu hadi Makumbusho ya Taifa. Kwa sasa ni sehemu ya Historia ya Taifa la Tanzania.
 
MERCEDEZ BENZ 230.6

MERCEDEZ+BENZ+230.6.JPG

Mercedez Benz 230.6 lilijulikana kama gari la jumuiya kwani lilitumiwa na Rais wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli za jumuiya Afrika Mashariki iliyoundwa mwaka 1967 na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambapo kila nchi ilikuwa na gari kama hilo. Moja ya sifa ya gari hilo kwa wakati huo ni kuwa na uwezo wa kubeba watu wengi zaidi.Uwezo wake ni kubeba marais wageni wawili, mpambe wa Rais, mwandishi habari wa Rais na Rais mwenyeji kwa mara moja. Mercedez Benz 230.6 lilikuwa na namba za kipekee ambazo ni RE-1 (yaani Royal Excellency 1).Hata hivyo Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilidumu kwa miaka 10 tu (1967 – 1977) ambapo ilivunjika kwa sababu mbalimbali. Gari hilo likapelekwa Makumbusho ya Taifa Oktoba mwaka 2002 na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
 
MERCEDEZ BENZ E 300; GARI YA MWISHO MWALIMU KUITUMIA

MERCEDEZ+BENZ+E-300.JPG

Mercedez Benz E 300 lilitengenezwa nchini Ujerumani na kununuliwa na serikali ya Tanzania Desemba 17, 1996 ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alilitumia kwa shughuli za kitaifa na binafsi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani baada ya kustaafu Urais. Mercedez Benz E-300 litaendelea kukumbukwa zaidi kwani ndilo gari la mwisho kwa Hayati Mwalimu Nyerere kulitumia enzi za uhai wake hapa nchini kwani alilitumia kwa mara ya mwisho kabisa Agosti 31,1999 akienda kupata matibabu huko nchini Uingereza. Alisafiria gari hilo kutoka nyumbani kwake Msasani hadi uwanja wa kimataifa wa Dar es Salaam (kwa sasa Mwalimu Julius Nyerere). Hata hivyo kwa MASIKITIKO MAKUBWA Baba wa Taifa hakurudi tena kulitumia tena gari hilo kwani alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas huko nchini Uingereza. MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI,AMEN. Gari lake alilotumia kwa mara ya mwisho (Mercedez Benz E 300) likatolewa na mkewe Mama Maria Nyerere kwa ajili ya kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa Septemba 24, 2004.
 
Nyerere3.png

Hili ni jumba la Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere, Butiama mkoani Mara.
 
upload_2017-4-27_12-33-14.png

Bao alilokuwa anacheza, viatu na vyombo alivyotumia Mwalimu.

Ukifika Butiama kuna bao lingine ambalo lilitengenezwa kwenye jiwe.

GRM_63.jpg
 
upload_2017-4-27_12-37-52.png

Redio na Joho alilovaa Mwalimu wakati akihitimu. Redio hii alipewa zawadi huko Ujerumani mwaka 1969
 
Kazi nzuri ila hariri kazi yako hasa sehemu uliyoandika kwamba "Mwalimu aliongoza Tanganyika kama Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1961-1964"
Hapo si kweli aliongoza mwaka 1960-1961 kabla ya kung'atuka. 1962 Akawa rais wa Jamhuri ya Tanganyika mpaka 1964. Baada ya muungano mwaka 1964 hadi 1985 alikuwa rais wa JMT
 
Ahsante mkuu, katika historia tumesoma kwamba alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Tanganyika Huru kuanzia tarehe 9 Desemba, 1961 hadi tarehe 22 Januari, 1962 alipojiuzulu na kumwachia Mheshimiwa Rashidi Mfaume Kawawa wadhifa huo ili yeye aende kuiimarisha TANU mikoani.
 
Habari Wakuu, lengo la uzi huu ni kukusanya taarifa nyingi kadri tunavyoweza zinazomhusu Baba wa Taifa letu na kuziweka mahala pamoja. Mnaruhusiwa kuongeza makala zake, vitabu na machapisho pia hotuba zake.

Let's Celebrate Our Founding Father.

View attachment 501723

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "baba wa taifa". Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule. Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."

Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama Waziri Mkuu, halafu kama Rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama Rais.

Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.

Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma linashughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu".

MAISHA YA MWL JK NYERERE

Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).

Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.

Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.

Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.

Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary.

Mwaka 1949 alipata [[skolashipu[[ ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).

Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.

Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.

Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.

Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.

Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.

Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi.

Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.

Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.

Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.

MAFANIKIO ALIYOYAPATA MWL JK NYERERE

Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani".

Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda.

Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).

TUZO ALIZOPATA MWL JK NYERERE

View attachment 501724

RAIS WA AWAMU YA 3 BENJAMIN MKAPA AKITANGAZA KIFO CHAKE MWALIMU NYERERE.

Hii hapa chini ni video inayoonesha Makumbusho ya Butiama.

Sunbae,
''Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA),
chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.''

Mimi nimefanya utafiti wa historia ya African Association, Tanganyika African Association,
TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kuwa Mwalimu Nyerere alisaidia kuijenga TAA sikuona popote si katika vitabu nilivyopitia
au kwa wanachana wa TAA niliofanyanao mahojiano, au katika Nyaraka za Sykes ambao
wao ndiyo walikuwa waasisi wa African Association na TANU.

Historia inaonyesha kuwa Mwalimu Nyerere aliingia katika ''serious politics,'' 1953 baada
ya kuchaguliwa kuwa rais wa TAA tarehe 17 Aprili, 1953 katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi
wa Arnautoglo akishindana na Abdulwahid Sykes.

Mwalimu Nyerere alimshinda Abdul Sykes uchaguzi ule kwa kura chache sana.
Kupata habari zaidi za uchaguzi huu unaweza kumsoma Judith Listowel (1965).

Vipi Nyerere aliweza kuchaguliwa ni kisa kinachojitegemea na kinahitaji utulivu na umakini
kwani ni katika historia ambayo hata Mwalimu Nyerere mwenyewe hakuieleza.

Si hilo tu hata TANU ilipoandika historia yake iliyotafitiwa na Chuo Cha Kivukoni historia hii
muhimu haikupewa nafasi na wala jina la Abdulwahid Sykes na viongozi wengine walioleta
mabadiliko ya siasa Tanganyika baada ya Vita Kuu ya Pili hawakutajwa.

Unaweza kupata historia hii hapo chini ikusaidie kuboresha hii historia ya Mwalimu Nyerere:
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK, 2011
Mohamed Said: FB: JUMA MWAPACHU AMZUNGUMZIA BABA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom