Julius Malema afungiwa kutumia Twitter kwa muda

Julius Malema afungiwa kutumia Twitter kwa muda

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1626267704206.png

Kiongozi wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) nchini Afrika Kusini bwana Julius Malema amezuiwa kwa muda kuandika katika akaunti yake ya Tweeter kwa kukiuka miongozo ya Twitter, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Mbuyiseni Ndlozi, mbunge na mwanachama wa chama cha EFF, Jumanne aliweka picha ya ujumbe ambao unaonesha kuwa bwana Malema amezuiwa kwa muda kuandika kwenye twitter.

Bwana Malema amezuiliwa kuandika na kushiriki ujumbe wa wengine kwenye akaunti yake ya twitter kwa muda wa takribani saa 12.

Bwana Malema alitishia kuhamasisha wafuasi wake kushiriki katika vurugu kubwa ambazo zinapinga kufungwa kwa Zuma, zilizoanzia KwaZulu-Natal na jimbo la Gauteng​


“Hatutaki askari mtaani kwetu ! La sivyo, tunaungana na wanaoandamana. Wapiganaji wote wote wanapaswa kuwa tayari...hawawezi kutuua sisi sote. Tunataka suluhu ya kisiasa katika tatizo la kisiasa na sio wanajeshi ,” bwana Malema aliandika kwenye Tweeter akipinga wanajeshi kukabiliana na maandamano.

Rais Cyril Ramaphosa alitoa agizo kwa wanajeshi kwenda katika majimbo mawili kusaidia kuzuia ghasia zilizosababishwa na kufungwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma.

Bwana Ramaphosa alitoa onyo kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya wanaoweka maudhui au taarifa za uongo na uchochezi mtandaoni.

Mamlaka imesema watu wapatao 12 wanachunguzwa kwa kuhamasisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii.

Waziri wa kushughulia masuala ya polisi Beki Cele alisema wanafanyia uchunguzi ujumbe wa Twitter na binti wa Zuma, Dudu Zuma-Sambudla, kukosoa utendaji wa sheria.

Akaunti ya Dudu ilishirikishwa mtandaoni ilikuwa inaikosoa serikali na kusifia au kuwahamasisha waandamanaji wanaopinga kufungwa kwa baba yake.
 
Ujinga wa wanasiasa wa kiafrika, wanawatumia mateja na maskini na wanyonge kwa political gains zao, na hao wajinga wanakubali kutumika.

Nchi yao wenyewe, wanaiharibu kumkomesha nani Cyril Ramaphosa?? Bilionare?

Wangevamia vituo vya polisi, mattress na mahakama, ningewaelewa, kwa sasa nawaona ni vibaka na wenye njaa tupu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Serikali ya Africa kusini inabidi wakae chini ili kumaliza mzozo huu maana bila amani kupatikana hii nchi itakuwa na hali mbaya ya kisiasa tunapoelekea.
 
Kuna muda unatamani wazee walioleta umoja katika bara hili wangerudi ili waone kazi zinazoendelea sahivi, punzikeni tu mashujaa wa afrika
 
Malema ni mnafiki sana. Yeye ndio aliyekuwa anamlipua Zuma kwa ufisadi leo hii anaigeuka mahakama?
Hajaigeuka mahakama, sema yeye hataki wanajeshi ndo wawe ngao ya wangese ambao wamepewa madaraka thats y anasema wanajeshi wasipoondolewa nao watajiunga na waandamanaji!
 
Hajaigeuka mahakama, sema yeye hataki wanajeshi ndo wawe ngao ya wangese ambao wamepewa madaraka thats y anasema wanajeshi wasipoondolewa nao watajiunga na waandamanaji!
Kwann hataki wanajeshi ? Huyo malema Hana Nia nzuri
 
Komredi Tate Malema banaaa.....🤣🤣

Leo Zuma kawa RAFIKI KIPENZI?!!!

Siasa banaaa ha ha ha


Siasa ziliua URAFIKI WAO MKUBWA na kuwa mahasimu....leo Tate Kamarade Malema anapiga "political mileage" kwa yanayoendelea SA 🤣
 
Hapana mkuu GT Magonjwa Malema siyo mzulu bali Msotho ila Kizulu anakiongea kwa ufasaha kama wa Africa kusini wengine ambao siyo wa Zulu.
Lakini Ramaphosa ni mtshivenda (kabila la Venda). Wazulu wanadhani wanaonewa kwa Zuma kuwekwa ndani. Suala hili pia linachukuliwa kikabila kwa upande mwingine.
 
Kuna muda unatamani wazee walioleta umoja katika bara hili wangerudi ili waone kazi zinazoendelea sahivi, punzikeni tu mashujaa wa afrika

Wazee wapi? wale waanzilishi wa hii tabia ya Udikteta hapa barani Africa?
 
Back
Top Bottom