SI KWELI PreGE2025 Julius Malema wa Afrika Kusini asema CHADEMA ni tawi la mabeberu

SI KWELI PreGE2025 Julius Malema wa Afrika Kusini asema CHADEMA ni tawi la mabeberu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hiki kijipeperushi je taarifa hii ina ukweli kiasi gani?

Kishindo July 7, 025.jpg
 
Tunachokijua
Julius Malema ni mwanasiasa na mwanaharakati kutokea nchini Afrka Kusini akiongoza chama cha Economic Freedom Fighters (EFF).

Madai

Juali 1, 2025 kipeperushi cha Kishindo kiliandika taarifa yenye kichwa kinachosema MALEMA AMTUKANA LISSU, CHADEMA. Kipeperushi hiko kikaambtana na vichwa vidogo vinavyosomeaka;

  • “Amwita Gavana wa mabeberu Tanzania, ahoji kama bado ni mwanaume halisi wa afrika au ‘transgender’ “
  • Asema CHADEMA ni tawi la mabeberu, ajivunia kuzuiwa Uingereza, Marekani kwa kupinga ubeberu”

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatialia na kuchunguza uhalisia wa taarifa hiyo na kujiridhisha kuwa haina ukweli.

Ufuatiliaji kupitia kwenye ukurasa wa wa mtandao wa X wa Julius Sello Malema, JamiiCheck imejiridhisha kuwa Malema hakuchapisha taarifa hiyo katika ukurasa wake kama inavyodaiwa na gazeti hilo.

Aidha ukurasa wa X wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) ambacho taarifa huyo inadai pia kuwa ndiyo chanzo cha taarifa yao hakuna taarifa hiyo.

Ufuatiliaji kwa njia ya maneno muhimu katika kurasa hizo mbili ya Malema na chama chake cha EFF hakuna kumbukumbu inayoonesha kuwa walishawahi kuchapisha maneno “Lissu” wala “CHADEMA” hivyo taarifa hiyo inapotosha kwani chanzo waalichokitumia hakikuwahi kuchapisha taarifa hiyo. Tazama hapa na hapa.
Back
Top Bottom