Petu Hapa said:Wanakutana kulumbana na kupembua wakiwa na imani maongezi yao na agenda zao zitachangia katika kuendeleza taifa hili.
Petu Hapa,
..Cordesia,Mabenki,wafadhili etc hawapaswi kuchangia shughuli zisizokuwa na tija kama makongamano ya kisiasa.
..hii ni karne ya Science and Technology, sasa siyo vizuri kupoteza muda na pesa kujadili siasa, kama hili kongamano la Issa Shivji na wenzake.
Hapa umeniacha nje mkuu!Hii ni sawa na mnugu kuwa na tattoo. Tattoo haiongezi ability ya mtu kufanya mambo, ni good feel factor tu.
Jokakuu,
Hapa umeniacha nje mkuu!
JokaKuu:
Kuna kitu kinaitwa social routines. Hawa elites na intelligensia wetu wamezoezwa na mikutano na makongamano ambayo yanabakia kwenye vyumba vya mikutano bila kuwa na impacts yoyote kwa walengwa.
Hii ni sawa na mnugu kuwa na tattoo. Tattoo haiongezi ability ya mtu kufanya mambo, ni good feel factor tu.
companero said:Leo mjadala ni kuhusu zahama ya uchumi duniani ambapo Gavana wa Benki, Prof. Benno Ndulu, atakuwepo kujadili athari zake kwetu na namna ya kukabiliana na zahama hiyo
Most thinkers don't act, kwahiyo sitaraji wasomi wetu watachukua hatua za kiutendaji. Kutegemea kwamba watakuwa watendaji wanachoyasema ni ndoto - kwani kazi yao ni kuchochea fikira - za wanafunzi na jamii - na ndicho kinachofanyika.
Lakini, swala lako la pili ni la msingi kwamba mijadala hiyo iwekwe kwenye utaratibu ambao watendaji mbalimbali wanaweza kuyatumia maongezi hayo.
Raia Mwema said:Kidumba anasimulia akibainisha tofauti ya tija kati ya huko walikotoka na waliko sasa akisema: "Nilianza kulima kwenye skimu hiyo mwaka 1986, tulilima kienyeji, hatukuwa na utaalamu wowote, lakini baadaye skimu yetu iliboreshwa, tukapata utalaamu kupitia mabwana shamba, shamba darasa na mzungu mmoja aliyekuja hapa kijijini kwetu.
"Nimeongeza uzalishaji wa mpunga, sasa navuna gunia kati ya 25 hadi 30 za mpunga kwa ekari moja, huko nyuma nilivuna kati ya gunia saba hadi kumi. Mwaka jana nilivuna gunia 31 katika ekari yangu moja niliyolima, niliuza gunia 15 na kubakiza 16 kwa ajili ya chakula na mbegu.
"Hapa ni kulima mwaka mzima, tunaita hakuna kulala, mpunga nalima mara moja kwa mwaka, halafu kuna vitunguu nalima mara mbili kwa mwaka, mwaka jana nililima ekari mbili na kuvuna gunia 80 kila ekari, lakini nikienda vizuri navuna hadi gunia 100 kwa ekari.
"Kwa mfano Julai mwaka jana nilivuna gunia 100 kwa kila ekari, safari ya pili nilivuna gunia 107, na safari ya tatu nilivuna gunia 96, bei ya Januari huwa ni shilingi 50,000 kwa gunia la vitunguu, lakini baada ya Januari huongezeka hadi kufikia shilingi 70,000."
naposema thinkers don't act, mara nyingi wanachochea fikira za mabadiliko - wanafundisha, wanahamasisha, wanachambua, na kujenga ideas ambavyo vyote kwa namna moja ama nyingine zinainform action. Wale thinkers wenye firkra za kimapinduzi ndio unaweza kuwakuta kwenye mapambano - chachage, shivji, fanon, rodney, karl marx, nyerere, - wakitaka kuleta mabadiliko kwa kushiriki katika hali halisi ya maisha ya watu - wengine wanakuwa observants, later analysts and critics.
agree to disagree.Sio kuwa nakataa shughuli walizofanya. Kama wanazifanya shughuli hizo as a part of academic rituals, which they should do, sina matata.
Lakini kusema kuwa wanayofanya yanaleta chachu za maendeleo ni kuwa irresponsible. Majority ya watanzania ambao wako responsible kuleta maendeleo wana-respond na vitu vingine kabisa na sio yanayotokea UDSM.
..sasa Dr.Ndulu anakwenda kuwahadithia Prof.Shivji na Prof.Soyinka kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani ili wafanye nini haswa?
..taifa letu halijitoshelezi kwa chakula, tena katika mashule yetu wanafunzi hawana waalimu wa kutosha, vitabu, na madawati,maabara, etc.
..sasa kama hali yetu ndiyo hiyo, hamuoni kwamba makongamano ya ku-theorize kama hili ni matumizi mabaya ya kidogo tulichonacho?
Kumbuka pale ni Chuo Kikuu. Pale ndipo walipo wanafunzi wetu ambao wakihitimu wanaenda kufanya kazi kwenye mabenki, mawizara na kwenye taasisi mbalimbali. Hivyo fursa kama hizi ni muhimu kwao ili wajue nini kinaendelea nchini na duniani. Vyuo vyote vikubwa duniani vinafanya hivyo. Vinaleta wataalamu kutoa mihadhara ya Umma ili kuwajenga wanafunzi wao watakaokuwa watunga sera na watekelezaji wa mipango yao ya uchumi na maendeleo. Noam Chomsky, Jeffrey Sachs, Joseph Stigltz, Amatya Sen wote hao huwa wanatoa mihadhara na kuwa na mijadala mikubwa katika vyuo vyao vikuu na mijadala hiyo ndio inatoa chachu ya kufikiria na kuvumbua mipango ya maendeleo. Sasa unataka wanafunzi wetu wasipate fursa za kuwasikia vinara wetu ambao wameshika hatamu za ufahamu na ujuzi wa mambo? Au unadhani kazi ya chuo ni kutoa to vyetu?
"Elimu Sio Cheti Ni Ujuzi" - HAKIELIMU
Companero:
Intellectual pikiniki yenu imekwisha. Nina uhakika mwakani mtarudia yaleyale na kusahau kuwa miaka iliyopita mlishayajadili.