Juma Ali Khatib: Vyama vya siasa viache kutoa mashinikizo kwa Rais Samia ikiwemo madai ya katiba mpya

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Kwa ufupi;

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Juma Ali Khatib amevitaka vyama vya siasa kuacha kutoa mashinikizo kwa Rais Samia ikiwemo madai ya katiba mpya na kutishia kufanya maandamano, kwani hivyo sio vipaumbele vya serikali vinavyotokana na matakwa ya wapiga kura.
 
Kwa sheria IPI?
Umri wako hautasaidia kizazi cha sasa
 
Baraza FEKI la vyama vya siasa na Mwenyekiti FEKI. Lini kachaguliwa huyu? Nani waliogombea hiyo nafasi na nafasi nyingine? Uchaguzi huo uliomchagua ulifanyika lini na wapi? Vyama gani vya upinzani vilivyoshiriki katika uchaguzi huo?
 
πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ‘πŸ½
Huyo aliyesema hayo maneno ni mpumbavu wahed.

Kwanza rais hapatikani bila kusoma moshes na chama. Amejidai eti yuko neutral kwa kutumia neno β€œvyama”, huku reference ikiwa ni chadema. Stupid.
 
Kwani lazima awe Rais?? Halazimishwi kuwa Rais, kama hawezi criticism anaacha!
URais siyo kazi nyepesi nyepesi ya kupeana ushikaji
 
Baraza la vyama vya siasa

Hawana mwakilishi hata mmoja, hawana ushawishi halafu wanajidai wanaongeaongea.

Hivyo ndio vyama mufilisi vinavyodhaminiwa na CCM Chama Cha Mazezeta
 
Mwenyekiti yuko sahihi kabisa.

Katiba mpya si hitaji la wananchi walio wengi.

Katiba mpya haikuwa katika ilani ya CHAMA KILICHOSHINDA UCHAGUZI NA KUUNDA SERIKALI.

#NchiKwanza
#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
#KaziIendelee
 
G55 imezaliwa tena.

Wanaoitaka katiba mpya wanataka KUUVUNJA MUUNGANO kwa kuwa na haya:

1)Serikali ya TANGANYIKA

2)Kiitwacho Zanzibar huru

Lengo lao ni vyeo vya kisiasa huku bara na kule visiwani.....

#KatibaIliyopoNiNzuri
 
Mwenyekiti yuko sahihi kabisa.

Katiba mpya si hitaji la wananchi walio wengi...
Mwenyekiti katoa ujumbe murua lakini wakati siyo husika, wadai katiba wenyewe wameshasanda, mapambano ya mwezi mmoja tu wamepoteana, unawasikia tena mkuu?

Wamebaki wachache nyuma ya keyboard kutukana! Hamna cha kongamano la katiba wala mjomba wake kongamano la katiba tena!! Walidhani Samia ni Kikwete, wakaja motooo, kawatuliza, wamepoaa!! Kiongozi wao huko Twitter kaacha hata kupost hizo ishu za katiba
 
Vipaumbele vya serikali vinapolalamikiwa na wapiga kura vinasikilizwa na nani?Je,iwapo serikali iliwadharau wapiga kura na kuzichakachua kura zao wanaenda kulalamikia wapi?

Swala langu lengine ni kwako Mwenyekiti, kama utakuwa muungwana utanijibu na hili.Je,wewe Mh.Juma Ali Khatib ni mwanachama wa chama gani cha siasa hapa Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…