PostGE2025 Juma Homera: Waliokamatwa 2045, wataachiwa ni 1,736 na 309 wataendelea kushikiliwa

PostGE2025 Juma Homera: Waliokamatwa 2045, wataachiwa ni 1,736 na 309 wataendelea kushikiliwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Juma Homera amesema watu 2045 walikamatwa wakati na baada ya maandamano yaliyozaa vurugu Oktoba 29, 2025 maeneo mbalimbali nchini.

Kati ya hao, 1,736 wataachiwa kutokana na msamaha ambao Rais Samia Suluhu Hassan aliutoa kwa kumwelekeza Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchambua waliofuata mkutambo na kuachiwa.

Hii ina maana 309 wataendelea kushikiliwa.

Rais Samia alitoa msamaha huo Novemba 14, 2025 alipolihutubia na kulizindua Bunge la 13, jijini Dodoma.

Dk Homera ametoa maelezo hayo leo Jumatano, Novemba 26, 2025 alipotembelea Ofisi za DPP jijini Dodoma kwa lengo la kuzungumza na watumishi ikiwa ni siku chache tangu kuteuliwa na kuapishwa na Rais Samia kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Acheni kuleta ujinga humu, mambo ya ccm yaishie huko huko ccm.
 
Back
Top Bottom