Juma Kakere yupo,alikuwepo na atakuwepo

sikuzamwisho

Member
Joined
Apr 12, 2019
Posts
48
Reaction score
185
Mwanamuziki bora wa muda Wote Juma Kakere ambaye mpaka leo Anatamba na kufanya vizuri na nyimbo zake Betty iliyotoka 2001,Pole kwa Safari iliyotoka 2004 na Mama Monica bado anafanya vizuri na Ujio wake mpya wa nyimbo kama 'Kaa la moto' ambao Umefanyika Wasafi Records,'Happy' na ngoma mpya matata inaitwa IMBE ambayo imerekodiwa studio ya combination sound kwa Man Water aka Man Maji hakika ni moto [emoji91]na Anazidi kuthibitisha habahatishi kwenye game la muziki kwa kwenda sambamba na mabadiliko kama Wanamuziki wa Kizazi kipya Wanavyofanya.Ukiachilia kazi mbalimbali ambazo Ameshirikishwa ukiwemo 'Utanitoa Roho' wa Darasa pamoja na collabo nyingi alizofanya ambazo zipo mbioni kutoka kwenye project kadhaa mpya ambazo Ameziandaa pia amefungua milango kwa Wanamuziki wa Kizazi kipya ambao Wanauwezo kupata nafasi ya kuimba na Kumshirikisha.Mabadiliko ambayo amefanya ili kwenda kisasa na Muziki wa Kizazi kipya ni pamoja na kuwa na mitandao ya Kijamii ambapo Facebook anatumia jina Juma Kakere,Instagram Anatumia officialjumakakere pia rasmi Unaweza Kupata nyimbo zake mbalimbali kupitia facebook channel yake Juma Kakere OG Tuendelee kusapoti Muziki mzuri na kuchagua nyimbo zake zinazoishi kama Marry,Shangwe ya Harusi,Pole kwa Safari,Betty na Mambo ya kiswahili.

 
Hivi huyu si mtoto wake ni yule jamaa anaitwa Deddy alikuwa anafanya kazi sana na Mabeste pamoja na marehemu Pancho .
 
Mbona unampa sifa kubwa hivo wakati mwenye sifa hizo ni Mungu TU!!!??? maana Mungu ndiye aliye sema ktk vitabu vitakatifu kuwa yeye alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo......


Ila sishangai maana watanzania siku hizi tumekuwa ni watu wa kusifia mpaka tunapitiliza yani.
 
Ubarikiwe Mtumishi Upo sahihi Nimekuelewa Unashauri Turekebishaje
 
Mtu mpaka anazeeka katoa vinyimbo viwili tu vilivyopigwa pigwa redioni na kwenye TV leo hii umwite mwanamuziki bora wa muda wote? Hebu kuweni serious jamani!!..
 
Mtu mpaka anazeeka katoa vinyimbo viwili tu vilivyopigwa pigwa redioni na kwenye TV leo hii umwite mwanamuziki bora wa muda wote? Hebu kuweni serious jamani!!..
Majina Yanaumba Unaitwa kalagabaho,nenda kasikilize Kaa la moto na Happy Utakubali
 
Dingilii yuko yechu kinyama uyu..Naikubali sana safari na Hepiii hepiiui hepiiiiii!!!Dooh ni kisanga robo3 bablai
 
katoka sasa hivi kufanya interview apa p/bongo anajua
 
Nyimbo zake nyingi ni za kiutu uzima sana, burudani tosha kwa sisi wapenzi wa mziki huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…