sikuzamwisho
Member
- Apr 12, 2019
- 48
- 185
Mwanamuziki bora wa muda Wote Juma Kakere ambaye mpaka leo Anatamba na kufanya vizuri na nyimbo zake Betty iliyotoka 2001,Pole kwa Safari iliyotoka 2004 na Mama Monica bado anafanya vizuri na Ujio wake mpya wa nyimbo kama 'Kaa la moto' ambao Umefanyika Wasafi Records,'Happy' na ngoma mpya matata inaitwa IMBE ambayo imerekodiwa studio ya combination sound kwa Man Water aka Man Maji hakika ni moto [emoji91]na Anazidi kuthibitisha habahatishi kwenye game la muziki kwa kwenda sambamba na mabadiliko kama Wanamuziki wa Kizazi kipya Wanavyofanya.Ukiachilia kazi mbalimbali ambazo Ameshirikishwa ukiwemo 'Utanitoa Roho' wa Darasa pamoja na collabo nyingi alizofanya ambazo zipo mbioni kutoka kwenye project kadhaa mpya ambazo Ameziandaa pia amefungua milango kwa Wanamuziki wa Kizazi kipya ambao Wanauwezo kupata nafasi ya kuimba na Kumshirikisha.Mabadiliko ambayo amefanya ili kwenda kisasa na Muziki wa Kizazi kipya ni pamoja na kuwa na mitandao ya Kijamii ambapo Facebook anatumia jina Juma Kakere,Instagram Anatumia officialjumakakere pia rasmi Unaweza Kupata nyimbo zake mbalimbali kupitia facebook channel yake Juma Kakere OG Tuendelee kusapoti Muziki mzuri na kuchagua nyimbo zake zinazoishi kama Marry,Shangwe ya Harusi,Pole kwa Safari,Betty na Mambo ya kiswahili.