Juma Kaseja anatafuta kiki kwa Djigui Diara

Kaseja alikua kipa mzuri sana golini ila kwenye footwork sina uhakika analingana na Diarra
Achana na footwork kupiga pass ,Juma k juma anapiga ,faulo na penalty ndani ya 90 minutes ukikutana na washambuliaji wa zamani waulize mwamba alivyokuwa anawageuza .kwa walioanza kuangalia ligi ya tz kupitia Azam hawajui vitu vya kaseja,lunyamila, Hussein masha,etc
 
Wanazungumzia Foot work,hata Chilavet wa Chile alishafanya mengi,kafunga sana magoli ya faulo na penalty, ila hakuwa na passing ability ya hali ya juu kama ilivyo kwa wakina Onana. Kaseja tulimuona tukisema tumuhesabie successful pass alizozipiga kwenye maisha yake ya soka,inawezekana hajafikia hata nusu idadi ya pass alizo piga Diara. Diara anauwezo wa kupiga short pass,long pass,penetration pass in all directions na zinafika,Kaseja hiki kitu hana.
 
Watu Wana kuza Mambo, Kaseja alikua mdakaji mzuri na kweli ilishawahi kutokea kupiga Penalty mara chache.
Kwa swala la kulingana na Diara katika kucheza mpira hapana.
Diara Yuko mbali Sana, Wapo Makipa wachache Sana kwa Afrika wenye footwork kama ya Diara.
Tuna mzungumzia Kaseja aliyekua akiwekwa bench na Ivo Mapunda.
 
Mbona sijaona kosa la kaseja ila ambao hawakumshuhudia J K Juma enzi Zamaleki wanatolewa ndo atakua na dought. Ila Diarra kwa karne hii yuko poa
 
Na yeye hajasema anamzidi Diara amesema anachokifanya Diara kucheza na mpira na yeye alifanya sababu kabla ya kuwa kipa alikuwa mchezaji.
Sina shaka na ubora wa kaseja kwenye kudaka ila kwenye kuchezea mpira anatupanga siyo kweli
 
Well said.
 
Bhebhe nyanda.
 

Sifa za Kijinga....! Pasi na goal keeping wapi na Wapi?

Akili za Wachambuzi Uchwara hizi, huwa kipindi kizima Cha Radio ama Television wanajadili Diarra kapiga pasi ngapi badala ya Kufanya saves ngapi?
 
Sifa za Kijinga....! Pasi na goal keeping wapi na Wapi?

Akili za Wachambuzi Uchwara hizi, huwa kipindi kizima wanajadili Diarra kapiga pasi ngapi badala ya. Kufanya. saves ngapi?
Hivi unajua moja nguzo ya mafanikio ya Guardiola ni makipa wenye foot work nzuri?

Ushajiuliza why sasa hivi ktk modern football timu nyingi kubwa zina prefer makipa wenye foot work nzuri?Ukianza kwa Ederson na City,njoo kwa Raya na Arsenal,njoo kwa Man Utd na Onana,njoo kwa Liverpool na Allison,njoo kwa Emanuel Neur na Bayern.

Diara ukiachana na kudaka,ila yy mara nyingi ndie anaye anzisha mashambulizi kupitia pasi zake. Siku hizi hawataki kipa anayedaka kama nyani tu, wanataka anaye daka na mwenye foot work nzuri,kipa awe pia na jicho la kuanzisha mashambulizi,kupitia magap anayo yaona.
 
Sina shaka na ubora wa kaseja kwenye kudaka ila kwenye kuchezea mpira anatupanga siyo kweli
Wachezaji wa zamani mpira ulikuwa redioni zaidi kuliko televisheni, unaweza kuwa sahihi ila mhusika kajipima kaona alikuwa na uwezo wa kuchezea mpira.
 
Watanzania hawapendani kuweni wazalendo
–khalid Aucho–
 
Mimi nilimuona akiokota goli tano nyavuni kwake za Al Ahaly.
 
Ajilinganishe na Manula mwenzake kavuka boda analipwa kwa dollar
Ana medali ya cafcc
Kafika robo Afcon
Kafika robo ya cafcl
Wakati wake alijitahidi ila asijilinganishe na Diara
Kwan yuko wap siku hiz Manula
 
humu siku hizi inaonekana wengi wa wachangiaji ni vijana wadogo!,
Diarra kwa kaseja bado hajamfikia, kaseja enzi zake alikua hatari hasa kuanzia 2001 mpk 2010 hapo,.......

anyway, naona siku hizi watoto wengi wanawapinga wazoefu
 
Mimi nilimuona akiokota goli tano nyavuni kwake za Al Ahaly.
Ahly? Nafikiri umri wako mdogo umeanza kufuatilia mpira wakati wa azam ndio kwanza ulifika mjini,aliyefungwa tano na ahly ni manura ,Kaseja umfunge tano unaanzia wapi,hata akiwa kagera hizo tano sijawahi kuziona .Tatizo tunajadiliana na watoto wasiojua hili wala lile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…