JUMA LA VITABU ULIMWENGUNI

JUMA LA VITABU ULIMWENGUNI

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
LEO SIKU YA VITABU DUNIANI 1

"The School Trip to Zanzibar"

Mwandishi Mohamed Said
Mchapaji: Africa Proper Education Network, Dar es Salaam

Hiki kitabu kimechapwa mwaka jana 2020 na kinawafaa sana watoto wa shule za msingi kwa kujifunza Kiingereza na historia ya Zanzibar.

Kupitia kitabu hiki mwanafunzi atajifunza mengi katika maisha ya kila siku ya Wazanzibari na utamaduni wao.





LEO SIKU YA VITABU DUNIANI 2

''The Torch on Kilimanjaro''
Mwandishi Mohamed Said
Mchapaji: Oxford University Press, Nairobi

Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa Oxford University Press, Nairobi kwa ajili ya kusomesha Kiingereza na Historia kwa shule za msingi.

Ni kitabu kinachoeleza harakati za kudai uhuru zikiongozwa na Julius Nyerere msimuliaji akiwa mtoto mdogo aliyeshuhudia harakati hizo.

Kitabu hiki ni riwaya inayoeleza matukio ya kweli ya historia ya Tanganyika katika miaka ya 1950 wakati wananchi wamejizatiti kupambana na ukoloni wa Muingereza.

Kitabu kimechapwa mara mbili na hiyo picha hapo ni toleo la pili.
Toleo la kwanza lilichapwa mwaka wa 2007.

May be an image of 2 people and text that says 'The torch on Kilimanjaro AFRICA READERS 15 OXFORD Mohamed Said'


LEO SIKU YA VITABU DUNIANI 3

''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism ni Tanganyika.''

Mwandishi: Mohamed Said
Mchapaji: Minerva Press, London

Kitabu hiki kimezungumzwa sana na kinafahamika.

Kimechapwa mara kadhaa pamoja na tafsiri ya Kiswahili kuanzia mwaka wa 1998 kilipochapwa kwa Kiingereza London na Minerva Press na tafsiri ya Kiswahili ilipochapwa na Phoenix Publishers, Nairobi 2002.
Picha ya kulia ni tafsiri ya kwanza ya Kiswahili iliyochapwa na Phoenix Publishers, Nairobi 2002.





LEO SIKU YA VITABU DUNIANI 4

''Uamuzi wa Busara''

Mwandishi: Mohamed Said
Mchapaji: Abantu Publications, Nairobi Kenya.

Mchapaji wa kitabu hiki alikusudia kitabu hiki kitolewe wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya Uchaguzi wa Kura Tatu wa mwaka wa 1958.

Utangulizi wa kitabu ilikuwa uandikwe na mmoja kati ya viongozi wa juu wa CCM ambao ndiyo warithi wa historia ya TANU.

Kitabu kinaeleza historia muhimu sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika chini ya chama cha TANU.
Ingawa kitabu kilitoka kwa muda muafaka lakini lengo lililokusudiwa halikufanikiwa.

Kitabu hakikuandikiwa utangulizi kama ilivyokusudiwa wala hakikutumika katika kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Tabora.

Kitabu hiki kimefeli na ni ''out of print,'' yaani hakipatikani.
Duka moja maarufu la vitabu walikikataa kukiuza walikichukua kisha wakakirudisha kwa mchapaji.

May be an image of 1 person and text that says 'Abantu Uamuz wa busara wa Tabora Mohamed'
 
Back
Top Bottom