Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Namungo FC imemtangaza rasmi Juma Ramadhan Mgunda, maarufu kama "Gurdiola Mnene," kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo. Mgunda anachukua nafasi ya Mwinyi Zahera, ambaye sasa atakuwa mshauri wa benchi la ufundi.
Kocha Mgunda atafanya kazi kwa kushirikiana na Ngawina Ngawina na Shedrack Nsajigwa katika benchi la ufundi la Namungo FC.
Kibarua chake cha kwanza kama kocha mkuu huwenda kitakuwa dhidi ya Simba Sports Club, mchezo utakaofanyika kesho Ijumaa, Oktoba 25, katika uwanja wa KMC Complex.
Kocha Mgunda atafanya kazi kwa kushirikiana na Ngawina Ngawina na Shedrack Nsajigwa katika benchi la ufundi la Namungo FC.