Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kikaso hicho kitawakutanisha Wakurugenzi na Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kujadili namna bora ya kuongeza ufanisi, uwajibikaji na usimamizi wa watumishi wa umma.
===================================
Ndugu Wanahabari; Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana hapa leo tukiwa na afya njema. Pia, niwashukuru ninyi kwa utayari wenu wa kushirikiana na Ofisi hii wakati wote hususani kunapokuwa na jambo muhimu la kueleza umma kuhusu masuala ya tumishi wa umma na utawala bora. Jitihada zenu na mchango wenu kwa Ofisi hii ni mkubwa sana.
Ndugu Wanahabari; naomba kutumia fursa hii pia kuwakumbusha kuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) ina majukumu mbalimbali kwa mujibu wa Hati ya Mgawanyo wa Majukumu kwa Mawaziri kama ilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 619A & 619B la tarehe 30/8/2023. Moja ya majukumu hayo ni kusimamia Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma Serikalini.
Ndugu Wanahabari; Mkutano wa leo unalenga kuwaalika Wakurugenzi au Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kushiriki kwenye kikao kazi cha Wakuu za Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa umma.
Ndugu Wanahabari; Kikao hiki muhimu kitafanyika katika Ukumbi wa Mabele Hall hapa Jijini Dodoma tarehe 1 - 3 Juni, 2026 na kitaongozwa na Kaulimbiu isemayo “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ulio Sikivu, Jumuishi, wenye Matokeo na Uwajibikaji Kuelekea Dira 2050”.
Ndugu Wanahabari; Kikao kazi hiki kimekuwa kikifanyika kila mwaka na kinatoa fursa ya kubadilishana uzoefu katika kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali hususani katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Ndugu Wanahabari; Kikao, kitajadili kwa kina na kufafanua matumizi ya mifumo ya kidijiti ya e-Uhamisho, e-Watumishi, e-Utendaji, e-Mrejesho, HR Assessment kwa kuzingatia Shabaha na vipaumbele vya Taifa kuelekea Dira 2050.
Vile vile, kikao kitatumika kujadili changamoto na mafanikio yaliyopo katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu pamoja na kupendekeza namna bora ya kushughulikia changamoto zilizopo.
Ndugu Wanahabari; naomba ifahamike kuwa viongozi mbalimbali wenye dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu katika utumishi wa umma watapewa maelekezo mahususi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi Umma. Hivyo, ninasisitiza viongozi tajwa kushiriki kikao kazi hicho wao wenyewe bila ya kuwakilishwa.
Ndugu Wanahabari; , Mgeni rasmi katika mkutano huu ni Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia Rasilimaliwatu na Utawala katika Utumishi wa Umma nchini.
Ndugu Wanahabari; Kikao hiki kinaandaliwa na Ofisi yangu, hivyo ninatoa wito kwa washiriki wote waliotajwa kujisajili katika mfumo wa TSMS kupitia linki TSMS ili kurahisha taratibu za maandalizi, na mwisho wa kujisajili ni tarehe 29 Mei, 2026 saa 6:00 usiku.
Ndugu Wanahabari; kutokana na umuhimu wa Kikao Kazi hiki, niwatake Wakuu wote wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kufika katika Ukumbi wa Mabele Hall uliopo katika Jiji la Dodoma tarehe 31 Mei, 2026 kuanzia saa 4:00 asubuhi ili kuchukua vitambulisho vyao kwa ajili ya kikao.