Juma Mwapachu anazungumza kuhusu historia ya Uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
upload_2018-4-14_15-11-6.png

Utangulizi

Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nansio, Ukerewe wakati Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda Nansio mwaka wa 1953 kumuona baba yake, Hamza Kibwana Mwapachu kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka huo uliokuwa ufanyike miezi michache mbele.

Abdul Sykes alikuwa anataka kauli ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu Nyerere kuwa ndiyo Hamza hajabadili fikra yake na anamtaka Abdul ampishe Nyerere katika nafasi ya urais wa TAA?

Hamza Mwapachu alirejea katika fikra yake na akamueleza Abdul kuwa Nyerere achukue nafasi ya urais na mwaka ujao, 1954 iundwe TANU. Juma Mwapachu kashuhudia haya kwa macho yake hakuhadithiwa.

Juma Mwapachu kasoma niliyoandika kuhusu historia ya TANU na hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoniandikia:

''Mohamed naafiki kabisa na maelezo yako.

Ndugu Msekwa hajaandika historia ya ukweli kuhusu vuguvugu la siasa za kugombea uhuru kuelekea uundwaji wa TANU.

Historia haifutiki wala kupinduliwa.
Hivi tatizo ni nini hasa kutoa maelezo ya ukweli?

Dr Kyeruzi alinipa nakala ya makala ya kitabu chake ' The Muhaya Doctor' baada ya kunitumia salaams kupitia kwa kaka yangu Harith Bakari kuniita niende kumuona nyumbani kwake Bukoba.

Nilikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo akitaka nimsaidie kuchapisha kitabu chake.

Nisiseme zaidi.

Muhimu ni sura moja ya kitabu hicho ikifafanua historia ya kukuzwa kwa uongozi wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mapambano yalishika moto kuanzia 1949 mjini Dar-es-Salaam. Dr. Kyeruzi ameandika kwa makini historia hiyo.

Wewe Mohamed ni mkweli katika kunukuu historia sahihi.

Ajabu kwangu Mwalimu Nyerere naye hakutaka kuandika kuhusu historia hii, kwa mfano, Nyerere baada tu ya harusi yake Butiama alipitia Mwanza na kuonana na rafiki yake, Hamza Mwapachu ambaye alisafiri toka Ukerewe kuonana na Kambarage kwa mara ya kwanza baada ya kurejea kutoka Scotland masomoni.

Chief Abdallah Fundikira pia alikutana na Nyerere wakati huo.
Mazungumzo yao yalikuwa kumshawishi Nyerere kuongoza vita ya uhuru.

Wakati huo Edward Twinning alikuwa bado hajapiga marufuku watumishi wa serikali kujihusisha na siasa.

Lakini Twinning alitambua kwa haraka kwamba sera yake ya kuwapeleka uhamishoni mbali na Dar es Salaam wakina Hamza Mwapachu na Dr. Kyeruzi na hata Ally Sykes ilikuwa inashindwa kuzima uongozi wa siasa.

Hivi Msekwa hajui historia hii?
Na kwanini Nyerere hakutaka kuandika historia hii?

Katika mahojiano ambayo Nyerere kaweza kuongelea kuingia kwake katika siasa nasikitika kusema kwamba maelezo yake huwa mepesi au kijuujuu.

Nyerere alinipenda kama mwanawe hivyo siwezi kumlaumu.
Lakini hawa wengine kama Msekwa lazima tuwakosoe.

Wasipinde historia ya vita vya uhuru.

Nasikitika sana kwamba Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walifariki mapema mno baada ya uhuru.

Hawa marafiki kama ndugu walikuwa hazina ya jinsi Tanganyika ilivyojiandaa na kujenga misingi ya vita vya huru.''
 
Heshima kwako, Mzee Mohamed Said

Huyu Mwapachu unayemzungumzia ndiyo yule BALOZI.?
 
Mungu azidi kukupa umri zaidi,kazi hii ilikosa mtu wa kuifanya kwa usahihi na bila unafiki,endelea kaka kumbukumbu zitakuweka hai hata baada ya kuondoka hapa duniani.
 
Ndiyo yeye Balozi.
Kaka habari. Pole na hongera kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutupatia historia ya kweli ya nchi yetu.

Nilipata kusikia habari za Chief Makongoro wa Ikizu kuwa naye ni miongoni mwa watu walioshiriki katika kupigania Uhuru wa Nchi yetu. Kama ukipata wasaa na iwapo unajua chochote juu ya huyo Chief, tafadhali naomba utuwekee Mada juu yake.
 
Chief...
Najua kuwa Chief Makongoro ana historia nzuri na uhusiano mkubwa na Baba wa
Taifa.

Katika utafiti wangu wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes nimekutananae katika
sakata ya Sheikh Suleiman Takadir alipomwita Nyerere Mtume wa Afrika.

Watoto wa Chief Makongoro wapo ninaamini wao ni aula zaidi kuandika historia ya
baba yao.
 
Mkuu, hivi ni kwanini sijawahi kuona umeandika Uzi humu Jf pasipo kumtaja Abdul Sykes?
 
Ushimen,
Ikiwa ni historia ya African Association, TAA, TANU, Julius Nyerere na historia ya uhuru wa Tanganyika lazima uanze na katibu muasisi wa African Association Kleist Sykes 1929, baba yake Abdul Sykes. Baada ya kipindi chake ni lazima uje kwa wanae, Abdul, Ally na Abbas. Abdul ndiye aliyekibeba chama kuanzia 1950 hadi 1954 alipoasisi TANU pamoja na Nyerere na wazalendo wengine jumla yao watu 17 mdogo wake Ally akiwa katika hao waasisi 17. Abdul ndiye aliyekuwa na nyaraka zote za historia hii kuanzia 1929 baba yake alipoasisi African Association hadi 1954 TANU ilipoundwa. Mimi ndiye mtafiti pekee ukimtoa Muingereza John Iliffe ndiye niliyeziona nyaraka zote hizi hadi hivi sasa ambazo umri wake ni miaka 80. Nasikitika sana kuwa nyaraka hizi hazijawekwa Makumbusho ya Taifa hadi hivi sasa. Wapo waliojaribu kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika bila ya kumtaja Abdul Sykes. Leo baada ya mimi kumuandika Abdul Sykes na kumuunganisha na wazalendo wengine kama Hamza Mwapachu historia zao hazina tena thamani. Historia ya uhuru na kuundwa kwa TANU na historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere haiwezi kukamilika bila ya kumtaja Abdul Sykes. Hii ndiyo sababu ninapoandika historia ya TANU namtaja Abdul Sykes.
Kama vile isivyowezekana kuandika historia ya Azimio la Arusha na Vijiji Vya Ujamaa bila kumtaja Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ndivyo hivyo hivyo isivyowezekana kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika bila kumtaja Abdul Sykes.
 
Promo ya kitabu
Mchawi,
Kumtaja Abdul haiwezi kutangaza kitabu.
Kitabu hiki kimepata umaarufu sana kwa msaada wa JF na mimi kujulikana kwingi lakini kitabu kimepata umaarufu kutokana na historia yake Abdul Sykes...historia yake na si jina lake. Abdul kwa watu wa Dar es Salaam ya wakati wake alikuwa kijana maarufu sana wala hakuhitaji kuandikwa na yeyote ili ajulikane.
Ajabu ni kuwa kule kumfuta Abdul Sykes katika historia ya TANU nikaja mimi kuandika historia yake ndiko kulikonyanyua jina lake zaidi ya miaka 30 kupita baada ya kifo chake
mwaka wa 1968.
 
View attachment 744346

Utangulizi

Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nansio, Ukerewe wakati Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda Nansio mwaka wa 1953 kumuona baba yake, Hamza Kibwana Mwapachu kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka huo uliokuwa ufanyike miezi michache mbele.

Abdul Sykes alikuwa anataka kauli ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu Nyerere kuwa ndiyo Hamza hajabadili fikra yake na anamtaka Abdul ampishe Nyerere katika nafasi ya urais wa TAA?

Hamza Mwapachu alirejea katika fikra yake na akamueleza Abdul kuwa Nyerere achukue nafasi ya urais na mwaka ujao, 1954 iundwe TANU. Juma Mwapachu kashuhudia haya kwa macho yake hakuhadithiwa.

Juma Mwapachu kasoma niliyoandika kuhusu historia ya TANU na hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoniandikia:

''Mohamed naafiki kabisa na maelezo yako.

Ndugu Msekwa hajaandika historia ya ukweli kuhusu vuguvugu la siasa za kugombea uhuru kuelekea uundwaji wa TANU.

Historia haifutiki wala kupinduliwa.
Hivi tatizo ni nini hasa kutoa maelezo ya ukweli?

Dr Kyeruzi alinipa nakala ya makala ya kitabu chake ' The Muhaya Doctor' baada ya kunitumia salaams kupitia kwa kaka yangu Harith Bakari kuniita niende kumuona nyumbani kwake Bukoba.

Nilikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo akitaka nimsaidie kuchapisha kitabu chake.

Nisiseme zaidi.

Muhimu ni sura moja ya kitabu hicho ikifafanua historia ya kukuzwa kwa uongozi wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mapambano yalishika moto kuanzia 1949 mjini Dar-es-Salaam. Dr. Kyeruzi ameandika kwa makini historia hiyo.

Wewe Mohamed ni mkweli katika kunukuu historia sahihi.

Ajabu kwangu Mwalimu Nyerere naye hakutaka kuandika kuhusu historia hii, kwa mfano, Nyerere baada tu ya harusi yake Butiama alipitia Mwanza na kuonana na rafiki yake, Hamza Mwapachu ambaye alisafiri toka Ukerewe kuonana na Kambarage kwa mara ya kwanza baada ya kurejea kutoka Scotland masomoni.

Chief Abdallah Fundikira pia alikutana na Nyerere wakati huo.
Mazungumzo yao yalikuwa kumshawishi Nyerere kuongoza vita ya uhuru.

Wakati huo Edward Twinning alikuwa bado hajapiga marufuku watumishi wa serikali kujihusisha na siasa.

Lakini Twinning alitambua kwa haraka kwamba sera yake ya kuwapeleka uhamishoni mbali na Dar es Salaam wakina Hamza Mwapachu na Dr. Kyeruzi na hata Ally Sykes ilikuwa inashindwa kuzima uongozi wa siasa.

Hivi Msekwa hajui historia hii?
Na kwanini Nyerere hakutaka kuandika historia hii?

Katika mahojiano ambayo Nyerere kaweza kuongelea kuingia kwake katika siasa nasikitika kusema kwamba maelezo yake huwa mepesi au kijuujuu.

Nyerere alinipenda kama mwanawe hivyo siwezi kumlaumu.
Lakini hawa wengine kama Msekwa lazima tuwakosoe.

Wasipinde historia ya vita vya uhuru.

Nasikitika sana kwamba Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walifariki mapema mno baada ya uhuru.

Hawa marafiki kama ndugu walikuwa hazina ya jinsi Tanganyika ilivyojiandaa na kujenga misingi ya vita vya huru.''
Nlionana naye kama wiki moja hivi
Nyuma juma,alikuwa amefanyiwa sherehe ndogo ya siku yake ya kuzaliwa...nkaenda kumsalimia
Kwenye kikao hicho alikuwepo mama j.kahama pia

Ova
 
Back
Top Bottom