Juma Nature:Singeli ni muziki wa kihuni.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506





Licha ya Singeli kuwa muziki ulioibuka kwa kasi na kujizolea mashabiki lukuki na kufanikiwa kuzalisha vipaji kadhaa mwanamuziki Mkongwe Juma Kasim Nature ameibuka na kusema muziki huo ni wa kihuni na hautadumu.

Akiongea katika studio zake za Halisi Records mapema wiki hii na mwandishi wa habari hizi, Juma Nature amedai kuwa Singeli ni muziki ambao hautoishi kuwa muziki wa kudumu kwa muda mrefu bali unapita tu kwasababu ni muziki wa kihuni.

Akaongeza pia kuwa mahabiki hawapendi mambo ya kipumbavu ambayo yanaletwa na baadhi ya wahuni wanaovamia muziki.

“Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” alisema.

“Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumbavu pumbavu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,” alisema Nature.

Source: Bongo5
 
Mpitoo!?!?ngoja tusubri tuone.time will tell.
 
Mi mwenyewe huwa nahisi singeli ni upepo tuu utavuma na kuisha, tena imepata umaarufu kwa kuwa ilipigiwa promo na Efm, sasa na mawingu wakaidakia juu juu kwa kasi hawajui hata wanaipeleka wapi.
Singeli ina maisha mafupi kwa sasa
 
Singeli ndio mziki wa aina gani? Na wakina nani wanafanya mziki wa singeli?
 
Ukimuona kwenye kanzu na kofia unajiuliza. Kaacha ×××n*i ?
 
Yeye anauona ni muziki wa kihuni lakini vijana wenzie wameiona fursa wameanza kuitumia na wanapiga mpunga manfongo toka fiesta imeanza mbaka inaisha atakuwa kaingiza si chini ya milioni 20 sio pesa ndogo na akizidi kujitahidi ataingiza pesa nyingi zaidi wakati huo Nature amekaa kijiweni anawaponda!

-Nyerere-
 
Endeleeni kuota tu...
Kuiua singeli ni LAZIMA uiue Temeke na Kinondoni kwanza(haiwezekani)..!
Ukiweza kufanya hilo(haiwezekani) basi SINGELI itabaki kuwa HISTORY tu(haiwezekani)..!
[HASHTAG]#LongLiveSINGELI[/HASHTAG]..!!!
 
Kila singeli utasikia: eeh baba eeeh baba eeeeeeh baba!
Mziki wa hovyo kabisa huu, naupa miezi miwili iliyobaki sidhani kama utafika mwaka mpya huu mziki, kila singeli beats zile zile isipokuwa lyrics tu, na lyrics zenyewe eeeh baba eeeh baba, mara shemeji na uhuni mtupu! Upuuzi kabisa!
By the way, msaga sumu haimbi singeli ndo maana ataendelea kuwapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…