Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506

Licha ya Singeli kuwa muziki ulioibuka kwa kasi na kujizolea mashabiki lukuki na kufanikiwa kuzalisha vipaji kadhaa mwanamuziki Mkongwe Juma Kasim Nature ameibuka na kusema muziki huo ni wa kihuni na hautadumu.
Akiongea katika studio zake za Halisi Records mapema wiki hii na mwandishi wa habari hizi, Juma Nature amedai kuwa Singeli ni muziki ambao hautoishi kuwa muziki wa kudumu kwa muda mrefu bali unapita tu kwasababu ni muziki wa kihuni.
Akaongeza pia kuwa mahabiki hawapendi mambo ya kipumbavu ambayo yanaletwa na baadhi ya wahuni wanaovamia muziki.
“Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” alisema.
“Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumbavu pumbavu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,” alisema Nature.
Source: Bongo5