LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.
Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.
Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.
Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.
Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu.
Kwa zaidi ya miaka ishirini aliyo Fanya kazi hii, Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka
Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana.
Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke aliyepika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika.
KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."
Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.
Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..
MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.
Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.
Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.
"Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "
" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.
Hata hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.
Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.
Juma Njemba alifariki mwaka 2001. Waliokuwa NAE karibu wakati wa kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..
Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.
Juma Njemba alifanya vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua.
----------- Maoni ya AbuFizzer --------------
Nimesoma story hii, kwanza nikupongeze kwa kuweza kuandika ulichoandika, lakini nikukosoe kuwa hukuandika ukweli wa mambo kabisa.
Mtu huyu uliyemuandika mimi nimeishi nae mtaa mmoja, barabara moja, kata moja na Zaidi nimesoma na wanae, ninaijua familiar yake na historian nzima ya maisha ya marehemu mzee huyu.
Ni mtu aliyekuwa maarufu sana, na mjuzi sana wa kitabu na masala ya hesabu za nujumu.
Mtu huyu kwa awamu tofauti aliwahi kuwa msanii wa ngoma za asili, mtoza ushuru, fundi muashi, mwanafunzi, dobi, mwanasiasa, mfabiashara, mtu wa elimu ya nyota, dua, na nyiradi za tiba kwa wanadamu.
Alikuwa mtu mkarimu na mwenye umri mkubwa katika eneo aliloishi. Ni vema kutambua kuwa kwa andiko hili mimi na engine tunaoamini andiko hili halikufanyiwa utafiti wa kutosha kuandika kwa ajili ya kukabili upotoshaji wa kihistoria uliopo katika andiko lako.
Hii itasaidia jamii kumfahamu mtu huyu nguli wa elimu ya hesabu, nyota, dua na nyiradi ambaye alifahamika kwa watu bila kutumia vyombo vya habari, kinyume na wengi waliotumia vyombo vya habari kama marehemu Sheikh Yahya Hassan (akifahamika kwa jina la Yahya Hussein).
Pia itasaidia kuondoa simanzi kwa familiar yake kutokana na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na baadhi ya watu, ambao kwa sababu zao binafsi wanatumia vidole (kalamu) kupotosha historia ya mzee wao.
Ambaye alikuwa mtu asiye na ubaguzi wa kidini rangi au jinsia, alihofiwa na alipendwa, alitiiwa na aliwatii watu wake, alikirimiwa na alikirimu, aliaminiwa na kuitwa "baba wa mji"
Mzee Juma Njemba halikuwa jina lake Bali ilikuwa Lakabu yake, yeye haswa alikuwa na lakabu kadhaa kabla ya hiyo.
Miongoni mwa lakab zake (kun-ya) nickname zake ni Juma wa Mwanga, Njemba, Lubambala, Ng'anga nk.
Mzee huyu alizaliwa Mji wa kale wa Ujiji, katika kitongoji kidogo cha Kasimbu barabara ya Msafiri. Baba yake aliitwa Abdallah na mama yake aliitwa Johari Bint Lwamba.
Mzee Juma alizaliwa mwaka baina ya mwaka 1918 na 1920 kumbukumbu zinaonesha kuwa alikuwa miongoni mwa watu wenye umri mkubwa licha ya kuwa hakuwa mkubwa Zaidi ya babu yake Abdul Nondo ( mzee Haji Mitumba)
Alizaliwa katika familia ya watoto watatu wa kiume, Mussa akiwa mkubwa, yeye na mdogo wao akiitwa Bushiri.
Nitaendelea kadiri ya muda utakavyokuwa unapatikana
AbuFizzer anasema
Even dark of his, umeweka uwongo mwingi sana. Juma Njemba aliowa wake kwa dini ya kiislam, aliishi an wake wanne, akihitilafiana au kufiwa na mke aliongeza mke kwa kuoa mwingine. Hakudhulum mke wa mtu, alichumbia na kukubaliwa akaowa, alipokataliwa posa take hakuoa na hakudhuru mtu.
Pia umeandika kuhusu kuacha na kudhuru wenzi wake aliotalakiana nao, jambo ambalo si la kweli, mke wake wa kwanza akiitwa Bi. mtumwa bint Ali Saad, mwanamke huyu aliishi toka ujana hats kifo na mumewe na hawakujaliwa kupata mtoto.
Mke wake wa pili akiitwa Hawa bint Almas Msano mpaka leo anaishi Sengerema Mwanza amekuwa ajuza kwa umri wake alizaa nae bint aliyeitwa Asha.
Mke wa tatu sikumbuki jina lake lakini alizaa watoto wawili mmoja akiitwa Lwamba na Mwingine Mwamvua. Mwanamke huyu waliachana muda mrefu kwa mke huyu kurejea kwao Urambo ambako kaka yake alikuwa na uchumi hivyo aliamua kuachana na ndoa kuendelea kusimamia uchumi (pengine walikuwa na yao) lakini hakumuuwa wala hakukuwa na madhara, mama huyu kafa mwaka juzi 2016 Tanga Mjini.
Alimuoa pia mama wa kisenegal akazaa bint akiitwa Johari, mama Yule walitengana na hakumdhuru alifariki mwaka 2014 akiwa mtu mzima.
Alimuoa mwanamke mwingine akazaa nae mtoto wa kiume akiitwa Mwinyimbegu yupo mtu huyu pale Kigoma Ujiji na mama yake yu hai na hana madhara.
Alioa mwanamke wa kiha akiitwa Bora bint Maulid mungo mkuyu huyu kazaa nae watoto wanne. Wawili wa kiume wapo Dar Es salaam pale jiran ya Meeda Bar Sinza. Tena wapo na mama yao ambaye aliishi na marehemu mpaka kufa kwake. Na wawili wa kike mmoja ni mwalimu Mwanza na mwingine yupo huko Ujiji kwao.
Hivyo umeweka chumvi ya kutosha.
Lipo suala la kuuwa watu, lipo suala la uchawi nk tote uzushi.
Ila yupo aliandika hapa kuwa zama zile za ufanyaji wa biashara za magendo, mzee Yule alikuwa na ujuzi wa kukupa maandishi katika elimu yake ya kitabu na sio mti wala kizimba wala tunguri wala uchawi Bali ni katika uwezo wa elimu yake ya kitabu, basi utakuwa salama bila kukwaruzana na askari wala kukamatwa kwa Mali yako.
Ni hakika kuwa hakuna aliyekuwa akijipendekeza kwake, Bali aliheshimiwa mno, maana hakuwa akipenda waha na wamanyema kuonewa, maskini kuonewa, wanawake na watoto kuonewa hakupenda.
Siku moja akiwa darasani kwake akisomesha elimu zake, alitokea mama mmoja akamshitakia kuwa mwanafunzi wa huyu mzee akiitwa xxxxxxx Kamo (amekuwa marehemu),alikuwa akimtaka kimapenzi kwa lazima akisema anapata masomo yenye kuburi kubwa za Juma Njemba akikataliwa atamfanyia kisomo na kumdhuru.
Mzee Juma alimuondoa masomoni mtu huyu kwa tuhuma ile akisema elimu yake ni kinga kwa watu dhaifu kutokana na mabavu ya wenye nguvu.
Kesho nitasimulia kiss chake na Mkuu wa Mkoa Kannal Mahhawa aliyeonjeshwa joto la jiwe la elimu ya mzee huyu.
Pia nitasimulia kiss cha mtumishi mwenye dharau kwa wazee alivyoikimbia ofisi kwa kuona Simba.
AbuFizzer anasema
Kiukweli katika dua na maombi alijaaliwa sana. Wapo watu waliokuwa wakiwanyanyasa wafanyakazi wageni waliohamishiwa kikazi Kigoma, engine kwa ukirsto wao au kwa ugeni wao. Yeye aliwaita hao ni wanae, aliwatetea mno, kuanzia wakuu wa mikoa, wakuu wa polis, uhamiaji nk.
Hakuna aliyethubutu kumuonea mtu kwa sababu ya ukristo wake eti kwa kuwa miaka ile Ujiji ilikuwa na waislam wengi.
Na hakuna muislam aliyeonewa kwa dino yake au uswahili wake. Leo aitwa Sangoma huyu.
Kaishi vema na Padre Yusuf wa parokia ya Kusini Katubuka. Na kawatetea wakristo chungu tele. Hakuna haki ya kuwanyanyasa akisema " hawa ni watoto wetu, Mungu hana dini, binadamu ndio tuna dini" dini ni njia ya kufika kwake Mungu.
AbuFizzer anajibu,
Aliumwa saratani, na alikuwa mtu mzima sana, alizidiwa maradhi yake akiwa kitandani kwake. Mwaka 2006/2007 na 2008 Kigoma Ujiji ilifiwa na wazee mashuhuri wakiheshimiwa kwa elimu zao. 2006 alikufa gwiji Akiitwa Selemani Apelee, mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga kabla ya kutokea, (machale) kabla ya hatari alijua, na hats majambazi walipokusudia kumuua walimpiga sana kwa mapanga na marungu, na Zaidi hawakuweza walau kumjeruhi, walipoteza nao maisha. Waliona heri wamchome moto jambo ambalo halikufanikiwa pia moto haukuwa na nguvu ya madhara kwake.
Aliwaeleza wamuache na akawauliza iwapo wanataka kumuua kweli. Walipomthibitishia alijizingua na kuwaambia wamuue. Hapo walimpiga akafa.
Kisha 2007 alikufa Mzee Juma kwa saratani, waliwaeleza familiar na majirani zake kuwa atakufa kwa matadhi Yale, aliwaita wanae watatu wa kiume na kuwapa kila mmoja vitabu na elimu zake. Hivyo alipokuwa akiumwa alikuwa tayari ana warithi wanaosimamia kumuuguza na kumtunza, huyu mzee aliwaambia wanae karibu na kifo chake kuwa siku ya kufa kwake itakuwa Alhamisi inayoisha. Na kweli alikufa Alhamisi saa tano na nusu usiku.
Mji ulikuwa na simanzi kubwa kuondokewa nae, walizika, hakukuwepo na mahangaiko yoyote au miujiza ya kutisha katika kifo chake.
Siku ya tatu alitangazwa msibani mrithi wa Kazi zake, anaechukua jina la baba yake.
Wasichokijua watu ni kuwa Juma Njemba alikuwa chief wa kabila lake hivyo pia yupo miongoni mwa wanae ni chifu. Hata Yule aliyegombea urais na Magufuli akiitwa Chief Luta Losa Yemba wa chama anachoongoza Hamad Rashid wa kule Zanzibar ni motto wa mdogo wake Juma Njemba.
Mtu wa tatu akiitwa Issa Sadick huyu nae alikuwa mzee mwenye elimu kubwa na uganga mzito sana, watu wote hawa waliwasumbua wachawi na kuwapa taabu sana, wote walipokufa ilikuwa ni faraja kwa wachawi.
Wazee hawa walikuwa ni sehemu ya kimbilio la wengi, waliwaathiri watu wenye kuiba ndoa za watu, waliwaathiri watawala wenye majivuno, na kiburi na hata sass Kigoma huwaza kuhusu Juma Njemba kwa ajili ya mtawala wetu alivyo.
LIKUD anasema
Wacha urongo..Juma Njemba alifariki mwaka 2001 na alikufa kwa kiharusi cha kisheitwani...Chanzo cha kifo chake ni kuzidiana nguvu kati ya uchawi wake na kinga ya MTU ambae Juma Njemba alitaka kumuua kwa uchawi.
Kombora alilo piga Juma Njemba kwenda kumuua MTU huyo liligonga mwamba na kumrudia yeye mwenyewe na siku kadhaa baadae alifariki dunia...Unataka nifunguke zaidi what happened ?
Juma Njemba alipigwa Back To Sender
AbuFizzer anajibu,
1. Umepatia kwa kuwa mimi na mwanae tumekuwa na makuzi mamoja, mtaa mmoja, shule moja,
2. Umepatia bint huyo alizaliwa katika miaka huyo mzee akiwa na umri unaofanana na namba uliyoitoa.
3.hapa umeweka dhana isiyo sahihi ingawa namfahamu vema huyo mwandishi.
4. Hatuko sanjari, huyu kaandika defamation kwa mzee huyu mashuhuri, kadhalilisha jina lake, kabuni matukio, na kaisemea uongo familiar yake.
Lakini kwa mtazamo wako upo huru kulinganisha masala haya kwa kadiri ya vipimo vyako.
Nakupongeza kwa umakini wako katika hoja zako zote nne.
Kuna mantiki katika andishi lako na umetumia akili katika matumizi sahihi.
Muhimu mkatazeni Likud kutukana na aache kuharibu majina ya watu kwa uzushi.
AbuFizzer anasema,
Swali zuri sana!
Huyu kwenye labial lake alikuwa ni chief, na alikuwa ni mkuu wa ngoma za makabila yake pia, acha Kigoma alikuwa ni chief wao kwa Tanzania hii, toka ikiitwa Tanganyika. 1963 Kama sikukosea nchi yetu ilifuta utaratibu wa kuwatawalisha machifu.
Lakini baadhi ya Jamii ziliendelea kuheshimu. Kama Chief Fundikira wa Nyanyembe, au Mtwa Adam Sapi, Chifu Burito wa Zanaki nk.
Yeye alikuwa chifu wao. Hivyo kwa kadiri jamii ya labial lake walivyomuheshimu, kwa kadiri ya tabia zake kwa watu wake ndivyo pia jamii kwa upana walimchukulia hivyo.
Katika tabia ninazozijua alikuwa mtu mkali sana, mwenye sauti Nene. Hivyo akikemea kwa sauti ya ukali unajua tu hapa mziki mnene.
Jina la Njemba alipewa akiwa katika umri wa Kati kwenye miaka baina ya 1947 na sitini mwanzoni, huyu alikua msanii miaka hiyo wa ngoma za kirua, aliigiza walivyokuwa wakicheza.
Pia alikuwa msanii wa vichekesho kwenye stage, na aliwahi kuwa kamanda wa TANU YOUTH LEAGUE miaka ya TANU.
Ushahidi wa haya muulizeni Meya wa Zamani wa Mji wa Kigoma Ujiji Mzee Abdallah Shaabani Tofiki. Anajua Zaidi kwa ni shuhuda wa hayo. Au mzee Ramadhani Anzuruni (KIBOKO) mzee aliyesalia kwa umri mkubwa katika eneo alilokuwa akiishi Juma Njemba.

@LIKUD anasema,
I was talking about his dark side

@LIKUD anasema
Mjomba maelezo yako ni kielelezo tosha kwamba Juma Njemba alikuwa anatisha .
Maana ana karibia miaka 20 chini ya ardhi lakini bado wamuogopa ..
Nilichoongea sijaongeza chumvi hata kidogo..Juma Njemba hakuwa MTU wa mchezomchezo ..Alikuwa hatari sana na suala la kuoa ameoa wanawake wengi sana wengi walikuwa wanaenda kilingeni kwake kama wateja na alikuwa akivutiwa nao tu basi wanakuwa wakeze..
Mke wa kwanza wa Juma Njemba ninae mfahamu Mimi aliitwa " Mkamiti Mwanalugondo" bibi wa kinyamwezi kutoka Urambo Tabora ambae na yeye alikuwa fundi kama mumewe ..Huyu alifariki akiwa mkoani Mwanza mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili.. Huyu Mwanalugondo alikuwa anatoka kwenye familia ya kichawi pia...Yeye na babu yangu kizaa baba angu walizaliwa kijiji kimoja na mwaka mmoja 1918 ambao ndio mwaka aliozaliwa Juma Njemba ..
Alikuwa na wanawake wa Kirundi kibao, wanawake wa kiarabu ndio usiseme ..Mfano pale Nzega na Tabora mjini ana watoto wengi tu ambao amezaa na wanawake wa kiarabu.
Halafu jua kuwa Juma Njemba ni kikongwe rika la kina bibi fisi wa Mwanza..
Wanafunzi wake wengi ni watu wazima kwa sasa na wengi wao wamechuja kabisa wamebakiza uchawi tu wa kuumiza watu ..Nawajua wengi tu akina Athumani Balichako na Ali Zaidi hawa wapo kanda ya ziwa lakini hawana lolote kwa sasa ...
Juma Njemba hakuwa wa dunia hii...He was something else
AbuFizzer anasema
Kiukweli katika dua na maombi alijaaliwa sana. Wapo watu waliokuwa wakiwanyanyasa wafanyakazi wageni waliohamishiwa kikazi Kigoma, engine kwa ukirsto wao au kwa ugeni wao. Yeye aliwaita hao ni wanae, aliwatetea mno, kuanzia wakuu wa mikoa, wakuu wa polis, uhamiaji nk.
Hakuna aliyethubutu kumuonea mtu kwa sababu ya ukristo wake eti kwa kuwa miaka ile Ujiji ilikuwa na waislam wengi.
Na hakuna muislam aliyeonewa kwa dino yake au uswahili wake. Leo aitwa Sangoma huyu.
Kaishi vema na Padre Yusuf wa parokia ya Kusini Katubuka. Na kawatetea wakristo chungu tele. Hakuna haki ya kuwanyanyasa akisema " hawa ni watoto wetu, Mungu hana dini, binadamu ndio tuna dini" dini ni njia ya kufika kwake Mungu.
Kaka Mimi naomba kujua kifo chake alikufajee?
AbuFizzer anajibu,
Aliumwa saratani, na alikuwa mtu mzima sana, alizidiwa maradhi yake akiwa kitandani kwake. Mwaka 2006/2007 na 2008 Kigoma Ujiji ilifiwa na wazee mashuhuri wakiheshimiwa kwa elimu zao. 2006 alikufa gwiji Akiitwa Selemani Apelee, mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga kabla ya kutokea, (machale) kabla ya hatari alijua, na hats majambazi walipokusudia kumuua walimpiga sana kwa mapanga na marungu, na Zaidi hawakuweza walau kumjeruhi, walipoteza nao maisha. Waliona heri wamchome moto jambo ambalo halikufanikiwa pia moto haukuwa na nguvu ya madhara kwake.
Aliwaeleza wamuache na akawauliza iwapo wanataka kumuua kweli. Walipomthibitishia alijizingua na kuwaambia wamuue. Hapo walimpiga akafa.
Kisha 2007 alikufa Mzee Juma kwa saratani, waliwaeleza familiar na majirani zake kuwa atakufa kwa matadhi Yale, aliwaita wanae watatu wa kiume na kuwapa kila mmoja vitabu na elimu zake. Hivyo alipokuwa akiumwa alikuwa tayari ana warithi wanaosimamia kumuuguza na kumtunza, huyu mzee aliwaambia wanae karibu na kifo chake kuwa siku ya kufa kwake itakuwa Alhamisi inayoisha. Na kweli alikufa Alhamisi saa tano na nusu usiku.
Mji ulikuwa na simanzi kubwa kuondokewa nae, walizika, hakukuwepo na mahangaiko yoyote au miujiza ya kutisha katika kifo chake.
Siku ya tatu alitangazwa msibani mrithi wa Kazi zake, anaechukua jina la baba yake.
Wasichokijua watu ni kuwa Juma Njemba alikuwa chief wa kabila lake hivyo pia yupo miongoni mwa wanae ni chifu. Hata Yule aliyegombea urais na Magufuli akiitwa Chief Luta Losa Yemba wa chama anachoongoza Hamad Rashid wa kule Zanzibar ni motto wa mdogo wake Juma Njemba.
Mtu wa tatu akiitwa Issa Sadick huyu nae alikuwa mzee mwenye elimu kubwa na uganga mzito sana, watu wote hawa waliwasumbua wachawi na kuwapa taabu sana, wote walipokufa ilikuwa ni faraja kwa wachawi.
Wazee hawa walikuwa ni sehemu ya kimbilio la wengi, waliwaathiri watu wenye kuiba ndoa za watu, waliwaathiri watawala wenye majivuno, na kiburi na hata sass Kigoma huwaza kuhusu Juma Njemba kwa ajili ya mtawala wetu alivyo.
LIKUD anasema
Wacha urongo..Juma Njemba alifariki mwaka 2001 na alikufa kwa kiharusi cha kisheitwani...Chanzo cha kifo chake ni kuzidiana nguvu kati ya uchawi wake na kinga ya MTU ambae Juma Njemba alitaka kumuua kwa uchawi.
Kombora alilo piga Juma Njemba kwenda kumuua MTU huyo liligonga mwamba na kumrudia yeye mwenyewe na siku kadhaa baadae alifariki dunia...Unataka nifunguke zaidi what happened ?
Juma Njemba alipigwa Back To Sender
1. mkuu, hapo nilipo bold na kupigia mstari nikuwa,"sio watu wakipeleka pungufu" ila ni wakileta pungufu?
kwa sentensi hiyo inaonyesha au umeonyesha kwa mausudi wewe ni sehem ya familia au ni mtoto wake?
2. Kama binti yake wa mwisho alizaliwa 1994, kwahiyo most likely alimzaa binti huyo yeye akiwa na umri wa miaka 76 au zaidi right? Na mama wa huyu binti kuna uwezekano yupo hai bado, maana inaonyesha hakuwa wa makamo sana.
3. kwa namna unavyo andika, hivi wewe sio kweli yule mwanaye ambaye ni mwandishi wa habari?
BTW, mleta uzi #Likud ni mtu ambaye ana heshima sana hapa jukwaani na, binafsi huwa sinaga mashaka naye kabisa pamoja na nduguye #barafu
Sijaona tofauti kubwa sana baina yenu juu ya Mzee Juma Njemba, kwani wewe AbuFizzer umeeleza katika kuigamia only positive side yake, jambo ambalo yeyote angefanya katika kuitetea familia yake......na #Likud ameeleza the otherside ya coin ulioishika!
AbuFizzer anajibu,
1. Umepatia kwa kuwa mimi na mwanae tumekuwa na makuzi mamoja, mtaa mmoja, shule moja,
2. Umepatia bint huyo alizaliwa katika miaka huyo mzee akiwa na umri unaofanana na namba uliyoitoa.
3.hapa umeweka dhana isiyo sahihi ingawa namfahamu vema huyo mwandishi.
4. Hatuko sanjari, huyu kaandika defamation kwa mzee huyu mashuhuri, kadhalilisha jina lake, kabuni matukio, na kaisemea uongo familiar yake.
Lakini kwa mtazamo wako upo huru kulinganisha masala haya kwa kadiri ya vipimo vyako.
Nakupongeza kwa umakini wako katika hoja zako zote nne.
Kuna mantiki katika andishi lako na umetumia akili katika matumizi sahihi.
Muhimu mkatazeni Likud kutukana na aache kuharibu majina ya watu kwa uzushi.
Kama hakuwa na power yeyote,aliwezaje kuheshimika sana na kutetea wanyonge kama usemavyo??

Last edited: