Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Hahahahahahahahahahhahahahahahah
Nimecheka sana!! Nawe hujaokoka tu
 
Bila kuroga duniani utapata pesa ya kula tu ndogo ndogo na kila biashara utakayofanya utaishia kupata hasara hata kama hiyo biashara uliifanyia utafiti wa kina na tathmin miaka 1000 bado utaishia hasara. Mshana jr njoo uwarlekeze pesa nyeusi ikoje.
Dunia simama nshuke,sio kwa spidi hii!!!
 
Kaka Mimi naomba kujua kifo chake alikufajee?
Aliumwa saratani, na alikuwa mtu mzima sana, alizidiwa maradhi yake akiwa kitandani kwake. Mwaka 2006/2007 na 2008 Kigoma Ujiji ilifiwa na wazee mashuhuri wakiheshimiwa kwa elimu zao. 2006 alikufa gwiji Akiitwa Selemani Apelee, mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga kabla ya kutokea, (machale) kabla ya hatari alijua, na hats majambazi walipokusudia kumuua walimpiga sana kwa mapanga na marungu, na Zaidi hawakuweza walau kumjeruhi, walipoteza nao maisha. Waliona heri wamchome moto jambo ambalo halikufanikiwa pia moto haukuwa na nguvu ya madhara kwake.

Aliwaeleza wamuache na akawauliza iwapo wanataka kumuua kweli. Walipomthibitishia alijizingua na kuwaambia wamuue. Hapo walimpiga akafa.

Kisha 2007 alikufa Mzee Juma kwa saratani, waliwaeleza familiar na majirani zake kuwa atakufa kwa matadhi Yale, aliwaita wanae watatu wa kiume na kuwapa kila mmoja vitabu na elimu zake. Hivyo alipokuwa akiumwa alikuwa tayari ana warithi wanaosimamia kumuuguza na kumtunza, huyu mzee aliwaambia wanae karibu na kifo chake kuwa siku ya kufa kwake itakuwa Alhamisi inayoisha. Na kweli alikufa Alhamisi saa tano na nusu usiku.

Mji ulikuwa na simanzi kubwa kuondokewa nae, walizika, hakukuwepo na mahangaiko yoyote au miujiza ya kutisha katika kifo chake.

Siku ya tatu alitangazwa msibani mrithi wa Kazi zake, anaechukua jina la baba yake.

Wasichokijua watu ni kuwa Juma Njemba alikuwa chief wa kabila lake hivyo pia yupo miongoni mwa wanae ni chifu. Hata Yule aliyegombea urais na Magufuli akiitwa Chief Luta Losa Yemba wa chama anachoongoza Hamad Rashid wa kule Zanzibar ni motto wa mdogo wake Juma Njemba.

Mtu wa tatu akiitwa Issa Sadick huyu nae alikuwa mzee mwenye elimu kubwa na uganga mzito sana, watu wote hawa waliwasumbua wachawi na kuwapa taabu sana, wote walipokufa ilikuwa ni faraja kwa wachawi.

Wazee hawa walikuwa ni sehemu ya kimbilio la wengi, waliwaathiri watu wenye kuiba ndoa za watu, waliwaathiri watawala wenye majivuno, na kiburi na hata sass Kigoma huwaza kuhusu Juma Njemba kwa ajili ya mtawala wetu alivyo.
 
Wacha urongo..Juma Njemba alifariki mwaka 2001 na alikufa kwa kiharusi cha kisheitwani...Chanzo cha kifo chake ni kuzidiana nguvu kati ya uchawi wake na kinga ya MTU ambae Juma Njemba alitaka kumuua kwa uchawi.

Kombora alilo piga Juma Njemba kwenda kumuua MTU huyo liligonga mwamba na kumrudia yeye mwenyewe na siku kadhaa baadae alifariki dunia...Unataka nifunguke zaidi what happened ?

Juma Njemba alipigwa Back To Sender
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…