Njemba kafa na mrithi wake bwana[emoji3] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ray utapotezwa shaur aki
Unataka atajwe kwa sifa asizo nazo kisa hawezi kujitetea nazoHata ungekuwa rafiki wa hiyo familia kwa kiasi gani, bado usingesema kuwa "walikuwa wakileta" ila walikuwa "wakipeleka!"
Katika maandishi yako yote, umekuwa ukiandika kwa kumtukuza na kumsifu tu, swala linaloleta swali ni kwanini hujaandika hata sentensi moja juu ya mapungufu yake given yeye alikuwa mwanadamu aliyeweza kufanya mambo yaliyo beyond!
Katika moja ya maandishi yako humu, ulisema kuwa....baada ya huyo mzee kuugua 'aliwaambia wanae kuwa "angefariki siku ya alhamis iliochelewa" na ukasema alifariki dk chache usku kabla ya ijumaa.
Ningeomba utoe ufafanuzi ni kwanini tarehe ulioisema amafariki haikuwa alhamis, na siku uiliosema alizikwa haikuwa ijumaa?
BTW, ni kuwa woote humu jukwaani tunajua zaidi mazuri ya wazazi wetu, ila the dark part zao zinafahamika sana kwa watu wa nje ya familia zaidi!
Utakuwa nawe ni miongoni mwa wanaosoma ili kujibu" lakini hapana utakuwa umesahau kuwa hujaona poppet mimi nikiwa mwanafamilia yake, hata ilipotajwa sikuandika poppet kuwa mimi ni mwanafamilia.
Sijaoa wala kuolewa!
Napata ujasiri kwa kuwa taarifa yangu Kama itakuwa na mapungufu si ya kukusudia, ninaandika matukio ya 2007 Leo mwaka 2018. Huku nikiwa lengo langu ni kujustfy tens kwa maana ya nilichoshuhudia sio nilichoambiwa.
Zaidi nukta ya kasoro ya kalenda sio nzito Zaidi ya nukta ya kuuwa watu 2000 na bado akatukuzwa. Nani alikuwa anahesabu vifo hivyo? Ilikuwa wapi na wapi waliishi wakauliwa? Aliyetoa Siri hizi nani? Aliuwa akiombwa na nani? Au aliuwa tu hovyo hovyo?
Ushahidi wa haya uko wapi?
Kuhusu nukta ya tarehe sio kubwa iwapo tayari kuna mtu ameonesha kuwa May mwaka 2007 aliondoka Kigoma na miezi kadhaa iliyofuatia alipata taarifa ya kifo hicho.
Iweje bado hujaonesha upungufu wa mwaka alioutaja bosi kachumvi 2001? Lakini ukaona nukta hiyo hiyo ya kalenda ni muhimu kwangu.
Hats hivyo napendezwa sana na udadisi wako....karibu
Unataka atajwe kwa sifa asizo nazo kisa hawezi kujitetea nazo
Na waogope Sana watu wanaopewa third hand information kisha wakazifanyia kaziNyote mlihadithiwa lakini hamkumuona, hamkuzungumza nae, hamkumuhoji, yaani nyie ni "third hand information" na bado mnaushawishi umma uwaelewe kuwa mlichoambiwa ni kweli.
Nacheka[emoji6][emoji847][emoji6]
Watembeleeni wachamungu mpate kuondolewa nira mashingoni mwenu.
Unataka atajwe kwa sifa asizo nazo kisa hawezi kujitetea nazo
Ngumu kuverify si yupo likud aliyesema alikuwa na wake 200Sasa kwanini unadhani unafaa tukuamini?
1.Umefail kwny tarehe yake ya kufa na kuzikwa
2. Ulichioweza ni kuleta majina na idadi ya familia ya huyo Juma, ambayo ni ngumu kwa yyte humu ku verify kama usemacho ni kweli.
3. Umejikita only kuongea positive side bila ya angalau kijihusisha na anacho kiongea mleta mada na member wengine humu waliofika kilingeni kwake na kukubaliana na Likud
4. unakanusha tu anachosema Likud basi, yaani kama kuna kitu au jambo hutaki lisimwe
Wachawi alafu familia zao huwa za kimaskini sana ingawa zilipendelewa na wakoloni.Machifu ni wachawi mno!!
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.
Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.
Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.
Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.
Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu.
Kwa zaidi ya miaka ishirini aliyo Fanya kazi hii, Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka
Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana.
Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke aliyepika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika.
KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."
Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.
Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..
MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.
Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.
Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.
"Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "
" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.
Hata hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.
Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.
Juma Njemba alifariki mwaka 2001. Waliokuwa NAE karibu wakati wa kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..
Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.
Juma Njemba alifanya vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua
Ngumu kuverify si yupo likud aliyesema alikuwa na wake 200
Hiii ndio species ya lwama kweli hakutoki bwegeUtakuwa nawe ni miongoni mwa wanaosoma ili kujibu" lakini hapana utakuwa umesahau kuwa hujaona poppet mimi nikiwa mwanafamilia yake, hata ilipotajwa sikuandika poppet kuwa mimi ni mwanafamilia.
Sijaoa wala kuolewa!
Napata ujasiri kwa kuwa taarifa yangu Kama itakuwa na mapungufu si ya kukusudia, ninaandika matukio ya 2007 Leo mwaka 2018. Huku nikiwa lengo langu ni kujustfy tens kwa maana ya nilichoshuhudia sio nilichoambiwa.
Zaidi nukta ya kasoro ya kalenda sio nzito Zaidi ya nukta ya kuuwa watu 2000 na bado akatukuzwa. Nani alikuwa anahesabu vifo hivyo? Ilikuwa wapi na wapi waliishi wakauliwa? Aliyetoa Siri hizi nani? Aliuwa akiombwa na nani? Au aliuwa tu hovyo hovyo?
Ushahidi wa haya uko wapi?
Kuhusu nukta ya tarehe sio kubwa iwapo tayari kuna mtu ameonesha kuwa May mwaka 2007 aliondoka Kigoma na miezi kadhaa iliyofuatia alipata taarifa ya kifo hicho.
Iweje bado hujaonesha upungufu wa mwaka alioutaja bosi kachumvi 2001? Lakini ukaona nukta hiyo hiyo ya kalenda ni muhimu kwangu.
Hats hivyo napendezwa sana na udadisi wako....karibu
Inapendeza ukiwa unaujuaIssue hapa ni kutetea piga ua, Au issue hapa ni kuongea ukweli?
Nakufahamisha tena na tena!!Wewe ndio unajichanganya, umekiri indirect kuwa "wakti zikiletwa malipo pungufu'. Kumbuka zikiletwa ni ama kwangu ama kwetu. Zikipelekwa ni ama kwake ama kwao. Kwahiyo, kujifumbua huku ni kwa bahati mbaya umrkufanya bila kuwa ulikusudia. Hivyo usikanushe kuwa hujasema wewe ni sehemu ya uhusika wa famillia ila jitahdi kuendelea kuoaruka!
Swala la tarehe ni no excuse, limekufanya kulitia doa andiko lako, maana ni key issue ya mjadala huu, na pia inafanya tuzidi kuamni maelezo ya mtoa mada.
Kuna member mmoja humu amekiri kuwa mteja wa huyo mzee, na kwamba alitoroka kabla ya kumaliza dozi. Anakiri maelezo ya mleta mada ni ya kweli na kuwa, ni kweli kuwa Njemba alikuwa specialist wa kuuwa. Sasa embu jiulize alikuwa na wateja wangapi kwa siku kutoka kila kona nchini na nje ya mipaka? Chukua hio idadi kwa siku, kisha ifanye mara miaka aliofanya hio kazi....hivi huoni kuwa mleta mada naye anaweza awe amepunguza idadi?
Kauli yako, they way unatetea, ni kama kutakuwa na revenji kwa familia juu ya vifo vyoote hivyo.
Unaweza ututajie tena tarehe ya kifo chake, na tarehe ya kuzikwa kwake ulizofanyia mabadiliko?
Endelea mkuu kushusha nondo kuhusu Njemba..ubishi hauwez kuishaUtawaponza wenzako wakose utamu maana nataka nishushe nondo ..
HapanaInawezekanaje mtu aliye mwema kabisa akawa anaogopwa?
Wewe ni fasaha wa kuandikaNakufahamisha tena na tena!!
Ukimgusa mzee huyo umeugusa mtaa alioishi na jamii yake. Hivyo mimi ni sehemu ya watu wa mtaa huo. Sipingi kuwa hivyo
"zikiletwa" inategemea wakati huo nilikuwa upande gani, nipo mtaani kwangu na waletaji wameleta hapo. Nawezaje kusema "zikipelekwa"??
Kuhusu mjadala huu key point yake haiwezi kuwa tarehe ya kifo, kwa kuwa hatukupishana katika suala tarehe ya kufa kwake. Bali mwaka wa kufa kwake. Yeye alisema 2001 na mimi nilisema 2007. Yupo aliyesema pia 2007. Hivyo ukijustfy hapo utagundua nani alisema uongo.
Iwapo njema alikuwa specialist wa kuuwa ushahidi unatoka wapi?? Kuwa kuna "specialisation" hiyo. Bado ndugu yangu kaweka namba ithibati ya idadi hiyo ikiwa pungufu au kamili unaipataje? Lazima ukiwa timamu utatambua kuwa ni ubunifu.
Njemba aliyeishi Kama mtu wa peponi hata baiskeli hakuwa nayo, pepo ya daraja gani?
Lakini Zaidi ni idadi ya wake zake 200 kwa ushahidi upi?? Haya ni mazingaombwe tu. Na katika kauli zangu bado silazimishi yeyote akubali ninachoandika Kama nisivyokubali uongo wowote unaoandikwa dhidi ya mzee yule