Kwa hiyo unatutisha?Juma Njemba alikuwa mjomba wangu...wanashare mama na mama yangu
Usimuudhi mkuuWe huna hata tunguli aka rada?
Kumbe?LIKUD hiyo ya kufa na hiyo ya kupikwa kwenye pipa alifanyiwa zzk hadi leo ndio maana anajiamini yule mtoto , na ukicheza na zitto kwenye mila anakuondoa , yule dogo alifaidi dawa zile wengine tulishtuka alishakufa.
Tawire mkuuUsimuudhi mkuu
UjijiJuma Njemba alikuwa akiishi Kigoma sehemu gani?
Ungekuwepo najua ungemzibitiWengi hufa siku saba
Angepata tabu sana[emoji23]Ungekuwepo najua ungemzibiti
alikuwa anawabandua bure...?Nilisoma na mtoto wake alikuwa anawati
shia watoto wakike hatar walikuwa wanamuogopa
FUNGUA UZI WAKOHukufanya tafiti juu ya Mzee huyu nitarudi kuelezea juu ya habari zake kuliko kuendelea kupotosha
Nakumbukua nilitembelea Ujiji mwaka 2013 nikaenda kwenye BEACH YA LIVINGSTONE pale ndo nikakuta story hii. Jamaa alikuwa anaogopwa sana huyu ila kwa Mungu kila kitu kina zama zake!Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.
Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.
Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.
Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.
Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu .
Kwa zaidi ya miaka.ishirini aliyo Fanya kazi hii Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka
Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana ..
Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au.Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke alie pika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika .
KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."
Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.
Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..
MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.
Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.
Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.
" Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "
" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.
Hata.hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.
Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.
Juma Njemba alifariki mwaka 2001.Walio kuwa NAE karibu wakati wa.kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..
Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.
Juma Njemba alifany vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua
Hapana mkuu! Nilijaribu kudadisi wazee kadhaa juu ya hii habar wanilithibitishia ni kweliHistoria ya kusadikika
DuuuLIKUD nakushukuru kuknikumbusha story ya mzee wangu wa ujiji huyu mzee kwa wafanyabiashara wa mikoa ya Tabora, Mwanza, Kigoma, Shinyanga na wale wa nchi kama Rwanda na Burundi ikiwamo Congo watakumbuka zindiko lake la kupita na magendo bila kuonwa wala kukamatwa na askari na dawa ile ilikua mnapita mnaondoka askari mnawaona wao hawawaoni hata iwe mchana.