Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Urakoze chane mzee baba..Shusha nondo zako ..mi.nilisimuliwa wakati nafanya utafiti wangu kuhusu uchawi wa kimanyema pale ujiji mwaka 2016
Tutulie tutamjua Mzee Njemba tuuu
 
aliyerithishwa mikoba hiyo ni nani???
Je, nae anaendeleza kazi hiyo mpka sasa??
Ni nani anayesifika kwa uchawi kwa sasa pande hizo???
 
Nimesoma story hii, kwanza nikupongeze kwa kuweza kuandika ulichoandika, lakini nikukosoe kuwa hukuandika ukweli wa mambo kabisa.

Mtu huyu uliyemuandika mimi nimeishi nae mtaa mmoja, barabara moja, kata moja na Zaidi nimesoma na wanae, ninaijua familiar yake na historian nzima ya maisha ya marehemu mzee huyu.

Ni mtu aliyekuwa maarufu sana, na mjuzi sana wa kitabu na masala ya hesabu za nujumu.

Mtu huyu kwa awamu tofauti aliwahi kuwa msanii wa ngoma za asili, mtoza ushuru, fundi muashi, mwanafunzi, dobi, mwanasiasa, mfabiashara, mtu wa elimu ya nyota, dua, na nyiradi za tiba kwa wanadamu.

Alikuwa mtu mkarimu na mwenye umri mkubwa katika eneo aliloishi. Ni vema kutambua kuwa kwa andiko hili mimi na engine tunaoamini andiko hili halikufanyiwa utafiti wa kutosha kuandika kwa ajili ya kukabili upotoshaji wa kihistoria uliopo katika andiko lako.

Hii itasaidia jamii kumfahamu mtu huyu nguli wa elimu ya hesabu, nyota, dua na nyiradi ambaye alifahamika kwa watu bila kutumia vyombo vya habari, kinyume na wengi waliotumia vyombo vya habari kama marehemu Sheikh Yahya Hassan (akifahamika kwa jina la Yahya Hussein).

Pia itasaidia kuondoa simanzi kwa familiar yake kutokana na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na baadhi ya watu, ambao kwa sababu zao binafsi wanatumia vidole (kalamu) kupotosha historia ya mzee wao.

Ambaye alikuwa mtu asiye na ubaguzi wa kidini rangi au jinsia, alihofiwa na alipendwa, alitiiwa na aliwatii watu wake, alikirimiwa na alikirimu, aliaminiwa na kuitwa "baba wa mji"

Mzee Juma Njemba halikuwa jina lake Bali ilikuwa Lakabu yake, yeye haswa alikuwa na lakabu kadhaa kabla ya hiyo.

Miongoni mwa lakab zake (kun-ya) nickname zake ni Juma wa Mwanga, Njemba, Lubambala, Ng'anga nk.

Mzee huyu alizaliwa Mji wa kale wa Ujiji, katika kitongoji kidogo cha Kasimbu barabara ya Msafiri. Baba yake aliitwa Abdallah na mama yake aliitwa Johari Bint Lwamba.

Mzee Juma alizaliwa mwaka baina ya mwaka 1918 na 1920 kumbukumbu zinaonesha kuwa alikuwa miongoni mwa watu wenye umri mkubwa licha ya kuwa hakuwa mkubwa Zaidi ya babu yake Abdul Nondo ( mzee Haji Mitumba)

Alizaliwa katika familia ya watoto watatu wa kiume, Mussa akiwa mkubwa, yeye na mdogo wao akiitwa Bushiri.

Nitaendelea kadiri ya muda utakavyokuwa unapatikana
kama alikuwa kama shehe yahya akiitwa mchawi/mshirikina ni sahihi kabisa.
 
I was talking about his dark side
Even dark of his, umeweka uwongo mwingi sana. Juma Njemba aliowa wake kwa dini ya kiislam, aliishi an wake wanne, akihitilafiana au kufiwa na mke aliongeza mke kwa kuoa mwingine. Hakudhulum mke wa mtu, alichumbia na kukubaliwa akaowa, alipokataliwa posa take hakuoa na hakudhuru mtu.

Pia umeandika kuhusu kuacha na kudhuru wenzi wake aliotalakiana nao, jambo ambalo si la kweli, mke wake wa kwanza akiitwa Bi. mtumwa bint Ali Saad, mwanamke huyu aliishi toka ujana hats kifo na mumewe na hawakujaliwa kupata mtoto.

Mke wake wa pili akiitwa Hawa bint Almas Msano mpaka leo anaishi Sengerema Mwanza amekuwa ajuza kwa umri wake alizaa nae bint aliyeitwa Asha.

Mke wa tatu sikumbuki jina lake lakini alizaa watoto wawili mmoja akiitwa Lwamba na Mwingine Mwamvua. Mwanamke huyu waliachana muda mrefu kwa mke huyu kurejea kwao Urambo ambako kaka yake alikuwa na uchumi hivyo aliamua kuachana na ndoa kuendelea kusimamia uchumi (pengine walikuwa na yao) lakini hakumuuwa wala hakukuwa na madhara, mama huyu kafa mwaka juzi 2016 Tanga Mjini.

Alimuoa pia mama wa kisenegal akazaa bint akiitwa Johari, mama Yule walitengana na hakumdhuru alifariki mwaka 2014 akiwa mtu mzima.

Alimuoa mwanamke mwingine akazaa nae mtoto wa kiume akiitwa Mwinyimbegu yupo mtu huyu pale Kigoma Ujiji na mama yake yu hai na hana madhara.

Alioa mwanamke wa kiha akiitwa Bora bint Maulid mungo mkuyu huyu kazaa nae watoto wanne. Wawili wa kiume wapo Dar Es salaam pale jiran ya Meeda Bar Sinza. Tena wapo na mama yao ambaye aliishi na marehemu mpaka kufa kwake. Na wawili wa kike mmoja ni mwalimu Mwanza na mwingine yupo huko Ujiji kwao.

Hivyo umeweka chumvi ya kutosha.

Lipo suala la kuuwa watu, lipo suala la uchawi nk tote uzushi.

Ila yupo aliandika hapa kuwa zama zile za ufanyaji wa biashara za magendo, mzee Yule alikuwa na ujuzi wa kukupa maandishi katika elimu yake ya kitabu na sio mti wala kizimba wala tunguri wala uchawi Bali ni katika uwezo wa elimu yake ya kitabu, basi utakuwa salama bila kukwaruzana na askari wala kukamatwa kwa Mali yako.

Ni hakika kuwa hakuna aliyekuwa akijipendekeza kwake, Bali aliheshimiwa mno, maana hakuwa akipenda waha na wamanyema kuonewa, maskini kuonewa, wanawake na watoto kuonewa hakupenda.

Siku moja akiwa darasani kwake akisomesha elimu zake, alitokea mama mmoja akamshitakia kuwa mwanafunzi wa huyu mzee akiitwa xxxxxxx Kamo (amekuwa marehemu),alikuwa akimtaka kimapenzi kwa lazima akisema anapata masomo yenye kuburi kubwa za Juma Njemba akikataliwa atamfanyia kisomo na kumdhuru.

Mzee Juma alimuondoa masomoni mtu huyu kwa tuhuma ile akisema elimu yake ni kinga kwa watu dhaifu kutokana na mabavu ya wenye nguvu.

Kesho nitasimulia kiss chake na Mkuu wa Mkoa Kannal Mahhawa aliyeonjeshwa joto la jiwe la elimu ya mzee huyu.

Pia nitasimulia kiss cha mtumishi mwenye dharau kwa wazee alivyoikimbia ofisi kwa kuona Simba.
 
Mwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
Dokezo kidogo mkuu....
 
Hakufa wapo wawili sio mkoba Bali elimu ya kitabu na kuburi tu. Hats wachungaji wapo wenye nguvu na uwezo wa Mungu katika kuitikiwa maombi
Ninaemjua alikufa ..hao unao wasema labda walikuwa " wahemba" wanafunzi wake
 
Back
Top Bottom