Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tutulie tutamjua Mzee Njemba tuuuUrakoze chane mzee baba..Shusha nondo zako ..mi.nilisimuliwa wakati nafanya utafiti wangu kuhusu uchawi wa kimanyema pale ujiji mwaka 2016
Tungekuwa tushazika LIKUD kitaambo,tena kisu cha usoSipati picha kama huyo Juma Njemba angekua member wa humu Jf..... tehteehhh
Naomba namba yake mkuuWatu wa namna hiyo wapo katika jamii ndio maana vifo vingi sio vya Mungu. Kuna njemba mmoja anamkamua kiboko maziwa ambayo anachanganya na miti fulani, akirusha hewani tu na kunuia jina husika unaondoka
Ras nyoka tu wa mafia ulimshindwa au kwakua uchäwì hauvuki majiAngepata tabu sana[emoji23]
kama alikuwa kama shehe yahya akiitwa mchawi/mshirikina ni sahihi kabisa.Nimesoma story hii, kwanza nikupongeze kwa kuweza kuandika ulichoandika, lakini nikukosoe kuwa hukuandika ukweli wa mambo kabisa.
Mtu huyu uliyemuandika mimi nimeishi nae mtaa mmoja, barabara moja, kata moja na Zaidi nimesoma na wanae, ninaijua familiar yake na historian nzima ya maisha ya marehemu mzee huyu.
Ni mtu aliyekuwa maarufu sana, na mjuzi sana wa kitabu na masala ya hesabu za nujumu.
Mtu huyu kwa awamu tofauti aliwahi kuwa msanii wa ngoma za asili, mtoza ushuru, fundi muashi, mwanafunzi, dobi, mwanasiasa, mfabiashara, mtu wa elimu ya nyota, dua, na nyiradi za tiba kwa wanadamu.
Alikuwa mtu mkarimu na mwenye umri mkubwa katika eneo aliloishi. Ni vema kutambua kuwa kwa andiko hili mimi na engine tunaoamini andiko hili halikufanyiwa utafiti wa kutosha kuandika kwa ajili ya kukabili upotoshaji wa kihistoria uliopo katika andiko lako.
Hii itasaidia jamii kumfahamu mtu huyu nguli wa elimu ya hesabu, nyota, dua na nyiradi ambaye alifahamika kwa watu bila kutumia vyombo vya habari, kinyume na wengi waliotumia vyombo vya habari kama marehemu Sheikh Yahya Hassan (akifahamika kwa jina la Yahya Hussein).
Pia itasaidia kuondoa simanzi kwa familiar yake kutokana na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na baadhi ya watu, ambao kwa sababu zao binafsi wanatumia vidole (kalamu) kupotosha historia ya mzee wao.
Ambaye alikuwa mtu asiye na ubaguzi wa kidini rangi au jinsia, alihofiwa na alipendwa, alitiiwa na aliwatii watu wake, alikirimiwa na alikirimu, aliaminiwa na kuitwa "baba wa mji"
Mzee Juma Njemba halikuwa jina lake Bali ilikuwa Lakabu yake, yeye haswa alikuwa na lakabu kadhaa kabla ya hiyo.
Miongoni mwa lakab zake (kun-ya) nickname zake ni Juma wa Mwanga, Njemba, Lubambala, Ng'anga nk.
Mzee huyu alizaliwa Mji wa kale wa Ujiji, katika kitongoji kidogo cha Kasimbu barabara ya Msafiri. Baba yake aliitwa Abdallah na mama yake aliitwa Johari Bint Lwamba.
Mzee Juma alizaliwa mwaka baina ya mwaka 1918 na 1920 kumbukumbu zinaonesha kuwa alikuwa miongoni mwa watu wenye umri mkubwa licha ya kuwa hakuwa mkubwa Zaidi ya babu yake Abdul Nondo ( mzee Haji Mitumba)
Alizaliwa katika familia ya watoto watatu wa kiume, Mussa akiwa mkubwa, yeye na mdogo wao akiitwa Bushiri.
Nitaendelea kadiri ya muda utakavyokuwa unapatikana
Ile wakanda ni kwa watu spesho!.. Sasa nyie hadi mbunge wenu anajisifu wazi, wazee wa mwisho wa reli.Why kigoma???
Mnatusema vibaya wakati huko kwenu mna kijiji chenu kabisa/ gamboshii
😁😁😁😁Ile wakanda ni kwa watu spesho!.. Sasa nyie hadi mbunge wenu anajisifu wazi, wazee wa mwisho wa reli.
Mwisho ndio hapo kigoma ujiji mbele ni ziwani labda useme nyuma yake kidogo wachepuke waende BurundiHuyu itakuwa ndie amesababisha pawe mwisho wa Reli(isiendelee mbele).
Naomba uniroge[emoji445]Mi uchawi naotumia unatoka Ur of the Chaldeans. Mshana Jr anaujua..Maana hata uchawi wa kilebanenga hautii maguu
Even dark of his, umeweka uwongo mwingi sana. Juma Njemba aliowa wake kwa dini ya kiislam, aliishi an wake wanne, akihitilafiana au kufiwa na mke aliongeza mke kwa kuoa mwingine. Hakudhulum mke wa mtu, alichumbia na kukubaliwa akaowa, alipokataliwa posa take hakuoa na hakudhuru mtu.I was talking about his dark side
Dokezo kidogo mkuu....Mwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
Hakufa wapo wawili sio mkoba Bali elimu ya kitabu na kuburi tu. Hats wachungaji wapo wenye nguvu na uwezo wa Mungu katika kuitikiwa maombiAlikufa ..
Daahh,we ndo umemaliza kabisa mkuu.Angalao kapicha basi, akipita sokoni...