Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

mimi niluwahi kwenda kwa huyo mzee lakini niliogopa kumalizia zindiko la milango saba ya ziwa tanganyika, nikaondoka kwa kutoroka tukiwa mlango wa tatu , nadhani umenikumbusha mbali mno wala hujakosea kitu.
Kwa nini uliogopa
 
LIKUD hiyo ya kufa na hiyo ya kupikwa kwenye pipa alifanyiwa zzk hadi leo ndio maana anajiamini yule mtoto , na ukicheza na zitto kwenye mila anakuondoa , yule dogo alifaidi dawa zile wengine tulishtuka alishakufa.
Viongozi wengi wa East Africa wa kipindi hicho walipikwa na Juma Njemba
 
Umenikumbusha mbali sana kuna siku nilikutana naye mitaa ya ujiji kagera pale niliruka nyumba moja ya nyasi hivi speed 120km/hr
Kwa nini ulikuwa unamuogopa
 
Mwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
 
Nimesoma story hii, kwanza nikupongeze kwa kuweza kuandika ulichoandika, lakini nikukosoe kuwa hukuandika ukweli wa mambo kabisa.

Mtu huyu uliyemuandika mimi nimeishi nae mtaa mmoja, barabara moja, kata moja na Zaidi nimesoma na wanae, ninaijua familiar yake na historian nzima ya maisha ya marehemu mzee huyu.

Ni mtu aliyekuwa maarufu sana, na mjuzi sana wa kitabu na masala ya hesabu za nujumu.

Mtu huyu kwa awamu tofauti aliwahi kuwa msanii wa ngoma za asili, mtoza ushuru, fundi muashi, mwanafunzi, dobi, mwanasiasa, mfabiashara, mtu wa elimu ya nyota, dua, na nyiradi za tiba kwa wanadamu.

Alikuwa mtu mkarimu na mwenye umri mkubwa katika eneo aliloishi. Ni vema kutambua kuwa kwa andiko hili mimi na engine tunaoamini andiko hili halikufanyiwa utafiti wa kutosha kuandika kwa ajili ya kukabili upotoshaji wa kihistoria uliopo katika andiko lako.

Hii itasaidia jamii kumfahamu mtu huyu nguli wa elimu ya hesabu, nyota, dua na nyiradi ambaye alifahamika kwa watu bila kutumia vyombo vya habari, kinyume na wengi waliotumia vyombo vya habari kama marehemu Sheikh Yahya Hassan (akifahamika kwa jina la Yahya Hussein).

Pia itasaidia kuondoa simanzi kwa familiar yake kutokana na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na baadhi ya watu, ambao kwa sababu zao binafsi wanatumia vidole (kalamu) kupotosha historia ya mzee wao.

Ambaye alikuwa mtu asiye na ubaguzi wa kidini rangi au jinsia, alihofiwa na alipendwa, alitiiwa na aliwatii watu wake, alikirimiwa na alikirimu, aliaminiwa na kuitwa "baba wa mji"

Mzee Juma Njemba halikuwa jina lake Bali ilikuwa Lakabu yake, yeye haswa alikuwa na lakabu kadhaa kabla ya hiyo.

Miongoni mwa lakab zake (kun-ya) nickname zake ni Juma wa Mwanga, Njemba, Lubambala, Ng'anga nk.

Mzee huyu alizaliwa Mji wa kale wa Ujiji, katika kitongoji kidogo cha Kasimbu barabara ya Msafiri. Baba yake aliitwa Abdallah na mama yake aliitwa Johari Bint Lwamba.

Mzee Juma alizaliwa mwaka baina ya mwaka 1918 na 1920 kumbukumbu zinaonesha kuwa alikuwa miongoni mwa watu wenye umri mkubwa licha ya kuwa hakuwa mkubwa Zaidi ya babu yake Abdul Nondo ( mzee Haji Mitumba)

Alizaliwa katika familia ya watoto watatu wa kiume, Mussa akiwa mkubwa, yeye na mdogo wao akiitwa Bushiri.

Nitaendelea kadiri ya muda utakavyokuwa unapatikana
 

I was talking about his dark side
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…