jembelamkono
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 2,733
- 2,012
BILASHAKA WATAKUWA WALIAMBULIA KIDOGO KAILIMUWatoto wake hawakurithi mikoba?
Alirithishwa mjukuu ila na yeye alikufa soon thereafter ..Alitumiwa majambazi wa kirundi
Angalao kapicha basi, akipita sokoni...
Ndio Dawa yao hao washamba,wasiopenda mawazo mbadala.LIKUD hiyo ya kufa na hiyo ya kupikwa kwenye pipa alifanyiwa zzk hadi leo ndio maana anajiamini yule mtoto , na ukicheza na zitto kwenye mila anakuondoa , yule dogo alifaidi dawa zile wengine tulishtuka alishakufa.
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.
Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.
Sifa za Juma Njemba zilienea katika mji wa kigoma na nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda.
Mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali walifurika kilingeni kwa Juma Njemba kwa ajili ya kazi moja tu ambayo ni kuwaua adui zao kwa kutumia uchawi wa Juma Njemba.
Kazi hii ya kuua watu kwa uchawi ilimtajirisha sana bwana huyu .
Kwa zaidi ya miaka.ishirini aliyo Fanya kazi hii Juma Njemba anakadiriwa kuwa amewauwa kichawi takribani watu elfu mbili na ushee ambao ni sawa na wastani wa karibu watu mia kwa mwaka
Juma Njemba alioa wanawake wengi sana .Anakadiriwa kuwa alioa zaidi ya wanawake 200 huku wengi kati yao akiwa anawaoa na kuwaacha na aliwaacha kwa sababu ndogo sana ..
Kwa mfano akiwa anakula chakula halafu kikawa kimezidi chumv, au chai ikapungua au.Kuzidi sukari au akatafuna jiwe kwenye wali basi mwanamke alie pika chakula hicho atapewa talaka tatu papo hapo na wataliki wake wote walikuwa wanaishia kufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya muda mfupi na walio bahatika kuishi basi waliishia kuwa vichaa au kuugua maradhi mazito kama vile kiharusi nakadhalika .
KATIKA HILO SABABABU YAKE ILIKUWA " WAKE ZANGU KWA MAISHA NINAYO ISHI MIMI SIWEZI KWENDA PEPONI..PEPO YANGU NI HAPA HAPA DUNIANI ..PEPONI HAKUNA WALI WENYE MCHANGA WALA ULIOZIDI CHUMVI..SITAKI KUPATA TABU YA AINA YOYOTE ILE HAPA DUNIANI NA YEYOTE ATAKAE NISABABISHIA TABU YA AINA YOYOTE ILE BASI NITAMFUTILIA MBALI..."
Ukiachilia mbali mke wake wa kwanza na wa pili ambao aliwaoa wakati wa ujana wake kabla hajapata hiyo ilmu ya kuua watu kwa uchawi wake zake wote alikuwa anawaoa wakiwa bikira na alikuwa akiamini.wakeze hao walikuwa ni ma hurulain wake wa hapa DUNIANI.
Akimpenda binti yako basi anatuma tu ujumbe kuwa siku fulani atakuwa mgeni wako ambapo atakuja kumposa binti yako na hakuna mzazi ambae alikataa kumuozesha bintiye kwa Juma Njemba.Walio thubutu kufanya hivyo walikufa wao au binti zao au wote kwa pamoja..
MTU huyu aliogopwa kama Mungu..Wageni walio Tembelea katika kata aliyo ishi kwa sababu mbalimbali walikuwa wanaenda kuripoti na zawadi kwa Juma Njemba na wakati wa kuondoka walienda kumuaga kwa heshima zote.
Siku moja moja.alikuwa anapenda kuhemea soko kuu la pale Ujiji Kigoma.
Wafanyabiashara wa sokoni hapo walikuwa wakimuona walikuwa wakijipendekeza kwa kumuomba wampe bidhaa zao bure.
" Baba pitia hapa dukani kwangu uchukue walau kilo kumi za nyama baba ..Hii ni swadaka yangu kwako "
" Baba ukitoka buchani upitie hapa kilo 20 za mchele bill itakuwa kwangu" .Hayo ni maneno ya baadhi ya wafanya biashara wakijipendekeza kwa Juma Njemba.
Hata.hivyo Juma Njemba alikuwa akikataa ofa hizo za nidhamu ya uwoga kwa kuwaambia kwamba yeye ana uwezo kuliko wao.
Ilikuwa ukimdhulumu MTU basi ataenda kulalamika kwa Juma Njemba halafu Juma Njemba atatuma ujumbe wa kukuita na ukifika atakwambia ulimpe deni lake.
Juma Njemba alifariki mwaka 2001.Walio kuwa NAE karibu wakati wa.kifo chake wanasema kilikuwa ni kifo cha mateso makubwa sana..
Watu wa Kigoma waliposikia Juma Njemba amefariki walifanya sherehe kubwa sana.
Juma Njemba alifany vituko na matukio Mengi sana ya kichawi ..Nikipata nafasi nitakuwa natupia kimoja baada ya Kingine ili watu waweze kujua
Hii ndio Jf bana ,Asante kwa kuweka mambo sawaEven dark of his, umeweka uwongo mwingi sana. Juma Njemba aliowa wake kwa dini ya kiislam, aliishi an wake wanne, akihitilafiana au kufiwa na mke aliongeza mke kwa kuoa mwingine. Hakudhulum mke wa mtu, alichumbia na kukubaliwa akaowa, alipokataliwa posa take hakuoa na hakudhuru mtu.
Pia umeandika kuhusu kuacha na kudhuru wenzi wake aliotalakiana nao, jambo ambalo si la kweli, mke wake wa kwanza akiitwa Bi. mtumwa bint Ali Saad, mwanamke huyu aliishi toka ujana hats kifo na mumewe na hawakujaliwa kupata mtoto.
Mke wake wa pili akiitwa Hawa bint Almas Msano mpaka leo anaishi Sengerema Mwanza amekuwa ajuza kwa umri wake alizaa nae bint aliyeitwa Asha.
Mke wa tatu sikumbuki jina lake lakini alizaa watoto wawili mmoja akiitwa Lwamba na Mwingine Mwamvua. Mwanamke huyu waliachana muda mrefu kwa mke huyu kurejea kwao Urambo ambako kaka yake alikuwa na uchumi hivyo aliamua kuachana na ndoa kuendelea kusimamia uchumi (pengine walikuwa na yao) lakini hakumuuwa wala hakukuwa na madhara, mama huyu kafa mwaka juzi 2016 Tanga Mjini.
Alimuoa pia mama wa kisenegal akazaa bint akiitwa Johari, mama Yule walitengana na hakumdhuru alifariki mwaka 2014 akiwa mtu mzima.
Alimuoa mwanamke mwingine akazaa nae mtoto wa kiume akiitwa Mwinyimbegu yupo mtu huyu pale Kigoma Ujiji na mama yake yu hai na hana madhara.
Alioa mwanamke wa kiha akiitwa Bora bint Maulid mungo mkuyu huyu kazaa nae watoto wanne. Wawili wa kiume wapo Dar Es salaam pale jiran ya Meeda Bar Sinza. Tena wapo na mama yao ambaye aliishi na marehemu mpaka kufa kwake. Na wawili wa kike mmoja ni mwalimu Mwanza na mwingine yupo huko Ujiji kwao.
Hivyo umeweka chumvi ya kutosha.
Lipo suala la kuuwa watu, lipo suala la uchawi nk tote uzushi.
Ila yupo aliandika hapa kuwa zama zile za ufanyaji wa biashara za magendo, mzee Yule alikuwa na ujuzi wa kukupa maandishi katika elimu yake ya kitabu na sio mti wala kizimba wala tunguri wala uchawi Bali ni katika uwezo wa elimu yake ya kitabu, basi utakuwa salama bila kukwaruzana na askari wala kukamatwa kwa Mali yako.
Ni hakika kuwa hakuna aliyekuwa akijipendekeza kwake, Bali aliheshimiwa mno, maana hakuwa akipenda waha na wamanyema kuonewa, maskini kuonewa, wanawake na watoto kuonewa hakupenda.
Siku moja akiwa darasani kwake akisomesha elimu zake, alitokea mama mmoja akamshitakia kuwa mwanafunzi wa huyu mzee akiitwa xxxxxxx Kamo (amekuwa marehemu),alikuwa akimtaka kimapenzi kwa lazima akisema anapata masomo yenye kuburi kubwa za Juma Njemba akikataliwa atamfanyia kisomo na kumdhuru.
Mzee Juma alimuondoa masomoni mtu huyu kwa tuhuma ile akisema elimu yake ni kinga kwa watu dhaifu kutokana na mabavu ya wenye nguvu.
Kesho nitasimulia kiss chake na Mkuu wa Mkoa Kannal Mahhawa aliyeonjeshwa joto la jiwe la elimu ya mzee huyu.
Pia nitasimulia kiss cha mtumishi mwenye dharau kwa wazee alivyoikimbia ofisi kwa kuona Simba.
Hii ya kwenda kuzimu ipoje mkuu? Hebu jazia nyama story ya Joseph kabaseleHilo zindiko ni hatari sana linahitaji ujasiri wa hali ya juu..Alikuwaga pia na zindiko la kumzika MTU kaburini, MTU kupikwa kwenye pipa pamoja na Yale ya " kusafiri" kwenda kuzimu kama lile lililo muua Joseph Kabasele
Hii ni ya Kweli??? Duuh inatishaKisa chake cha mwisho huyu bwana alishawahi kumpa mimba mkuu fulani kigoma tena mwanaume baada ya kwenda kumkatia nyanya zake kule ziwa tanganyika rutale,huyo ndo juma njema kiumbe aliyetisha kwa uchawi lakini na yeye akafa kama wengine,kaburi lake ilikuwa kila likichimbwa linajaa maji mpka wakaamua wamzike hivyo hvyo kwenye maji
Duh, mambo ya Mwisho wa reliMwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
Unamuongelea Binti Rukungu?Na yule bibi aliyekufa misukule ikawa inatoka nje kufata maiti
Jina nimesahau kitu kama nyarukungu, yule wa rubuga