Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Ebu tuambie mkuu alikwambiaje
Mwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
 
Unasema yasiyo kweli, mjukuu wa kwanza wa Mzee Juma anaitwa Mahmudu anaishi Dar Es salaam. No dereva wa gari za ujenzi.
My point is mjukuu alie rithishwa mkoba wa Juma Njemba anaitwa Said na yeye alifariki wiki kadhaa baada ya arobaini ya Juma Njemba...
 
Kuanzia katikati ya miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani Kigoma aliishi " fundi " mmoja aliye julikana kwa jina la Juma Njemba.

Juma Njemba alikuwa MTU hatari sana katika masuala ya ulozi na alijikita zaidi katika kazi ya kuua watu kwa uchawi.
Mkuu ukipata muda fatilia pia habari ya BITI RUKUNGU! Huyo alikuwa gwiji hatareee pia.
 
Bila kuroga duniani utapata pesa ya kula tu ndogo ndogo na kila biashara utakayofanya utaishia kupata hasara hata kama hiyo biashara uliifanyia utafiti wa kina na tathmin miaka 1000 bado utaishia hasara. Mshana jr njoo uwarlekeze pesa nyeusi ikoje.
 
Kuna fasihi kali sana ndani ya hiki kisa Sky, yaelekea kuna Juma Njemba aneishi sasa hivi akichukua mabinti za watu(wengine sijui ni wake za watu!?) na kuwawowa huku wazazi wao au waume zao wakiufyata maana wakiinua sauti kulalamika wanapotezwa

Kwamba kifo cha Juma Njemba tunaeishi nae kitafurahiwa sana na watu kwa kufanya sherehe tena hasa na hao hao wanaojifanya kujinyenyekeza kwake na kijipendekeza kwa kumlamba miguu huku mioyoni mwao hawamkubali yeye na kazi zake za ulozi
Utakuwa mwafilosofia wewe bila shaka
 
Back
Top Bottom