Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

juma njemba? hahahahahhaa alikuwa na balaa si kitoto, wanao bisha waendelee kubisha, yupo mtalaamu mwingine anatokea mwakizega alikuwa ana balaa si masikhara, yupo binti rukungu. wapo weeengi. kuna mzee mmoja nmesahau jina lake yeye alikuwa akikunyooshea kidole basi nenda kaandike urithi kabisa, alikuwa anakunja vidole vya mikono yake yote, akivinyoosha vyoote ujue watu watano wameondoka, kula yake ilikuwa ndani tu baada ya kujizindua. wapo wale wazee wa mwamgongo na mwambao wa ziwa walikuwa na hatari si kitoto....

si vyema kuyazungumzia haya coz hayajengi
 
Binadamu wakatili jinsi hii wapo.wapo. Lakini unakuta ni 'hybrid' ya binadamu na jini katili (yaani jini anakuwa anajamiiana na binadamu anazaliwa mtoto ambaye sisi tunamwona ni mtu ila kwa uhalisia ni shetani (jini). 'Watu' wa namna hii wanaweza kujiita ni waganga wakafanya kazi ya 'kiganga' lakini ni maalum kwa kuua watu tu. Wengine wanabaki kuwa ni watu wa kawaida wanafanya kazi (hata za ofisini) lakini ni wachawi 'wakali' kuliko maelezo.

Watu kama hawa wanajibadilisha kuwa wanyama au hata binadamu ili wasababishe ajali.
Ukiwa unaendesha gari lako ghafla unaona mtoto mdogo au bibi kizee akikatiza mbele. Ukimkwepa LAZIMA gari lako lipinduke (maana ndio leo la huyo mchawi). Ndio maana unaweza kuona gari limepinduka mahali ambapo wala hakuna kona na barabara ni nzuri na wala spidi sio kali. Dereva anaweza kuona kitu ambacho wenzake kwenye gari hawakioni.

Usipomkwepa huyo bibi kizee au mtoto, ukamlenga unapopita alipo, husikii mlio wa kumgonga na ukitazama nyuma kwenye kioo cha gari lako humwoni popote. Kuna mchawi (tena mtoto mdogo tu) alishaeleza namna ambavyo yeye na bibi yake na wachawi wenzie walivyoweka jiwe zito kwenye usukani wa meli 'rubani' wa meli akashika usukani ('rudder') kuongoza meli ikakataa. Hakuna mtua aliyekuwa anawaona. Meli Ikaelekea kwenye mkondo ikapinduka wakafa mamia ya watu. Wakati meli ilipokuwa inazama wao 'walipaa' tu (maana ni wanga) wakaja nchi kavu. Huyo alikuwa ni mtoto wa darasa la tatu. Ndio mambo yaliyo duniani hayo.
 
Wacha urongo..Juma Njemba alifariki mwaka 2001 na alikufa kwa kiharusi cha kisheitwani...Chanzo cha kifo chake ni kuzidiana nguvu kati ya uchawi wake na kinga ya MTU ambae Juma Njemba alitaka kumuua kwa uchawi.

Kombora alilo piga Juma Njemba kwenda kumuua MTU huyo liligonga mwamba na kumrudia yeye mwenyewe na siku kadhaa baadae alifariki dunia...Unataka nifunguke zaidi what happened ?

Juma Njemba alipigwa Back To Sender
Wwe nae sio wa hivi hivi,hiyo ICBM iliijuaje sasa
 
juma njemba? hahahahahhaa alikuwa na balaa si kitoto, wanao bisha waendelee kubisha, yupo mtalaamu mwingine anatokea mwakizega alikuwa ana balaa si masikhara, yupo binti rukungu. wapo weeengi. kuna mzee mmoja nmesahau jina lake yeye alikuwa akikunyooshea kidole basi nenda kaandike urithi kabisa, alikuwa anakunja vidole vya mikono yake yote, akivinyoosha vyoote ujue watu watano wameondoka, kula yake ilikuwa ndani tu baada ya kujizindua. wapo wale wazee wa mwamgongo na mwambao wa ziwa walikuwa na hatari si kitoto....

si vyema kuyazungumzia haya coz hayajengi
Aiseeh!ila na wao si wamekufa Piaa!Africa bwanaa!
 
Pamoja na yote yaliyoletwa humu, nimewaza jinsi ambavyo LIKUD anamshambulia jamaa anaye mtetea mdingi wake kwa kumwita tapeli, anayetaka watu wamfate etc.

Kuna kitu naona LIKUD kama kaharibiwa dili, labda alitaka kutueleza mbeleni baadhi ya ujuzi aliochota kwa mzee ili watu wamtafute.

Ila naona ukoo umekaza imebidi akimbilie utapeli.
 
Mara siku moja akaja mzee wa heshima zake kapigilia kanzu na kofia ktk meza ya mama mmoja aliyekuwa akijishugulisha na kuuza samaki soko kubwa Ujiji. Kisha yule mzee akauliza kwa kumtaja jina la yule muuza samaki: wewe ndiye fulani (jina la muuzaji). Yule mama akaitikia ndiyo mimi baba. Yule mzee akaanza kulalamika huku akiondoka akisema watu wengine bwana huyu (fulani) sasa ana nini masikini, anatafuta riziki yake hapa. Yule muuza samaki akabaki anashangaa wakati yule mzee anaondoka huku akimlaumu aliyemsotea huyo mama.

Ndiyo watu wengine waliokuwa wakifanya biashara hapo wakamuuliza yule mama; unamjua huyo mzee? Yule mama akajibu simfahamu. Akaambiwa huyo ndiye JUMA NJEMBA. Yule mama akashikwa na khofu kubwa juu ya maisha yake ingawa mzee alikuwa tayari kapuuza kazi aliyokuwa kapewa.

Inaonekana kuna mtu alimfuata Juma Njemba ili ammalize huyo muuza samaki.
Aiseeh! Huyo alikua zaidi ya binadamu!!
 
Ni kama Brand flanihivi...Mtu mmoja anajaribu kuiharibu na mtu mwingine anajaribu kuitetea, maana Njemba katumia miaka mingi kuitengeneza Brand yake na Familia yake, anapotokea mtu mmoja akaiharibu lazima moto uwake period!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] looh
 
juma njemba? hahahahahhaa alikuwa na balaa si kitoto, wanao bisha waendelee kubisha, yupo mtalaamu mwingine anatokea mwakizega alikuwa ana balaa si masikhara, yupo binti rukungu. wapo weeengi. kuna mzee mmoja nmesahau jina lake yeye alikuwa akikunyooshea kidole basi nenda kaandike urithi kabisa, alikuwa anakunja vidole vya mikono yake yote, akivinyoosha vyoote ujue watu watano wameondoka, kula yake ilikuwa ndani tu baada ya kujizindua. wapo wale wazee wa mwamgongo na mwambao wa ziwa walikuwa na hatari si kitoto....

si vyema kuyazungumzia haya coz hayajengi

Hata mwambao Ziwa upande wa Rukwa nako kuna mafundi wengi balaa ambao wengi ni hybrid ya kalemii(DRC) na ufipa,ukiipataa hii hata ni hatari

Ile story ya kuiba mwenge wa UHURU nayo ushawahi isikia mkuu, Na kuna ile ya mwewe kubeba ng'ombe japo siiamini sana,
 
Back
Top Bottom