Juma Nkamia ampinga Rais Magufuli kuhusu miaka 7 ya Urais

Nyerere alikiri kuwa kuna watu walimpotosha kuwa Tanzania bado inamuhitaji na hivyo asing'atuke madarakani kumbe wale watu walikuwa wanatetea matumbo yao wakijua kuwa mzee aking'atuka basi nao kula yao itakwenda na maji.
Mtu kama Ngamia hana uhakika wa kuchaguliwa tena kwa hiyo anajua kuwa mda wa kukaa madarakani ukiongezwa basi ndio itakuwa pona pona yake. Ameshau kuwa uchaguzi ni takwa la msingi la kidemokrasia na utawala bora.
Kama tulivyopinga na kusema kuwa heshima ya Tanzania ni kubwa kuliko njaa ya Kimbisa, ndivyo hivyo hivyo tutakavyompinga Ngamia kwa kusema kuwa faida ya demokrasia na utawala bora ni kubwa kuliko hizo gharama za uchaguzi.
 
[emoji16][emoji16][emoji16] Ngamia eee??? Basi ukame wa jangwa utakuwa unamsumbua ndo maana.
 
Iko siku atasema tuondoe ukomo wa Rais kuwa madarakani.
 
Kwani ikiwekwa miaka 7 ndio fedha hazitatumika? Hata ukiweka miaka 10 ni yaleyale tu.
 
Maigizo ya CCM unayajua au unayasikia?? Hii inaitwa camouflage
 
Yani kuna watu wanafanya mchezo wa kijinga wakidhani watanzania wote ni mambumbumbu..

Hatujasahau hata Lowassa alitafuta watu wa kumuomba/kumshawishi agombee urais wakati ilikuwa ndoto yake ya miaka yote.

Kwani si wawe wawazi tu?
 
Kagame nae alianza na hizi ''sitaki nataka'' na mwisho wa siku akadai ati wananchi na wazee ndani ya chama ''walimbembelza'' akubali kuruhusu referendum. Nkamia hana ubavu wa kupingana na Pogba. Kuna namna hapa na wanawapumbaza tu
Unajua viongozi huwa wanawaona wanaowaongoza ni wajinga sana!
 
MKUU, INA MANA WEW HUJAKONEKTI DOTI? HUO NI MCHEZO WA KUIGZA NA WANAJUA FKA WAPGA KURA WENG NI WAJNGA..
 
Hivi wanadhani sisi na watoto wadogo hatuelewi kinachoendelea. Juzi Polepole kaenda kwa rais kisha akamwambia kwamba hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa muda. Na wala hakukuwa na mjadala wowote kuhusu hilo. Kisha leo Nkamia anajifanya kwamba atapelekea mswaada kwa spika kuona wanafanyaje ili hilo litimie. Ukweli ni kwamba anataka kuongezewa muda, ila inabidi ajifanye ameshakataa isipokuwa analazimishwa. Mbona mambo mengine anayokataza hasa ya wapinzani hakuna anayethubutu kufanya lolote na ukijaribu tu unashughulikiwa?
 
Nkamia ametoa maoni yake.
Mh Magufuli ameshatoa msimamo wake kuwa hapendelei mjadala huo ni vema tukaheshimu msimamo wa kiongozi wetu.
Hata hivyo najua watanzania wengi wangependa atawale muda mrefu zaidi ili adumishe yale mazuri anayoyafanya.
 
Yani hii ni series mjuwe kuwa series itakayo fuatia Mtukufu atakubali kuongeza iyo miaka maana wana nchi wana mtaka afanye hivyo !!! Ccm vijana ambao siyo wa lumumba tunaelewa hii game!
 
nkamia ni mwanafunzi wa magufuli sengerema sec
 
Mzee Mkapa angekaa miaka 7, na Mzee Kikwete angekaa miaka 7 , leo hii Rais wetu JPM bado asingekuwa madarakani. Maendeleo tunayoyaona leo hii sababu ya JPM bado yasingekuwepo. Nkamia aache kujipendekeza na asitake kutuharibia nchi kwa uroho wake. Mfumo wa miaka 5 kwa muhula mmoja unafaa sana na udumishwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…