Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Juma Nkamia: Hayati Magufuli alitaka nifukuza CCM, kwakuwa alipenda sifa nikaja na hoja ya miaka 7 ya Urais

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

Pia soma
4CD39811-B5A2-498D-931A-70D18D4789EF.jpeg
 
Angebaki na msimamo wake hata kama angefukuzwa chamani angeheshimika zaidi, lakini kitendo cha kutaka Magufuli atawale miaka saba ili kujikomba kwake ndio alijivua heshima yote.

Atambue hata wale wengine waliofukuzwa CCM kwasababu ya misimamo yao walikuwa na watoto pia, lakini waliondoka ili kulinda heshima zao.
 
Wala tumsimsikilize huyu hayawani mkubwa. Yaani katika watu walikuwa wanampa kiburi cha kuongeza ukomo wa utawala Magufuli mmoja wapo ni Juma Mkamia.

Siwezi kumsamehe
 
Hivi huyu jamaa alirudi bungeni 2020?
Si unaona saa hizi anatafuta nafasi ya kufikiliwa 2025. Maana saa hizi ukitaka upewe nafasi huko we mponde Magu.

Hivi karibuni ummy mwalimu alitrend sana lakini alipomsifia mwendazake kupitia msd walivyoisimamia kwa sheria inayotumika sasa na ikafanya vizuri amepotezwa kabisa.

Mama kaona huyu kumbe sio mwenzetu. Sie tunapambana kuzima moto wa Magu ye anachochea kuni.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

View attachment 2216559
rubbish
 
Ni laana kuwa na nchi yenye watu wajinga afu watu hao ndio wanakuwakilisha kwenye chombo cha juu cha uwakilishi wa wananchi. Sasa hapa Nkamia anamuexpose Magufuli au anajiexpose yeye mwenyewe na ujinga wake kuonyesha jinsi yuko tayari hata kujiuza kwa ajili ya tumbo lake?

Watu kama Nkamia ndani ya CCM wapo kibao na Magufuli aliwacheki sometimes aliwabufua for what fools they are, sometime aliwapuuza na sifa zao za kinafiki. Kazi ipo kwa maza kama akidhani wanaomponda Magu leo basi ndio wema kufanya nao kazi.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Chemba mkoa wa Dodoma amenukuliwa na Dar Mpya (blog) akisema kuwa alikataa Muswada wa Habari ambao ulilenga kuweka mazingira magumu kwa waandishi wa Habari.

Namnukuu

Magufuli alitaka kunifukuza @ccm_tanzania baada ya kukataa muswada wa habari ambao ulilenga kuwakandamiza waandishi wa habari. Mimi nina watoto na wanasoma,Kujinusuru nikaamua kubadili gia angani nikaja na hoja ya miaka saba na kwakuwa mzee alipenda sifa kesi ikaisha"

View attachment 2216559
Eeh kumbe ilikuwa ni njaa..[emoji23].. Kwahiyo alifanya hivyo ili kuchumia tumbo.. Hoja ingepita je!?[emoji848][emoji2827]
 
Back
Top Bottom