Juma Nkamia, kauli yako kuhusu Mecky Mexime haijanifurahisha

Nkamia mburula tu huyu jamaa, mbona wakati akina kaburu na mwenzake Malinzi wanabadilisha kanuni ya kadi 3 za njano kwa mchezaji kuchagua mechi za kucheza mbona hakutia neno!??
 
Kama alitoa kauli hiyo nadhani aliteleza tu na ni vizuri kama ni muungwana akaomba radhi hadharani.
 
Nkamia katoa kauli hiyo baada ya kuulizwa maoni yake juu ya uteuzi wa Mexime.. Sasa maswala ya kadi 3 za njano yanakujaje hapa?.. Na kwani kuna mwandishi alimfuata na kumuuliza, akagoma kutoa mawazo yake.. Au alitakiwa aitishe press conference na kutoa tamko?
 
Ndio maana SA watu wanabomoa masanamu ya wakoloni wabaguzi maana wanavyoendelea kuyaona yanawaongezea uchungu. Huenda na hapa tukatumia mbinu zinazofanana na hizo pale wenye akili watakapoanza kujiuliza nani na nai walipataje uwaziri au nafasi za uongozi wa umma!
Kwani huyo kocha wa Ujerumani ana miaka mingapi mpaka anachukua kombe la dunia!?
 
Kwani kina Di mateo, Andre vila boaz ni watu wazima hao mbona wamefanya wonders......tatizo la kuwapa uwaziri watu wasiokua na mbele wala nyuma wanaishia kuropoka tu kama bata
 

Mbona Na Wewe Ulichokiandika Hapa HAKIJATUFURAHISHA? Na Wewe Nakushauri Uache Kufanya Mambo Kwa Mazoea Na Ki POPOMA.
 
Sasa naanza kumuelewa Boko kwenye ule waraka wake aliposema makocha mbinu za kizamani,marefa na maamuzi ya kizamani,ligi ya mtindo wa kizamani,viongozi ubunifu wa kizamani...hakumalizia moja tu "mashabiki nao wakizamani"...kama ni ukongwe Kingunge anafaa kuwa Raisi wa Tanzania
 
Mhhhhh hapana labda nkamia naye alikuwa kajitoa ufahamu wakati akijibu swali hilo.
 
Basi apewe kingunge hiyo kazi maananadhani anamzidi hata huyo kibadeni....
 
Viongozi wa aina ya Nkamia ni mizigo kwa taifa maana hawajui hata vigezo kwenye vitu vya msingi!
 

Mpeni Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…