Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akihojiwa katika kipindi cha Jambo (TBC 1) cha leo tarehe 5/6/'15, waziri mwenye dhamana ya michezo nchini ametoa maoni yake kuhusu kocha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars- Mecy Maxime kuwa hafai kwa sababu bado mdogo, na kama angeulizwa yeye kuhusu kocha msaidizi angependekeza mtu kama Abdalah Kibadeni.
Kwangu mimi, naona hoja yake haina mashiko kwa kuwa kazi ya ukocha si ya kubeba matofali, bali ni ujuzi. Wapo kina Pep Guardiola ni vijana na wanafanya vizuri. Hata hao aliowataja yeye kuwa wanafaa wamekuwa makocha siku nyingi lakini sioni kigezo cha kuwapa timu ya taifa kwa kuwa hakuna jipya walilowahi kufanya hadi kustahili nafasi hiyo.
Namshauri waziri aache kufanya mambo kwa mazoea.
Kama inshu ni Ujuzi;
Abdalah King Kibadeni ni kocha ambae yupo kwenye gemu tangu kitambo. Ameanza kufundisha soka mwishoni mwa miaka ya 80 ambapo Maxime alikua chekechea. Katika miaka yote hiyo amefundisha timu za vijana, timu za ligi kuu, timu ya taifa.. na pia anamiliki akademi yake mwenyewe.
Kama inshu ni Mafanikio;
Abdalah King Kibaden Mputa ni kocha pekee mzawa toka Tanzania mwenye mafanikio makubwa katika michuano ya Africa.. kwani aliifikisha fainali Simba Sc katika kombe la Shirikisho mwaka 1993. Amechukua kombe la chalenji jijini mwanza akiwa na timu ya taifa. Hapo sijataja idadi ya makombe ya ligi kuu, klabu bingwa africa mashariki aliyochukua.
Sasa kwa CV hii jamani, unapataje uthubutu wa kumlinganisha huyu "gwiji" Abdalah King Kibaden Mputa na "mwanae" Maxime??? Inabidi ujitoe akili ili ufanye mlinganyo huo.
Ni vyema Maxime alivyopata "shavu" la kuonja ukocha wa timu ya taifa.. ila ni kosa la jinai kusema Maxime ni bora kuliko Abdalah King Kibaden Mputa.