Mbunge wa jimbo la Chaani Mhe, Juma Usonge ameendelea na utoaji wa vyakula kwa wanafunzi wa watahiniwa wa kidato cha pili skuli za Sekondari Jimbo la Chaani wilaya ya kaskazin A Unguja.
Usonge amesema ikiwa yeye ni kiongozi wa jimbo hilo na mdau mkubwa wa elimu amesema utoaji wa sadaka iyo ni mwendelezo wake tangu aingie madarakani katika jimbo hilo na atahakikisha anaendelea kuwapa nguvu wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao ya maisha.
Ameyasema hayo leo huko skuli ya sekondari Chaani katika ziara yake ya utoaji wa sadaka ya vyakula kwa wanafunzi wa kidato cha pili wanaotarajiwa kufanya mitihani yao tarehe 11-11-2024, hivyo ametoa wito kwa wanafunzi kuzingatia waliyo fundishwa na kuwa na nidhamu,utii na juhudi katika kutafuta elimu kwani ndio njia ya mafanikio.
Mbunge Usonge ametoa mchele,mafuta na harage zaidi ya skuli nne za sekondari zilizopo katika jimbo hilo na kuahidi kuendelea na zoezi hilo kwa misingi ya kutatua changamoto ya vyakula katika kambi za wanafunzi jimbo hilo.
Kwa upande wao wanafunzi wameshukuru na kumpongeza mbunge kwa msaada huo kwani utawawezesha kujiandaa vyema na mitihani yao ya mwezi unao kuja kwa hali ya amani na usalama kabisa.
Katika ziara hiyo Usonge aliongozana na viongozi wake wa Wadi na jimbo katika kuwatembelea wanafunzi na kuwashajiisha kusoma kwa bidii zaidi ili wafikie malengo yao na kuacha mambo yasiyo wahusu katika umri wao.