Jumaa Aweso waziri wa maji: Malalamiko dhidi ya Mtuwasa kuto kulipa vijana wasoma mita za maji kwa zaidi ya miezi mitano

Jumaa Aweso waziri wa maji: Malalamiko dhidi ya Mtuwasa kuto kulipa vijana wasoma mita za maji kwa zaidi ya miezi mitano

Mr Kipe255

Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
37
Reaction score
2
Ndugu Kiongozi,

Sisi ni Kikundi cha Vijana wa Kusoma Mita za Maji katika Wilaya ya Mtwara, kilichosajiliwa kisheria na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani chini ya Ofisi ya Mkurugenzi.

Kikundi chetu kilipata fursa ya kuidhinishwa na Mamlaka ya Maji Mtwara (MTUWASA) kutekeleza kazi ya usomaji wa mita kuanzia Agosti 2023 hadi Juni 2025, ambapo mkataba wetu ulisitishwa kufuatia maelekezo ya Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso.

Wakati MTUWASA inasitisha mkataba huo mwezi Juni 2025, Mamlaka hiyo tulikuwa tunaidai malipo ya nyuma ya zaidi ya miezi mitano. Kutokana na deni hilo, MTUWASA walisaini makubaliano ya maandishi ya kulipa malimbikizo hayo ndani ya kipindi kisichozidi Miezi minne (4), kuanzia Julai hadi Oktoba 2025.

Pamoja na kuwepo kwa makubaliano hayo ya kisheria, MTUWASA wameshindwa kulipa deni letu hadi sasa tunapozungumza (Oktoba 2026).

Kama kikundi, tumefanya jitihada kubwa za kufuatilia haki yetu katika ngazi mbalimbali za uongozi bila mafanikio. Tumeshawasilisha malalamiko yetu rasmi katika ofisi zifuatazo:
1. Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
2. Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mikindani.
3. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
4. Mfumo wa Kidijitali wa E-Malalamiko wa Wizara ya Maji.
5. Mfumo wa Kidijitali wa E-Malalamiko wa Wizara ya Vijana.
6. Mfumo wa Kidijitali wa E-Malalamiko wa Wizara ya Ajira na Kazi.

Tunaamini kwa dhati kuwa, kupitia ujumbe huu wa wazi kwako kama kiongozi mwenye dhamana kubwa katika sekta hii, utaingilia kati ili sisi vijana tuliotumikia sekta hii kwa weledi, uaminifu na utiifu mkubwa tupate haki yetu tunayoidai MTUWASA ndani ya muda mfupi.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
Kikundi cha Vijana Wasoma Mita – Mtwara.
 
Back
Top Bottom