Jumamosi+Jumapili=!?

Jumamosi+Jumapili=!?

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
11,605
Reaction score
1,843
Vijana wawili walikuwa wakivuta bangi, lilipo wakolea wakawa wanabishana kuhusu siku... mmoja anasema kuwa leo ni Jumamosi na mwingine anasema kuwa ni Jumapili...

Walipokosa jibu wakaamua wamuulize mtu yeyote atakaye pita mbele yao...
Kwa bahati akapita jamaa, nao bila ya kusita wakamuuliza...;
Eti leo ni jumamosi au ni jumapili maana tunabishana sana, Mie nasema Jumamosi na mwenzangu anasema kuwa leo eti ni Jumapili?

Yule jamaa akamjibu; Kwanini m-bishane si mfanye kuwa leo ni jumatatu tu.

Wakamuuliza kwanini hiwe Jumatatu banaaa...!?

Nashangaa kuona mnabishana wakati nyote mpo sahihi... Hizi siku mbili ziunganisheni na kuwa siku moja kwa hiyo Jumamosi + Jumapili = jumatatu. Mnaonaje!

Wavuta bangi wajibu... Poa mtu wetu... mambo si hayo bana...leo Jumatatu!
 
Back
Top Bottom