Uchaguzi 2020 Jumamosi ya tarehe 10 Oktoba itakuwa siku ya kutamaniwa na makundi mengi kumsikiliza Tundu Lissu baada ya kufungiwa kufanya kampeni

Uchaguzi 2020 Jumamosi ya tarehe 10 Oktoba itakuwa siku ya kutamaniwa na makundi mengi kumsikiliza Tundu Lissu baada ya kufungiwa kufanya kampeni

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Baada ya Mgombea Urais kupitia CHADEMA kukaa kimya kwa siku kadhaa, jumamosi hii ataendelea na kampeni Kama kawaida, siku hii itafuatiliwa na mamilioni ya watu duniani kote kwani Kila mtu anaitaji kupata ufafanuzi zidi ya masuala kadhaa yaliyojitokeza kipindi yeye akiwa kimya.

Lakini katika kipindi hiki akiwa ametulia, ndipo anapokea taarifa nyeti za mikakati ya tume na ccm kuvuruga uchaguzi, hivyo mpaka anakuja kuzungumza, watatamani kumfungia tena kitu kisichowezekana tena.

Kuna masuala yanahitaji ufafanuzi ikiwemo
- Hutuba ya Mgombea Uraisi kupitia CCM kule Zanzibar kuhusu masuala ya Muungano.
- Kuhusu walimu ngazi ya cheti.
- Kuvamiwa kwa ofisi za CHADEMA kanda ya Serengeti na Arusha.
- Waraka wa mwanasheria wa Lissu bwana Robert Amsterdam na effect yake kwenye uchaguzi huu.

Na mambo mengine mengi, bila Shaka, T. Lisu kwasasa ndiye mbeba maono ya wananchi wengi, kwani watu wengi wamechagua harakati za HAKI, UHURU na MAENDELEO ya WATU kuliko harakati za MAENDELEO YA VITU bila kujali HAKI NA MAENDELEO YA WATU( Unafuu wa Maisha ya mtu mmoja mmoja.
 
Walimu wana jambo lao..!
Wamedanganywa Leo na mgombea kwamba stashahada ni tamko la Kipumbavu la Naibu katibu Mkuu, kumbe Ilani ya Chama chao inatamka wazi walimu wa ngazi ya Cheti hawana chao tena.

IMG-20201005-WA0057.jpg
 
Walimu wana jambo lao..!
Wamedanganywa Leo na mgombea kwamba stashahada ni tamko la Kipumbavu la Naibu katibu Mkuu, kumbe Ilani ya Chama chao inatamka wazi walimu wa ngazi ya Cheti hawana chao tena.View attachment 1591519
Dah, kwahiyo aliyeandaa ilani hajui hata yaliyomo? Utekelezaji wake utakuwa palepale.
 
Lissu ni mtumbuizaji tu. Sio ajabu watu kuvutiwa na mtumbuizaji. Full comedy...
 
Sawa, ngoja Tunasubiri tumtie moyo ktk mipango yako na kumpa kura kadhaa. Km hapa kwangu wengi wameahidi kumpa tu kwa huruma yaani.
Lissu ni mtumbuizaji tu. Sio ajabu watu kuvutiwa na mtumbuizaji. Full comedy...
 
CCM; ile sera yenu ya Tanzania ya viwanda bado ipo? Mbona siisikii tena ikitajwa na wagombea wenu? Mnatueleza nini sisi wapiga kura wenu mliotuahidi 50 million kila kijiji? Tuendelee kusubiri au tumeliwa?
 
Akirudi kwenye kampeni mgombea wa Chadema asiiseme vibaya tume.

Namshauri awe kama mgombea wa CHAUMA yeye anajali sera za chama tu
 
Queen Sengiga wa ADC anahoja za msingi kuliko Tundu Lissu. Chadema jifunzeni kunadi sera zenu na sio matusi na kejeli.
 
Aje na majazba yake, apigwe knock out mpaka Oct 28.Hasira zake azielekeze kwa Mwenyekiti faru John,na sio kwa JPM kipenzi cha watanzania wote.
 
Namtakia Lissu tafakari njema na mapumziko mema arudi kwa kishondo kikuu kumuangamiza nduli wa ccm.
 
Sawa, ngoja Tunasubiri tumtie moyo ktk mipango yako na kumpa kura kadhaa. Km hapa kwangu wengi wameahidi kumpa tu kwa huruma yaani.
Uchaguzi huu Chadema wameshashindwa kwa mara nyingine. Wajipange upya kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.
 
Na nashauri akaanzie moshi. Leo nimemsikia mwanachama mmoja wa ccm kwamba viongozi wao wanawaambia kwamba wanaohudhuria mikutano ya Lissu hawatampa kura. Sasa akawa anauliza hivi ni kweli lisuu umati wote anao kutana nao wasimpe kura?.nilichomjibu achana na ujinga huo,lowassa walisema hivyo na kapata kura 6 kwa milioni 8. Na watu wanamwamini zaidi Lissu kuliko magu,kwa sababu magu amedanganya sana,
 
Back
Top Bottom