Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Mpo salama!
1. Kesho ni Siku ya kwenda kuabudu kwa madhehebu mengi ya Kikristo yakiongozwa na Kanisa Catholic na KKKT.
2. Kwa hapa Tanzania Kanisa Catholic ndio kanisa Kubwa lenye waumini wengi. Lakini pia ndilo Kanisa Mama linalobeba Makanisa mengine ya Kikristo.
3. Kanisa hili neno au tamko Lao linaathari moja kwa moja kwenye taifa na Jamii ingawaje sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuliona Jambo hilo.
4. Wale Masheikhe waliosema Kanisa Catholic kwa nini hawajatoa tamko lolote mpaka sasa la kupinga maandamano Wana hoja na wanajua Kanisa hilo linaushawishi na nguvu.
5. Hata mimi nashauri ni muhimu kwa Catholic kutoa tamko la namna yoyote ilimradi kutuliza hasira na chuki za wanaotaka kuandamana. Tamko Lao litapoza kwa namna moja ama nyingine.
6. Ni muhimu kujinyenyekeza na busara itumike kuliko kutunishiana misuli ili kuonyeshana Nani mwenye nguvu.
7. Kimsingi maslahi ya taifa na Watanzania ni muhimu zaidi.
8. Wote tunategemeana.
9. Lakini pia Kama nilivyosema serikali ipige marufuku masheikhe au baadhi ya watu wanaojitambulisha kama Waislam kurusha maneno na kejeli kwa Kanisa kwani huko ni kulikosea kanisa heshima na kukuza mgogoro na chuki.
10. Kuwaruhusu watu wa aina hiyo bila kuwapiga marufuku na serikali kuisema tuu TEC itabeba tafsiri isiyo nzuri. Wahadhiri wa dini ya kiislam wakemewe wazungumze kuhusu uislam wao na kama Wana haki wanazitaka waiambie serikali yenyewe na sio kutaja dini zingine.
11. Serikali haina dini lakini watu wake almost Wana dini. So sio rahisi kupuuza dini na chuki za kidini. Kwani zinahatarisha umoja wa kitaifa.
12. Kanisa Catholic ni muhimu nanyi kutumia busara ingawaje madai yenu ni kweli kabisa na serikali inapaswa iyafanyie kazi.
13. Mmefundishwa kusamehe Saba mara sabini. Pia mnafundisha waumini wenu hivyo. Fundisho hilo litumieni hapa kwenye wakati huu.
14. Tunajua binadamu kwenye imani yupo radhi asaliti chochote kile. Jambo hilo msilitumie vibaya kulivuruga taifa.
15. Haki ni muhimu Sana kama mlivyosema lakini Upendo ni muhimu zaidi. Wapendeni wanaowaudhi hiyo no kanuni ya Kristo.
16. Ni Muhimu serikali ifuatilie madai yanayotajwa hasa Yale muhimu na lalamiko kuu. Suala la utekaji ni suala ambalo sio zuri na linaleta utamaduni mbaya ndani ya taifa letu. Utamaduni huo ni hatari kwa sababu ukizoeleka sio ajabu Siku moja ukasikia kiongozi mkubwa wa serikali hajulikani halipo. So kwenye utekaji hakuna aliyesalama.
17. Kufikia hapo sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam