Jumapili Desemba 7 Mapadri na Askofu wa Kikatoliki ni muhimu wazungumzie Amani kuliko Haki

Bila HAKI kutafuta AMANI ni kujisumbua tu maana ukitafuta AMANI matokeo yake utapata UVUMILIVU tu na AMANI huwezi kuipata.
 
Amani hustawi zaidi kayika Haki. Hata Mungu anaitwa Mungu wa Vita, Mungu wa Haki.
 
Viongozi watuambie wajibu wao na haki zao
Na kisha raia aambiwe wajibu wake na haki yake.
Tuone kama kutatokea vurugu
 
Muwe mnafuatilia mambo siyo kuropoka. Huu ni utawala usiopokea ushauri wowote. Ukitaka kutekwa, kuuawa au kubambikiwa kesi ya uhaini, toa ushauri wa kuwataka watawala waache dhuluma au kuteka na kuua watu.

Ukumbuke kuwa viongozi wa dini zote kabla ya ule uchaguzi bandia, walifanya kikao, ambacho katibu wake alikuwa Father Kitima, wakatoa ushauri na mapendekezo yao. Kilichofuatia, huyo mtu wenu alitupa jalalani ushauri, kisha akaagiza watu wake kumwua Fr Kitima, Mungu akaonesha ukuu wake kwa kumlinda Father Kitima. Utawala wa awamu hii, hawasikilizi ushauri wa yeyote isipokuwa wa wahuni walioteka madaraka ya wana.
 
Nilikua nakuona kwa mbali upo kama da Mau ila hii comment imenihakikishia ni mwenyewe..!!
 
Taikoni ni msaliti wa Tanganyika nyuzi zako tuombe msamaha
 
Mkuu! kajaze kitu kwenye kichwa chako, hamna kitu humo. HAKUNA.
 
Kwamba unataka na kanisa letu lianze kuhubiri ya kinafiki kama wale mashekh wenu wa BAKWATA kwa ajili tu ya kumfurahisha yule KILAZA wa kizanzibari ambaye anaitawala nchi kwa kumwaga damu za watu kila kukicha? Wewe jamaa siku hizi umekuwa mtu wa ovyo sana.

Kwanza una habari kun jaribu la kumteka Father Kitima limefanyika jana usiku, na wahusika wameshtukiwa?

Sasa katika mazingira kama haya tutaanzaje kuhubiri amani? Hiyo si itakuwa ni dhambi ya unafiki na uwoga ambayo adhabu yake kwa Mungu ni kuchomwa na moto wa milele.

Acheni ujinga wewe, TEC wataendelea kuhubiri haki mpaka kiama haijalishi wanakutana na vitisho vingapi.

Mama yenu juzi alionesha kugadhibishwa na idadi ya matamko ya TEC na wala haumizwoli na kile kinachohubiriwa na TEC, yaan anachotaka afanye maovu kadri anavyojiskia ikiwemo kuua maelfu ya watu wasio na hatia kwa sababu zake binafsi, halafu wote tukae kimya kama hakuna kilichotokea eti kulinda amani, si upumbavu huo? Naona na wewe unataka tuufanye huo upumbavu.
 
Basi ushakuwaga mjinga mtibeli wala hatuna haja ya kukusoma tena
 
We kaa na usabato wako, nyie jumamosi wachungaji wenu wamewaeleza Nini, huko ushauri ungetoa kanisani kwenu
 
Usiwafananishe TEC na wahadhiri wale. TEC imeagatoa tamko lake inatosha. Hayo maigizo ya kuomba amani bila haki hayana nafasi ndani ya kanisa katoliki...wanasimama na ukweli na wako tayari kuufia ukweli huo...so kama itasikia kuhusu maandamano basi itakuwa ni suala la amani kama tunda la haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…