Jumapili Desemba 7 Mapadri na Askofu wa Kikatoliki ni muhimu wazungumzie Amani kuliko Haki

🚮
 
Kama mnaamini hilo kanisa lipo JF linasubiri maandishi yenu ili lifanye maamuzi sawa. Na serikali imeshaamua next step kwa kuweka askari mitaani, haijasubiri maandishi ya humu.
 
Ubinafsi ni sumu mbaya sana, wao wanajiwazia wao tu na sio wanaowaongoza. Huyo kijana ni mpishi sijui ni kwenye taasisi gani. Anaona ni vyema kutetea uovu unaompa kula jana na leo bila kujali maslahi ya kizazi chake kijacho na watanzania wengine kwa ujumla.

Wanajitoa ufahamu sio kwamba hawajui kuwa wanachofanya ni makosa. Sijawai kuona serikali ya ajabu ndani ya nchi kama hii ya sasa, imekumbatia uozo na uovu bila kujali raia wake.

Wao wimbo wao ni amani tu, haki isitendeke, yasiyofaa yote yaendelee kuwepo na kupewa nafasi kwa sababu ya amani ambayo kimsingi haipo.
 
Madai yao mnayajua, kwanini msitekeleze na wao watakaa kimya wala hamtowasikia....
 
Mkuu kwahiyo kobazi wenzako wanaoshikisha watoto ukuta na wako na watesi wa wananchi ndo wanakufurahisha ila wanaodai haki wanakuudhi?
 
Mimi sijaongelea demokrasia, maana hiyo ni subjective na jamii husika,niliongelea haki.

Hata Haki zipo ambazo ni subjective.
Lakini zipo Haki ambazo ni lazima kwa binadamu zote mfano Haki ya kuishi.

Haki nyingi za kitamaduni ni subjective.

Kuna haki kulingana na Wakati.
Mfano haki ya wakati huu inaweza isiwe haki kwa wakati ujao.
Mfano haki za kitamaduni nyingi zinabadilika kulingana na nyakati kama haki ya kumiliki Mali, haki ya kuoa wake wengi, haki ya kutolewa mahari. N.k
 
 

Attachments

  • IMG_0172.jpeg
    135.1 KB · Views: 19
Ko unapendekeza maandamano yasiyo na kikomo mpaka haki ipatikane? Maana Yake vita ndio suluhu ya wakati huu?
Hivi kwanini mnataka raia tu ndio tukubali kutawaliwa na tusiowataka..
Kwanini wao wasitusikilize sisi, kwani katika madai ya raia ombi lipi baya.

Mfano kwangu mimi, kwa haraka haraka
Nataka
katiba mpya.
Uchaguzi huru na wa haki.
Uwajibikaji.
Matumizi ya serikali yadhibitiwe.. mishahara kwa wabunge na mawaziri ipunguzwe,
Wale wabunge karibia 125 wasiochaguliwa wasiwepo
Kununua magari ya kifahari kufutwe na pesa hizo ziende kwenye maendeleo.
Na mengineyo mengi.

Je hapa lipi ni baya?
 
ujinga gani huu. Kwanza inatangulia haki ndio inafuata amani. Huu ujinga wa kusema amani kwanza ndio ifuate haki ni ujinga. Wakoloni wote wazungu na waarabu walitutangulizia dini. Wakahubiri amani amani huku waarabu wakituburuza utumwa tukibebeshwa bidhaa toka mwisho upande mmoja wa nchi yetu hadi pwani. Bidhdd zikauzwa na sisi wenyewe tukanadiwa kama bidhaa. Wazungu nao wakatuletea dini yao tukahubiriwa amani amani huku wenyewe wakitunyang'anya ardhi yetu yote yenye rutuba madini nakila mali asili huku wakitutumikisha sawa watumwa.
 
Hata Haki zipo ambazo ni subjective.
Lakini zipo Haki ambazo ni lazima kwa binadamu zote mfano Haki ya kuishi.
Hakika, sasa ilikuwaje watu wakauliwa kama kuku, halafu mpaka sasa hii serikali haramu haijakubali ilichokifanya?
 
Kama ni msomaji wa Neno la Mungu soma; Matendo 5:29 "Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu", ..mara kadhaa Petro alikabiliana na matukio yaliyomtaka aseme maneno kuwafurahisha watu..lkn hayo ndiyo yalikuwa majibu yake kwao..soma pia, I Samweli 15:22...kutii ni bora kuliko dhabihu..Kuhani Samweli alimkumbusha Mfalme Sauli pale alipodhani ni muhimu kuwapendeza wanadamu katika maamuzi yake lakn alikosea..maana yangu ni hii, Maaskofu wanatumia muda mwingi kuongea na Mungu na hivyo wanapewa ujumbe kwa ajili ya watu..hayo unayosema wayaseme hayana muhimu km si ujumbe unaotoka kwa yule wanamtumikia! jifunze kukumbuka..
 
Wewe unajizima data Pengine ni mnufaika WA huu utawala,lakini ukweli uko wazi na unaujua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…